Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Maraifa

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Maraifa

Kikwete alituwekea viongozi washamba. Wamelewa madaraka

1. Ukiukwaji wa haki za binadamu, mtu anapigwa risasi hadharani akiwa kazini alafu hakuna hata mtuhumiwa mpaka leo
2. Viongozi wa chama Cha upinzani wote wanna kesi mahakamani, na wote wamewahi kufungwa jela.
3. Waandisha wa habari za ukweli wamebambikiwa kesi zisizokuwa na dhamana
4. Watu wanatekwa kila uchao
5. Idara ya police kujichukulia hukumu mkononi
6. Mahakama hazina meno
7. Bunge linaagizwa
8. Matumizi ya pesa za serikali anatumia mtu mmoja and no editorial

Yaani Ni uchafu mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli akimaliza muda wake,akihojiwa kwa nini serikali ya awamu ya tano ilifail,atasema "nilikpotoshwa na mawaziri maprofesa wenye mazero kichwani"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
October 25, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Mataifa

Prof. Palamagamba Kabudi asema kuwa Vikwazo vinavyowekewa nchi za kiAfrika lazima vipitie kwanza Umoja wa Mataifa na kujadiliwa ktk Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA United Nations General Assembly) ili kupata baraka za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Prof. Kabudi anakosoa nchi mmoja au chache kubwa beberu kuamua kuweka vikwazo bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa ni njia batili na haikubaliki. Amekosoa vikwazo kuamuliwa na nchi moja beberu maana huathiri kina mama, watoto na wananchi wanyonge zaidi

Vikwazo vinaenda kinyume na mila na desturi za uungwana kwa nchi moja kutangaza vikwazo bila kuhusisha Umoja wa Mataifa au Jumuiya za Kikanda kujadili pendekezo la vikwazo kabla havijatekelezwa.

Kama Marekani na Uingereza wangekuwa na hoja za msingi kuhusu Zimbabwe wangepeleka azimio kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa".Prof. Kabudi.

Source: ITV Tanzania
Lakini tumuulize huyu Prof!!! Kwanini kuwe na vikwazo??? Asitufanye wote hapa Tz ni Wagogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi sisi hatuna ka nchi ka kufanyia ubeberu, na sisi tuwe tunakawekea vikwazo? maana vitisho vimekuwa vingi sana..
 
BBC watoa maoni juu ya katazo kwa nchi kadhaa ikiwemo Tanzania

Ius Gentium
October 25, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Mataifa

Prof. Palamagamba Kabudi asema kuwa Vikwazo vinavyowekewa nchi za kiAfrika lazima vipitie kwanza Umoja wa Mataifa na kujadiliwa ktk Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA United Nations General Assembly) ili kupata baraka za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Prof. Kabudi anakosoa nchi mmoja au chache kubwa beberu kuamua kuweka vikwazo bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa ni njia batili na haikubaliki. Amekosoa vikwazo kuamuliwa na nchi moja beberu maana huathiri kina mama, watoto na wananchi wanyonge zaidi

Vikwazo vinaenda kinyume na mila na desturi za uungwana kwa nchi moja kutangaza vikwazo bila kuhusisha Umoja wa Mataifa au Jumuiya za Kikanda kujadili pendekezo la vikwazo kabla havijatekelezwa.

Kama Marekani na Uingereza wangekuwa na hoja za msingi kuhusu Zimbabwe wangepeleka azimio kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa".Prof. Kabudi.

Source: ITV Tanzania
 
Huyu jinga hajui US=UN, asubirie maana yeye atakuwa wa kwanza kupigwa ban ya kuingia USA soon, wanaanza na wakubwa na familia zao kwanza halafu bdae ndio kina sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom