In that case, then we should not only allow voters to sue, but also to be sued by other voters by joining in the action as co-defendants.
Those voters in Temeke, Malampaka, Tandahimba, etc should also step in as co- defendants in an action brought by a Chake Chake voter against a Ngara MP. Right?
Najaribu kufikiria haki ya watu wa Ngara ya kumchagua mwakilishi wao bungeni inaweza kupindinduliwa vipi na haki mtu mmoja kutoka Chake Chake kumshtaki mbunge waliomchagua hata kama haki ya huyo Mpemba haikuathiriwa.
Theoretically, naona kama ni argument nzuri but I can't see how this will be implemented in practice.
In representative democracies, leadership is premised on constituents electing representatives to the legislative body, delegating to these representatives the responsibility of forming a government, advising that government of their local interests and needs and monitoring the efforts that the government is making to satisfy these needs.
Anachosema Prof Shivji ndicho nilichosema mimi awali hapa, ukiondoa mfano wa kesi ya Chediel Mgonja.
Halafu angalia washabiki wa Lema watakavyokuja kijumlajumla bila uelewa wa nini kimepingwa.
Kimomogoro anachekesha. If anything mpiga kura anatakiwa awe na haki kuliko mgombea.
Nyani Ngabu,
Nimeupenda ule mjadala wenu kule Great Thinker.
Nilikuwa naongea na jaji mmoja TZ, naye akasema mawakili wengi wanapinga hii sehemu ya hukumu kuhusu mpiga kura. Huenda wakafungua kesi nyingine kama njia ya kurekebisha hili kosa. Sijui wanafunguaje kesi za namna hiyo ila inaelekea kuna malalamiko mengi kuhusu hili suala la mpiga kura kusema hana haki kufungua kesi.
Nimecheka sana hiyo ya kwamba mgombea ana haki kubwa kuliko mpiga kura/ labda huyo wakili wamemu quote vibaya. Ila kama kasema hivyo, mmmmhhhhh!!!!!
Hawa majaji pamoja na mawakili wa Lema wanataka kutuambia kuwa ubunge ni ajira.ndio maana wanajikita kwenye hoja kwamba wajibu rufani wathibitishe ni jinsi gani walivyoathirika wao binafsi.Hii si kweli kabisa ubunge ni uakilishi wa eneo fulani ambapo mtu atakayechaguliwa kwa mujibu wa sheria.Ni mkataba kati ya wananchi wa eneo hilo na mbunge(social contract) sasa kama maneno ya kibaguzi na kashfa yalitolewa na mkatarufaa na kusikiwa na wajibu rufaa na maneno hayo ni kinyume na sheria ya uchaguzi kwa nini wakose locus standi?hayo maneno yaliwaathiri moja kwa moja wajibu rufaa kwa sababu matakwa yao yalikuwa wampate kiongozi aliyetokana na free and fair election. kwa kuwa maneno yaliotumika yalimuwezesha mkatarufaa kushinda uchaguzi huo basi haukuwa fair kwa sababu baadhi ya watu wakiwemo wajibu rufaa walikuwa prejudiced.kwa kuwa uotcomes ya matokeo yalikuwa na effect kwa wajibu rufaa kuona kuwa wanampata kiongozi aliyechaguliwa kwa kufuata sheria ya uchanguzi, na kwa kuwa maneno hayo yalikuwa kinyume na sheria hiyo na yakaweza kusababisha baadhi ya wapiga kura kuyaamini na kumpa ushindi hivyo basi wajibu rufaa walikuwa na locus standi
...Watu wengi tunapinga vitu kutokana na ushabiki...
kwenye social contract ni tofauti kidogo na ordinary contract mkuu kwani ni mkataba kati ya wananchi na mtawala hivyo hawa wapiga kura sio third part bali ni sehemu kabisa ya mkatabaKama unaingiza neno "mkataba" si ujue third party hawana chao kwenye mkataba unless mkataba unasema hivyo?
"Binafsi namuheshimu sana Professa Shivji, kwanza ni mwalimu wangu wa sheria, lakini katika hili napenda kumwambia kwamba asijadili suala hili katika mtizamo wa kitaaluma zaidi,kwani kufanya hivyo atapotoka,inabidi alitizame katika hali ya kisiasa pia kwani kuna kesi nyingi za uchaguzi zimekuwa zikifungulia na watu wanaotumwa na vigogo wa kisiasa na watu wenye fedha"alisema Lissu.
Niseme tu machache...
- Academicians are good at critics but when we welcome them on board they do the same 'mistakes' they used to criticize. Hapa nampongeza Mhe. Benjamin Mkapa aliyefika hatua ya kuwaita baadhi ya maprofessor kuwa uchwala maana waliishia critics bila kumshauri. Kwa hili niishie hapa nisiende nje ya mada.
