Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Maraifa

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Maraifa

October 25, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Mataifa

Prof. Palamagamba Kabudi asema kuwa Vikwazo vinavyowekewa nchi za kiAfrika lazima vipitie kwanza Umoja wa Mataifa na kujadiliwa ktk Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA United Nations General Assembly) ili kupata baraka za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Prof. Kabudi anakosoa nchi mmoja au chache kubwa beberu kuamua kuweka vikwazo bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa ni njia batili na haikubaliki. Amekosoa vikwazo kuamuliwa na nchi moja beberu maana huathiri kina mama, watoto na wananchi wanyonge zaidi

Vikwazo vinaenda kinyume na mila na desturi za uungwana kwa nchi moja kutangaza vikwazo bila kuhusisha Umoja wa Mataifa au Jumuiya za Kikanda kujadili pendekezo la vikwazo kabla havijatekelezwa.

Kama Marekani na Uingereza wangekuwa na hoja za msingi kuhusu Zimbabwe wangepeleka azimio kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa".Prof. Kabudi.

Source: ITV Tanzania

Kwa hiyo hili la vikwazo linafahamika kwa watawala wetu? Waziri anazungumza kwa unyonge na kulalamikia mabeberu. Bullies do not want to be bullied!
 
October 25, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Mataifa

Prof. Palamagamba Kabudi asema kuwa Vikwazo vinavyowekewa nchi za kiAfrika lazima vipitie kwanza Umoja wa Mataifa na kujadiliwa ktk Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA United Nations General Assembly) ili kupata baraka za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Prof. Kabudi anakosoa nchi mmoja au chache kubwa beberu kuamua kuweka vikwazo bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa ni njia batili na haikubaliki. Amekosoa vikwazo kuamuliwa na nchi moja beberu maana huathiri kina mama, watoto na wananchi wanyonge zaidi

Vikwazo vinaenda kinyume na mila na desturi za uungwana kwa nchi moja kutangaza vikwazo bila kuhusisha Umoja wa Mataifa au Jumuiya za Kikanda kujadili pendekezo la vikwazo kabla havijatekelezwa.

Kama Marekani na Uingereza wangekuwa na hoja za msingi kuhusu Zimbabwe wangepeleka azimio kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa".Prof. Kabudi.

Source: ITV Tanzania

Kama waziri unatakiwa kutatua matatizo sio kutoa maoni ambayo hayatafanyiwa kazi. Jitahidi kututoa kwenye list hizi na tuongeze watalii achana na kushinda kuongea na watu ambao hawasaidii kitu na kupiga makofi kinafiki
 
Hawa Jamaa walidai kuwa tunapigana VITA VYA KIUCHUMI na MABEBERU ..... Mbona wanaanza kulia mapema!!
 
Ama ni wakati muafaka wa kujitafakari na kujisahihisha kwa makosa yote ambayo ccm mmeyafanya. Siyataji kwani yanajulikana! Serikali ilishapokea maonyo matatu kutoka UE na USA lakini hayakufanyiwa kazi na kusahihisha makosa yaliyotajwa mle! Kama kweli wizara na serikali inaongozwa na watu wasomi waliopitiliza basi wangetumia busara kukaa na waliowatuhumu ili kuyajua makusudi yao badala ya kujimwambafai huku ikihitaji misaada na mikopo yao! Wafunge Safari ya kwenda EU na USA kusaka suluhu kwani kibano Chao siyo Cha kitoto, unless serikali iseme kuwa ni ajenda yake ya Siri ya kuwaumiza wananchi wake kwani wao ndio watakaozuiliwa kusafiri nchi hizo! Waziri mhusika jiuzulu tu kwa hili.
 
