Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Hivi, ni hoja hiyo tu ndio imemrudisha Lema jimboni? vipi hoja zingine. Shivj na wengine je, Lema alipaswa asishinde rufaa? kwa hizo hoja zenu?
 
In that case, then we should not only allow voters to sue, but also to be sued by other voters by joining in the action as co-defendants.

Those voters in Temeke, Malampaka, Tandahimba, etc should also step in as co- defendants in an action brought by a Chake Chake voter against a Ngara MP. Right?

Najaribu kufikiria haki ya watu wa Ngara ya kumchagua mwakilishi wao bungeni inaweza kupindinduliwa vipi na haki mtu mmoja kutoka Chake Chake kumshtaki mbunge waliomchagua hata kama haki ya huyo Mpemba haikuathiriwa.

Theoretically, naona kama ni argument nzuri but I can't see how this will be implemented in practice.

In representative democracies, leadership is premised on constituents electing representatives to the legislative body, delegating to these representatives the responsibility of forming a government, advising that government of their local interests and needs and monitoring the efforts that the government is making to satisfy these needs.

Let's start this thought experiment.

Say kuna mtu mwanachama wa FUC, mkazi na mpiga kura wa Chake Chake Pemba. Alikuwa na access na high level strategic meetings za FUC huko Chake Chake Pemba.

Katika hizo strategic meetings, candidate wa ubunge wa FUC Muleba katoa mchongo wa kushinda kwa kuhonga wahesabu kura wote strategy limeshapangwa, documents zipo, ma bank transfers yapo. Piga ua galagaza lazima ashinde ubunge Muleba ili aende ku introduce sheria fulani to an unsuspecting parliament ili kuruhusu takeover fulani katika biashara ya mafuta kwa WaIran. Huyu mtu ana documents za alliance na hawa waIran wamuendeshe kama remote control, awapatie parliamentary access to information.

Uchaguzi unapita, huyu mgombea wa FUC anashinda Muleba, kwa rushwa. Ushahidi wote huyu mjumbe wa FUC wa Chake Chake anao, anaweza kuuwakilisha mahakamani.

Nafsi yake inamsuta kwani anaelewa ubunge hawajashinda kihalali, na zaidi ya hapo mbunge hana nia nzuri na nchi kuna a conspiracy inaandaliwa.

Huyu mjumbe wa FUC asiwezeshwe kuchallenge ubunge wa huyu mbunge wa Muleba kwa sababu tu si mpiga kura wa Muleba?

Au si mgombea aliyeshindwa Muleba?

This scenario may read like a hyperbole from an overly excited mind, but it is actually very plausible under our current conditions.
 
hii mada mlkua mnajadili lakin toka mlipoanza tumia hii lugha ya kitumwa mmeharibu mambo...
 
Hawa majaji pamoja na mawakili wa Lema wanataka kutuambia kuwa ubunge ni ajira.ndio maana wanajikita kwenye hoja kwamba wajibu rufani wathibitishe ni jinsi gani walivyoathirika wao binafsi.Hii si kweli kabisa ubunge ni uakilishi wa eneo fulani ambapo mtu atakayechaguliwa kwa mujibu wa sheria.Ni mkataba kati ya wananchi wa eneo hilo na mbunge(social contract) sasa kama maneno ya kibaguzi na kashfa yalitolewa na mkatarufaa na kusikiwa na wajibu rufaa na maneno hayo ni kinyume na sheria ya uchaguzi kwa nini wakose locus standi?hayo maneno yaliwaathiri moja kwa moja wajibu rufaa kwa sababu matakwa yao yalikuwa wampate kiongozi aliyetokana na free and fair election. kwa kuwa maneno yaliotumika yalimuwezesha mkatarufaa kushinda uchaguzi huo basi haukuwa fair kwa sababu baadhi ya watu wakiwemo wajibu rufaa walikuwa prejudiced.kwa kuwa uotcomes ya matokeo yalikuwa na effect kwa wajibu rufaa kuona kuwa wanampata kiongozi aliyechaguliwa kwa kufuata sheria ya uchanguzi, na kwa kuwa maneno hayo yalikuwa kinyume na sheria hiyo na yakaweza kusababisha baadhi ya wapiga kura kuyaamini na kumpa ushindi hivyo basi wajibu rufaa walikuwa na locus standi
 
Anachosema Prof Shivji ndicho nilichosema mimi awali hapa, ukiondoa mfano wa kesi ya Chediel Mgonja.

Halafu angalia washabiki wa Lema watakavyokuja kijumlajumla bila uelewa wa nini kimepingwa.

Kimomogoro anachekesha. If anything mpiga kura anatakiwa awe na haki kuliko mgombea.