- Kuhusu hili la Rufaa ya Lema, mimi nasema hukumu ni sawa kwa busara za jopo la majaji na ninaomba ninikuu msingi wa Rufaa kama ulivyo kwenye hukumu.
...'So a vote has no right to petition and challenge the election results where his rights were not infringed'.
- Sasa sio kwamba mahakama imeondoa haki ya mpiga kura kupeleka shitaka mahakamani, hapana, bali mpiga kura hana haki kupinga matokeo pale ambapo haki yake haijaathirika. Sasa suala hapa sio mbona hukumu ya Mgonja...tuambiwe ni lini mahakama imetengua...Common, there is always first time experience; and this is it! Mimi naona premises za judgement ziko very clear kwa mtu ambaye ana nia ya kuelewa na si kubisha (critical in everything).
- Hivi mahakama si zina friends of court na hawa wasomi ni washauri mbona nao wanakuwa wanasiasa sasa?
- Nimalizie kwa kusema kwamba moja ya taaluma inayorudisha nchi yetu nyuma ni Wanasheria..Samahani kwa kusema hili. Kwanza wamekuwa wanasiasa zaidi na pia mapenzi kwa pesa yamekuwa makubwa. Hona wezi wa nchi hii kesi zao zinavyopigwa dana dana. Hivi jamani legal ethics huwa zinasemaje? Is it moral and ethical to look for loopholes to defend someone whom you know for sure is guilty? Najua kuna wanasheria wachache wazuri lakini wengi ni pesa mbele. Mbaya mahakimu na majaji nao wameingia kwenye mchezo huu mchafu.
- Mimi sio mwanasheria lakini nimpenzi wa kujifunza sheria na nina marafiki wengi wa sheria. Majaji ambao Tanzania wanaaminika ni majaji wa mahakama ya Rufaa, kwanza wanalipwa vizuri, wameridhika na pia wanaudhoefu.
- Prof, Shivj is one of good and respected opinion maker inabidi awe mwangalifu katika kutoa comments zake vinginevyo heshima yake itashuka maana kizazi hiki hakiangalii wewe ni nani bali unasema nini. Akawaulize maprof. wenzake wa sheria waliofungua practice mjini huku wakishuhudia anguko la wateja wao wakiwagalagaza na kupewa changamoto kali na waliokuwa wanafunzi wao mahakamani.
Ulevi wa kisiasa ni kama huo hapo juu!
Only in Tanzania, mwanasheria mmoja anaweza kumwambia mwanasheria mwengine asiangalie kesi kwa misingi ya taaluma ya sheria bali siasa.
Mimi nadhani mahakama ya rufani hoja yake ya msingi ingejikita katika uthibitisho je wale wapiga kura waliathiriwa vipi na mtokeo ya uchaguzi. Election has public interests.
Nakuhusu haki ya mpiga kura kushtaki mahakama ilitakiwa ieleze kwamba mpiga kura ataruhusiwa kufungua kesi endapo;
1. Haki ya mpiga kura binafsi zimeathiriwa.
2. Kama kuna vitendo vyovyote ambavyo vilifanyika na mpiga kura anaweza KUTHIBITISHA kwamba vitendo vile vilimuathiri yeye pamoja na uchaguzi kwa ujumla. Hapa akiwa na uwezo wa kuthibitsha alivyoathiriwa then he/she should have Locus stand.
N:B
Endapo kufungua kesi katika masuala ya uchaguzi itakuwa haki kamili ya mpiga kura bila kuonesha ni vipi ameathiriwa basi kutakuwa na mrundikano wa kesi ambazo zitakuwa zipo mahakaman muda mrefu maana huyu atakuwa anafungua kwa jambo hili, kesho mwingine ataibuka na jambo lingine na hii inatokana na siasa za Tanzania si za kidemokrasia bali za kukomoana.
Unalinganisha udiwani na ubunge?
Kwanza inabidi ieleweke unaenda kupinga uchaguzi wa aina gani.
Na pili, kama una compelling evidence kwa nini usiweze?
Sawa kabisa mkuu ni haki yako kufungua mashtaka lakini umbumbumbu wa sheria ndio uliowaangusha hao wakata rufaa CA vielelezo je????vithibitisho je????VILIVYOATHIRI mgombea wako asishinde utavionyesha pale mahakamani???????unavyoo????teh,teh,teh SHERIA ISIKIE TU.yap inawezekana kabisa. nakupa mfano mwingine kama ulivyosema unatoka jimbo la segerea ukafika kibakwe ukashuhudia live mgombea wa huko anatoa rushwa waziwazi, utanyamaza kisa si mgombea wa jimbo lako?. Kwa kifupi wanyonge hatuna haki tena. bora hata SHIVJI na wenzake wameliona hili na wajanja sasa hatupigi kura ng'o kwa sababu hata kama ukidhulumiwa huna pa kulalamika.
hii mada mlkua mnajadili lakin toka mlipoanza tumia hii lugha ya kitumwa mmeharibu mambo...