Du!... Kwanza hujanitendea haki kwa kuniita zumbukuku wakati bandiko langu lina lengo fikirishi. Mtu ana miaka 60 na kinga ya mwili kwa umri huo huanza kupungua, chanjo anayopewa itamlinda vipi wakati mwili wake umepunguza kazi ya kujilinda?. Naamini una uwezo wa kutafakari kwa kina kauli niliyoitoa na kujaijadili badala ya kurusha matusi humu na kuwaabudu wazungu ambao wanafanya kile unachoweza kufanya.
CC Fuso
..Umesema wazee kinga zao za mwili hupungua.
..kama hoja hiyo ni ya kweli basi wao ndio wanaotakiwa kupewa chanjo kwanza.
..vijana ambao kwa kawaida kinga za miili yao ziko juu wao hawana ulazima wa kupewa chanjo.
..hata bima ya afya kijana anaweza asikate, lakini mzee ni busara zaidi akawa nayo kutokana na kushambuliwa mara kwa mara na maradhi.
..kama hatuamini chanjo za mabeberu, na maadui zetu wa kizungu, kuna chanjo zilizotengenezwa na ndugu zetu wa UCHINA.
..binafsi nasisitiza watu wajikinge kwa kuvaa BARAKOA na kuepuka kushikana mikono. Hili nadhani kila Mtanzania anaweza kulizingatia.