Marekani ndio top baba.. Usijidanganye Kuna mwingine juu. Akiamua kupiga Bomu popote anapiga, akiamua kuweka vikwazo Hakuna wa kutengua....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Kabudi apambane kuhakikisha hatuwekewi vikwazo kama wanavyotishia USA. Hayo ya Wazimbabwe awaachie wenyewe
 
Nchi wanachama zenye kura za veto waache kuzitisha nchi nyingine zisizo na kura ya veto.
Kwa mfano kama sio ubeberu inawezekanaje nchi za kiafrika zaid ya 53 hakuna hata nchi moja yenye kura ya veto kwa niaba ya Afrika?
Umoja umezipa nguvu nchi za Ulaya,Marekani,Uchina na Urusi.
Just imagine hakuna hata nchi moja ya America ya kusini .....?
Kama ndivyo AU ijitoe tu UN kwa kuwa hawana any say zaidi ya kusemewa na kusakamwa kwa malengo ya kuendeleza unyonyaji.
Afrika mtapewaje kura ya veto wakati hata chakula chenu wenyewe hamjitoshelezi! Na mkifanya fyoko kuwa mnajitoa UN, vikwazo mtakavyowekewa hata Marais wenu watatembelea baiskeli.

Ili nchi iwe na kura ya veto lazima iwe na nguvu za kiuchumi na kijeshi.
 
October 25, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Mataifa

Prof. Palamagamba Kabudi asema kuwa Vikwazo vinavyowekewa nchi za kiAfrika lazima vipitie kwanza Umoja wa Mataifa na kujadiliwa ktk Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA United Nations General Assembly) ili kupata baraka za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Prof. Kabudi anakosoa nchi mmoja au chache kubwa beberu kuamua kuweka vikwazo bila kushirikisha jumuiya ya kimataifa ni njia batili na haikubaliki. Amekosoa vikwazo kuamuliwa na nchi moja beberu maana huathiri kina mama, watoto na wananchi wanyonge zaidi

Vikwazo vinaenda kinyume na mila na desturi za uungwana kwa nchi moja kutangaza vikwazo bila kuhusisha Umoja wa Mataifa au Jumuiya za Kikanda kujadili pendekezo la vikwazo kabla havijatekelezwa.

Kama Marekani na Uingereza wangekuwa na hoja za msingi kuhusu Zimbabwe wangepeleka azimio kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa".Prof. Kabudi.

Source: ITV Tanzania

Jinga huyo ndo katufikisha hapa kwa kumshauri Jiwe Ujinga, asubiri Travel ban yake..

Na aamue sasa atabeba mzigo wa Zimbabwe ama Chato
 
Ni jambo la kusikitisha sana waziri anapoamua kuonyesha alivyo mjinga (Ignorant) wa maswala ya kidiplomasia.

Wakati nchi zile tano za kiafrika, Tanzania ikiwemo, zilizokuwa mstari wa mbele kwenye kupinga ukoloni na ubaguzi wa rangi kusini mwa Afrika wao uamuzi wao huo uliridhiwa na Baraza gani la umoja wa mataifa na kwa azimio namba ngapi.

Kabudi hajui kuwa kuna vikwazo ambavyo nchi moja inaweza kabisa ikaiwekea nchi nyingine pasipo kuhitaji idhini ya UN security council.

Nakumbuka kuna kipindi wakati wa Mkapa Tanzania ilitishia kuiwekea vikwazo Burundi pale nchi hiyo iliposusa usuluishi wa Mwl. Nyerere, sijui yeye Kabudi alikuwa wapi wakati huo, au alikuwa bado na akili ndogo.

Lkn sasa maoni ya Kabudi hayana msingi make sasa ni Tanzania ndio inajiandaa kuanza kupambana na hivyo "Vikwazo" kama Marekani ilivyodokeza ambayo kwa wote wapigania haki ni hatua chanya sana.
 
Philip Mangula : CCM na ZANU-PF watangaza mshikamamo, Kila October 25 kuwa Siku Maalum ya Kumbukizi ya Vikwazo

24 Oct 2019
Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania na ZANU-PF zimeitaka jumuiya za kimataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe bila masharti yoyote.

Makamu Mwenyekiti CCM bara Philip Mangula na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania watangaza solidarity / mshikamano kupinga vikwazo na kwa pamoja wafafanua Ukoloni Mkongwe uliondolewa na sasa Ukoloni Mamboleo ndiyo 'unaotuumiza' kwa vikwazo nchi za KiAfrika

Hakuna Marekani kusikiliza hiki chama cha wahuni, tena waongeze vikwazo zaidi. Hivi vyama vikongwe vinaleta tabia ya kutawala kimabavu bila ridhaa ya umma.
 
Back
Top Bottom