TANZIA Prof. Nkunya wa TCU afariki dunia


..Umesema wazee kinga zao za mwili hupungua.

..kama hoja hiyo ni ya kweli basi wao ndio wanaotakiwa kupewa chanjo kwanza.

..vijana ambao kwa kawaida kinga za miili yao ziko juu wao hawana ulazima wa kupewa chanjo.

..hata bima ya afya kijana anaweza asikate, lakini mzee ni busara zaidi akawa nayo kutokana na kushambuliwa mara kwa mara na maradhi.

..kama hatuamini chanjo za mabeberu, na maadui zetu wa kizungu, kuna chanjo zilizotengenezwa na ndugu zetu wa UCHINA.

..binafsi nasisitiza watu wajikinge kwa kuvaa BARAKOA na kuepuka kushikana mikono. Hili nadhani kila Mtanzania anaweza kulizingatia.
 
Kusema kweli mm huwa nayatukanaga mabavicha tu mavijana ya CDM yakizingua....
manake yale ni dk 1 mbele, nikikutana na wazee kama Toxo hapo juu huwa napita vile....
 
Hajakufundisha huyu?ooh sorry kumbe wewe umesoma SAUT

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahaaah wapi! Hajui zile corridors zetu. Nothing personal! Ila kuna watu wana degree zao za SAUT na MBA za Mzumbe Vodavasta, halafu kuna vitu vingine tuna-set the bar too high, hawa watu hawako na sisi.

Namkumbuka Prof. vizuri. Tulikutana na kuongea enzi za ujana wangu. Yeye alikuwa Prof mimi ndio hivyo.
Kwa umri wetu, well, wengi tuko njia moja. No regrets, we lived our lives.
 
Bams, pia naomba hawa Wazee wetu wawe wanatuasa na kutulisha maneno ya Hekima na Busara, pindi wapatapo wasaa wa kufanya hivyo! Litakuwa ni jambo la Kheri na Baraka kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu!
 
Poleni sana Mkuu.
 
Ndugu zangu, kumbe wengi mna'testimony' kubwa kuhusiana na hili janga la Corona![emoji848] Kwakweli inatubidi kuchukua tahadhari kubwa sana na kujikinga dhidi ya ugonjwa huu! Poleni sana kwa wote mliokabiliana nao moja kwa moja au kufiwa na ndugu zetu![emoji19]
 
Poleni wafiwa, Poleni wana taaluma...academicians/scholars alinifundisha Chemistry miaka hiyo.......99% ya vijana wa humu JF hamjazaliwa

basi alitakiwa awe ameshastaafu

kazi za mikataba zinawaua maana hawapumziki

graduates wamejaa mitaani, kwa nini wazee wapewe mikataba ya maisha ?????

angalau kuna kijana sasa atapata ajira
 
Elimu yako kwenye chemistry au ujenzi wa madaraja upoje.
Kuna Yule mbobezi wa uchumi US aliondoka kazini akiwa na miaka mingapi ?
Au nyinyi ndio ma lecturer mnaotoa degree za nyumba za wageni au karatasi za course work zinakuwa ni "godoro"
Silence is golden if you have nothing to say
 
Aise, humu kuna wazee wetu. Tujifunze kubishana kwa hoja coz usipokuwa makini unamtukana mzazi wako yani.
 
basi alitakiwa awe ameshastaafu

kazi za mikataba zinawaua maana hawapumziki

graduates wamejaa mitaani, kwa nini wazee wapewe mikataba ya maisha ?????

angalau kuna kijana sasa atapata ajira
Haiwezekani kijana aliyegraduate juzi kujaza nafasi ya Profesa mbobezi.
Thats a fact of life.
 
Not so fast!
Omba na kusali.
Mungu ni mwema.
Mwinyi anakaribia 100 na anadunda!
 
Haiwezekani kijana aliyegraduate juzi kujaza nafasi ya Profesa mbobezi.
Thats a fact of life.
Nani kasema graduates maana yake ni vijana walio graduate juzi ???

