Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Maraifa

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Maraifa

Philip Mangula : CCM na ZANU-PF watangaza mshikamamo, Kila October 25 kuwa Siku Maalum ya Kumbukizi ya Vikwazo

24 Oct 2019
Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania na ZANU-PF zimeitaka jumuiya za kimataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe bila masharti yoyote.

Makamu Mwenyekiti CCM bara Philip Mangula na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania watangaza solidarity / mshikamano kupinga vikwazo na kwa pamoja wafafanua Ukoloni Mkongwe uliondolewa na sasa Ukoloni Mamboleo ndiyo 'unaotuumiza' kwa vikwazo nchi za KiAfrika

Hiki chama-Kongwe CCM hakioni vikwazo vya kisiasa dhidi ya vyama vingi vilivyoruhusiwa kikatiba Tanzania ni aina ya ukoloni mamboleo
 
Mheshimiwa kalamaganda kabugi, kwanini usimuite huyo balozi wa marekani kisha umtolee macho ili wabadili msimamo wao?
 
October 25, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Mataifa

Prof. Palamagamba Kabudi asema kuwa Vikwazo vinavyowekewa nchi za kiAfrika lazima vipitie kwanza Umoja wa Mataifa na kujadiliwa ktk Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA United Nations General Assembly) ili kupata baraka za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Prof. Kabudi anakosoa nchi mmoja au chache kubwa beberu kuamua kuweka vikwazo bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa ni njia batili na haikubaliki. Amekosoa vikwazo kuamuliwa na nchi moja beberu maana huathiri kina mama, watoto na wananchi wanyonge zaidi

Vikwazo vinaenda kinyume na mila na desturi za uungwana kwa nchi moja kutangaza vikwazo bila kuhusisha Umoja wa Mataifa au Jumuiya za Kikanda kujadili pendekezo la vikwazo kabla havijatekelezwa.

Kama Marekani na Uingereza wangekuwa na hoja za msingi kuhusu Zimbabwe wangepeleka azimio kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa".Prof. Kabudi.

Source: ITV Tanzania

Sasa kama ameamua kukuwekea vikwazo bila ruhusa, utamchukulia hatua gani?

Je hayo mabo ambayo yanasababisha vikwazo viwekwe si mabo ambayo yametendwa na iongozi kinyume na sheria za kimataifa walizozisaini?

Ni kweli najua tutaumia tukiwekewa vikwazo, lakini hilo la mweka vikwazo apate kibali sidhani kama lina nafasi.
SERIKALI YETU AJIREKEBISHE TU, INAWATISHIA NYAU WAKUBWA.
 
Kama ndivyo,Watangazie ulimwengu kuwa waliuadaa kwa nusu karne sasa la sivyo umoja huo hauna maana yeyote ya kuuita umoja wa mataifa.
Kwa maoni yako Umoja wa Mataifa una faida yo yote au unaleta vurugu tu?
 
Na ni kinyume na UN charter,nchi moja kuamua kuweka vikwazo nchi nyingine kwa visingizio visivyo na mashiko.
Ikiwezekana nchi wanachama waamue kwa pamoja vikao vya baraza la usalama la UNO view vinahama kila Mwaka ili kukwepa ukiritimba wa nchi moja kuhodhi venue za vikao kunakoweza kupelekea injustices katika maamuzi.
Nchi gani inaweza ku- host Umoja wa Mataifa kwa mfano? Urusi yenyewe inawekewa vikwazo itakuwa hizi nchi za dunia ya tatu?
 
Nchi gani inaweza ku- host Umoja wa Mataifa kwa mfano? Urusi yenyewe inawekewa vikwazo itakuwa hizi nchi za dunia ya tatu?
Kwani kuna unpresho gani kwa wajumbe kukutana huko America?
 
Kwa maoni yako Umoja wa Mataifa una faida yo yote au unaleta vurugu tu?
Nchi wanachama zenye kura za veto waache kuzitisha nchi nyingine zisizo na kura ya veto.
Kwa mfano kama sio ubeberu inawezekanaje nchi za kiafrika zaid ya 53 hakuna hata nchi moja yenye kura ya veto kwa niaba ya Afrika?
Umoja umezipa nguvu nchi za Ulaya,Marekani,Uchina na Urusi.
Just imagine hakuna hata nchi moja ya America ya kusini .....?
Kama ndivyo AU ijitoe tu UN kwa kuwa hawana any say zaidi ya kusemewa na kusakamwa kwa malengo ya kuendeleza unyonyaji.
 