Hili ni moja ya mapungufu ya katiba yetu, "mpiga kura ana haki ya kupinga matokea only kama haki yake ya kupiga kura ilivurugwa" mfano alikataliwa kupiga kura kwa sababu si za kisheria nk. Katiba hii mbovu inavuka mipaka na CCM waliweka mwanya huo na kuingiza nchi katika gharama za kipuuzi
Watu wengi tunapinga vitu kutokana na ushabiki, ni malezi tuliyopewa na CCM
 
Nyani Ngabu,
Nimeupenda ule mjadala wenu kule Great Thinker.

Nilikuwa naongea na jaji mmoja TZ, naye akasema mawakili wengi wanapinga hii sehemu ya hukumu kuhusu mpiga kura. Huenda wakafungua kesi nyingine kama njia ya kurekebisha hili kosa. Sijui wanafunguaje kesi za namna hiyo ila inaelekea kuna malalamiko mengi kuhusu hili suala la mpiga kura kusema hana haki kufungua kesi.

Nimecheka sana hiyo ya kwamba mgombea ana haki kubwa kuliko mpiga kura/ labda huyo wakili wamemu quote vibaya. Ila kama kasema hivyo, mmmmhhhhh!!!!!

1. Mimi nimeelewa kuwa katika kesi hii mgombea mwenyewe ndiye aliyepaswa kulalamika na si wapiga kura wake kama ilivyo pia kwamba kama wapiga kura wana kitu wanakilalamikia labda hawakutendewa haki ni jukumu lao kufungua kesi na si jukumu la mtu mwingine (third party), mfano mgombea kulalamika.
2. Tuchukulie mimi nimekutukana vibaya wewe. Halafu mtu mwingine aliyesikia yeye mwenyewe afungue kesi ya kunishitaki kuwa nimekutukana na aliyetukanwa wala haoni tatizo. Je, mahakama hapo ungetaka imsikilize nani: aliyetukanwa na yeye haoni tatizo lotote au aliyesikia na ambaye hakutukanwa?
3. Tukumbuke pia kuwa kesi hii si ya jinai na hivyo utaratibu wake wa kufungua na kuendesha mashtaka ni tofauti na ule wa kesi ya jinai.
 
Hawa majaji pamoja na mawakili wa Lema wanataka kutuambia kuwa ubunge ni ajira.ndio maana wanajikita kwenye hoja kwamba wajibu rufani wathibitishe ni jinsi gani walivyoathirika wao binafsi.Hii si kweli kabisa ubunge ni uakilishi wa eneo fulani ambapo mtu atakayechaguliwa kwa mujibu wa sheria.Ni mkataba kati ya wananchi wa eneo hilo na mbunge(social contract) sasa kama maneno ya kibaguzi na kashfa yalitolewa na mkatarufaa na kusikiwa na wajibu rufaa na maneno hayo ni kinyume na sheria ya uchaguzi kwa nini wakose locus standi?hayo maneno yaliwaathiri moja kwa moja wajibu rufaa kwa sababu matakwa yao yalikuwa wampate kiongozi aliyetokana na free and fair election. kwa kuwa maneno yaliotumika yalimuwezesha mkatarufaa kushinda uchaguzi huo basi haukuwa fair kwa sababu baadhi ya watu wakiwemo wajibu rufaa walikuwa prejudiced.kwa kuwa uotcomes ya matokeo yalikuwa na effect kwa wajibu rufaa kuona kuwa wanampata kiongozi aliyechaguliwa kwa kufuata sheria ya uchanguzi, na kwa kuwa maneno hayo yalikuwa kinyume na sheria hiyo na yakaweza kusababisha baadhi ya wapiga kura kuyaamini na kumpa ushindi hivyo basi wajibu rufaa walikuwa na locus standi

Kama unaingiza neno "mkataba" si ujue third party hawana chao kwenye mkataba unless mkataba unasema hivyo?
 
...Watu wengi tunapinga vitu kutokana na ushabiki...

1. inabid ufikirie lema angekuwa wa ccm au cuf unge-comment unavyo comment sasa? maana leo ni wa cdm kesho inaweza kuwa wa ccm 2. tusio na vyama interest iko kwenye namna bora zaid ya kushughulika na chaguz na kesi zake baadae 3. hata kama majaj wa kuheshmika sana ndo wametoa huo uamuz na ujadiliwe tu. tunajua wao pia ni binadam kama sie na tunajuaje kama hawakuwa influenced na chochote?
 