Watu wanatembea na ma vyeti yao mtaani miaka kibao kwa sababu serikali inatoa ajira za mikataba kwa wazee wanaotakiwa kukaa benchi!

Kwa nini ?

What was so special about Mzee Mfugale’s experties mpaka afie kazini kwa ajira za mkataba?

MFUGALE BRIDGE

 
Kwani lazima uajiriwe?
Huo ni ulemavu wa kufikiri.
 
Kwani lazima uajiriwe?
Huo ni ulemavu wa kufikiri.

kwani lazima hivi vikongwe viendelee kuajiriwa hata viki staafu ?

huo ni ubinafsi na ulemavu wa fikra, kushindwa kuelewa kwamba damu changa pia inahitajika kuwa groomed for tomorrow’s professors
 
Kinga dhidi ya COVID-19 bado iko kwenye hatua za awali za utafiti na hakuna nchi yoyote iliyofanikiwa kuwa na chanjo ya uhakika iwe huko uchina au hata ubeberuni.

Dunia nzima imejazwa hofu na kutoa mwanya kwa wajasiliamali wa makampuni ya madawa kuingiza sokoni bidhaa ambayo haijathibitika ubora wake, lakini wakati inatumika kwa binadamu watu hawa wanaendelea na utafiti. Kimsingi kwenye chanjo hii kwa mara ya kwanza inajaribiwa kwa binadamu moja kwa moja.

Kuzeeka kunakoonekana kwa macho ni kuzeeka kule kule kunakotokea ndani ya mwili wa binadamu kwenye ngazi ya chembe hai za mwili, kwa hiyo uwezo wa mwili kujitengenezea kinga unapofikia miaka sitini au zaidi hupungua kwa kiasi fulani na hapa ndipo ulipo mjadala mkuu na maswali kama uliyoyauliza wewe hapo juu hata kwa Dunia nzima.

Ieleweke kuwa kinga ya mwili imegawanyika katika sehemu kuu mbili, ile ya asili na ile ya kupasishwa. Hii ya asili Ina uhakika wa asilimia 80+ wakati hii ya kupasiwa Inacheza kwenye asilimia +-20.Kwa maana hiyo kinga ya asili ndio tunayopaswa kuiamini zaidi huku tukizingatia masharti ya afya ya jamii ikiwemo kuvaa barakoa.

Pamoja na utambuzi wa mfumo wa kinga mwilini, binadamu amekuja na ugunduzi wa kutengeneza kinga aidha ya asili kwa kumuambukiza binadamu vimelea vilivyofubishwa Ili mwili utengeneze kinga dhidi ya vimelea husika au vimelea vipandikizwe kwa mnyama anayefanana na binadamu kibaiolijia ili mnyama huyo atakapotengeneza kinga yake, hiyo itumike kwa binadamu kumkinga na ugonjwa uliokusudiwa.

Mchakato mzima wa utafiti huu huchukua miaka mitano hadi kumi ili kuja na jibu la uhakika kuhusu chanjo madhara yake na namna ya kuyadhibiti. Chanjo zinazotolewa sasa kwa mashinikizo tena kwa mashindano kati ya Magharibi na mshariki hazikukidhi vigezo vya kawaida na kutia shaka, lakini hazijathibitishwa kuwa na ufanisi hata huko ulaya walikochanjwa.... Watu wanalalamika kuambukizwa na kufa ingawa habari hizo hazisemwi sana huku kwetu.

Bado narudia tena kusema kuwa taasisi zetu za afya na hasa Mloganzila na Muhimbili, watalaamu wake waliosoma Biotechnical Engineering, Biology na Microbiology, Biochemistry na ma MDs, waingie chimbo kutafiti virus hivi vya COVID-19 kwani ni ugonjwa mpya ulioko kwenye tafiti kwa sasa... Tusitegemee eti wazungu wanajibu kwa sasa zaidi ya kuwa silaha ya maangamizi.

Uwe na siku njema mkuu Joka Kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…