Huyu anaetokwaga weupe wa beberu mdomoni huyu ,hajielewi kama urusi au China anagongwaga ban na marekan wanaomba suluhu ,harafu analeta upumbavu wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi zote 53 za ki-Africa zinachangia pesa kiasi gani kwny kuendesha shughuli za UN?
Nchi wanachama zenye kura za veto waache kuzitisha nchi nyingine zisizo na kura ya veto.
Kwa mfano kama sio ubeberu inawezekanaje nchi za kiafrika zaid ya 53 hakuna hata nchi moja yenye kura ya veto kwa niaba ya Afrika?
Umoja umezipa nguvu nchi za Ulaya,Marekani,Uchina na Urusi.
Just imagine hakuna hata nchi moja ya America ya kusini .....?
Kama ndivyo AU ijitoe tu UN kwa kuwa hawana any say zaidi ya kusemewa na kusakamwa kwa malengo ya kuendeleza unyonyaji.

dodge
 
Acha tabia ya kudharau viongozi

Yaani aheshimiwe tu kwa kuwa ni kiongozi? Heshima inakuwa earned sio forced. Huwezi kufanya vitu vya hovyo halafu utegemee kuheshimiwa eti tu kwa kuwa wewe ni kiongozi. Hakukosea aliposema aliokotwa jalalani.
 
Nchi wanachama zenye kura za veto waache kuzitisha nchi nyingine zisizo na kura ya veto.
Kwa mfano kama sio ubeberu inawezekanaje nchi za kiafrika zaid ya 53 hakuna hata nchi moja yenye kura ya veto kwa niaba ya Afrika?
Umoja umezipa nguvu nchi za Ulaya,Marekani,Uchina na Urusi.
Just imagine hakuna hata nchi moja ya America ya kusini .....?
Kama ndivyo AU ijitoe tu UN kwa kuwa hawana any say zaidi ya kusemewa na kusakamwa kwa malengo ya kuendeleza unyonyaji.
Unadhani kwanini hawajitoi Licha ya hizo kasoro ulizotoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
October 25, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Mataifa

Prof. Palamagamba Kabudi asema kuwa Vikwazo vinavyowekewa nchi za kiAfrika lazima vipitie kwanza Umoja wa Mataifa na kujadiliwa ktk Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA United Nations General Assembly) ili kupata baraka za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Prof. Kabudi anakosoa nchi mmoja au chache kubwa beberu kuamua kuweka vikwazo bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa ni njia batili na haikubaliki. Amekosoa vikwazo kuamuliwa na nchi moja beberu maana huathiri kina mama, watoto na wananchi wanyonge zaidi

Vikwazo vinaenda kinyume na mila na desturi za uungwana kwa nchi moja kutangaza vikwazo bila kuhusisha Umoja wa Mataifa au Jumuiya za Kikanda kujadili pendekezo la vikwazo kabla havijatekelezwa.

Kama Marekani na Uingereza wangekuwa na hoja za msingi kuhusu Zimbabwe wangepeleka azimio kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa".Prof. Kabudi.

Source: ITV Tanzania

Wa TZ bwana wanatoa burudani yaani miaka yote dunia nzima hadi mzee Mugabe kajifia ndiyo TZ inaliona leo hilo
Prof. Mwezio akikuwekea vikwazo na wewe muwekee siyo kulalamika.
ukiona huwezi na unaumia jua huyo ni mkubwa wako muheshimu sana na jirekebishe.
Hata hapa TZ wapinzani wana vikwazo kibao njia yao kusurvive ni kunyanza maana hawana namna ya wao kuweka vikwazo.
 
Nilisikia tumezalisha mahindi ya chakula ya kutosha hadi ziada tunapeleka nchi jirani, muhogo tunauza china.
Vikwazo havitafua dafu Tanzania, nchi hii ni "Dona katre" msiogope.
Kabudi anapende historia, atajisifu sana sisi kuwekewa vikwazo, ni promo kwake na serikali iliyomteua, vikwazo havina athari kwake kasema vitaathiri wale WANYONGE ZAIDI. Yeye siyo mnyonge hivyo hajali, hivi ni vya kawaida sana hatutaona athari yake kabisa.
Na kwanini tuogope ikiwa CHINA na URUSI wako upande wetu?!
 
Back
Top Bottom