October 25, 2019
Dar es Salaam, Tanzania
Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Mataifa
Prof. Palamagamba Kabudi asema kuwa Vikwazo vinavyowekewa nchi za kiAfrika lazima vipitie kwanza Umoja wa Mataifa na kujadiliwa ktk Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA United Nations General Assembly) ili kupata baraka za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Prof. Kabudi anakosoa nchi mmoja au chache kubwa beberu kuamua kuweka vikwazo bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa ni njia batili na haikubaliki. Amekosoa vikwazo kuamuliwa na nchi moja beberu maana huathiri kina mama, watoto na wananchi wanyonge zaidi
Vikwazo vinaenda kinyume na mila na desturi za uungwana kwa nchi moja kutangaza vikwazo bila kuhusisha Umoja wa Mataifa au Jumuiya za Kikanda kujadili pendekezo la vikwazo kabla havijatekelezwa.
Kama Marekani na Uingereza wangekuwa na hoja za msingi kuhusu Zimbabwe wangepeleka azimio kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa".Prof. Kabudi.
Source: ITV Tanzania