Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Prof. Shemdoe ametoa kauli hiyo Agosti 7, 2026, jijini Dar es Salaam, alipotoa salamu za OWM–TAMISEMI kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mbele ya wananchi, mara baada ya Rais Dkt. Samia kufungua rasmi Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka, Awamu ya Pili (BRT II), unaohusisha barabara za Kilwa, Chang’ombe, Sokoine na Kawawa.
Akizungumzia mchango wa wadau katika kufanikisha mradi huo, Prof. Shemdoe amewashukuru wadau mbalimbali, wakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), TANROADS, wakandarasi, washauri elekezi na watoa huduma, kwa ushirikiano wao uliowezesha kukamilika na kuzinduliwa kwa BRT II.
Amesema mradi huo unalenga kupunguza changamoto za usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam wanaotumia barabara za Kilwa, Chang’ombe, Sokoine na Kawawa, pamoja na kuboresha ufanisi wa usafiri wa umma jijini humo.
Amesema hatua hiyo si tu inaboresha usafiri kwa wananchi, bali pia inachangia kupunguza uzalishaji wa hewa yenye kiwango kikubwa cha gesi ya kaboni dioksidi (CO₂), inayozalishwa wakati injini za magari zinapochoma mafuta ya petroli na dizeli.
Kwa hatua hiyo, Serikali inaendelea kuimarisha usafiri wa umma wenye ufanisi na unaozingatia mahitaji ya wananchi, huku ikiweka mkazo katika kupunguza msongamano wa magari na athari za uzalishaji wa hewa ukaa jijini Dar es Salaam.
Pia soma:
~ Kwanini Kadi za Mwendokasi na zile za N-Card zisiunganishwe ili kupunguza utitiri wa kadi kwa Wananchi?
~ Mwendokasi hawana kadi mpya? Abiria wanasota kuomba wenye kadi wawalipie kila siku