Kama unaingiza neno "mkataba" si ujue third party hawana chao kwenye mkataba unless mkataba unasema hivyo?
kwenye social contract ni tofauti kidogo na ordinary contract mkuu kwani ni mkataba kati ya wananchi na mtawala hivyo hawa wapiga kura sio third part bali ni sehemu kabisa ya mkataba
 
"Binafsi namuheshimu sana Professa Shivji, kwanza ni mwalimu wangu wa sheria, lakini katika hili napenda kumwambia kwamba asijadili suala hili katika mtizamo wa kitaaluma zaidi,kwani kufanya hivyo atapotoka,inabidi alitizame katika hali ya kisiasa pia kwani kuna kesi nyingi za uchaguzi zimekuwa zikifungulia na watu wanaotumwa na vigogo wa kisiasa na watu wenye fedha"alisema Lissu.

Ulevi wa kisiasa ni kama huo hapo juu!
 
Niseme tu machache...
  • Academicians are good at critics but when we welcome them on board they do the same 'mistakes' they used to criticize. Hapa nampongeza Mhe. Benjamin Mkapa aliyefika hatua ya kuwaita baadhi ya maprofessor kuwa uchwala maana waliishia critics bila kumshauri. Kwa hili niishie hapa nisiende nje ya mada.
  • Kuhusu hili la Rufaa ya Lema, mimi nasema hukumu ni sawa kwa busara za jopo la majaji na ninaomba ninikuu msingi wa Rufaa kama ulivyo kwenye hukumu.

...'So a vote has no right to petition and challenge the election results where his rights were not infringed'.


  • Sasa sio kwamba mahakama imeondoa haki ya mpiga kura kupeleka shitaka mahakamani, hapana, bali mpiga kura hana haki kupinga matokeo pale ambapo haki yake haijaathirika. Sasa suala hapa sio mbona hukumu ya Mgonja...tuambiwe ni lini mahakama imetengua...Common, there is always first time experience; and this is it! Mimi naona premises za judgement ziko very clear kwa mtu ambaye ana nia ya kuelewa na si kubisha (critical in everything).
  • Hivi mahakama si zina friends of court na hawa wasomi ni washauri mbona nao wanakuwa wanasiasa sasa?
  • Nimalizie kwa kusema kwamba moja ya taaluma inayorudisha nchi yetu nyuma ni Wanasheria..Samahani kwa kusema hili. Kwanza wamekuwa wanasiasa zaidi na pia mapenzi kwa pesa yamekuwa makubwa. Hona wezi wa nchi hii kesi zao zinavyopigwa dana dana. Hivi jamani legal ethics huwa zinasemaje? Is it moral and ethical to look for loopholes to defend someone whom you know for sure is guilty? Najua kuna wanasheria wachache wazuri lakini wengi ni pesa mbele. Mbaya mahakimu na majaji nao wameingia kwenye mchezo huu mchafu.
  • Mimi sio mwanasheria lakini nimpenzi wa kujifunza sheria na nina marafiki wengi wa sheria. Majaji ambao Tanzania wanaaminika ni majaji wa mahakama ya Rufaa, kwanza wanalipwa vizuri, wameridhika na pia wanaudhoefu.
  • Prof, Shivj is one of good and respected opinion maker inabidi awe mwangalifu katika kutoa comments zake vinginevyo heshima yake itashuka maana kizazi hiki hakiangalii wewe ni nani bali unasema nini. Akawaulize maprof. wenzake wa sheria waliofungua practice mjini huku wakishuhudia anguko la wateja wao wakiwagalagaza na kupewa changamoto kali na waliokuwa wanafunzi wao mahakamani.

Mkuu, big up.
 
Ulevi wa kisiasa ni kama huo hapo juu!

Only in Tanzania, mwanasheria mmoja anaweza kumwambia mwanasheria mwengine asiangalie kesi kwa misingi ya taaluma ya sheria bali siasa.

Na only in Tanzania, jambo hilo litaonekana ni poa tu na msemaji ni "jembe" sana
 
Only in Tanzania, mwanasheria mmoja anaweza kumwambia mwanasheria mwengine asiangalie kesi kwa misingi ya taaluma ya sheria bali siasa.

hata mim hii imenishangaza zaid. sikutegemea jembe lisu angesema hvo alivosema. eti suala litazamwe ki-Tz zaid. utafikir tz 2ko so different from the rest na hii ni genetically. anazid kuniaminisha kuwa prof shivji yuko right. nimesoma mwananch la leo
 
Mimi nadhani mahakama ya rufani hoja yake ya msingi ingejikita katika uthibitisho je wale wapiga kura waliathiriwa vipi na mtokeo ya uchaguzi. Election has public interests.
Nakuhusu haki ya mpiga kura kushtaki mahakama ilitakiwa ieleze kwamba mpiga kura ataruhusiwa kufungua kesi endapo;
1. Haki ya mpiga kura binafsi zimeathiriwa.
2. Kama kuna vitendo vyovyote ambavyo vilifanyika na mpiga kura anaweza KUTHIBITISHA kwamba vitendo vile vilimuathiri yeye pamoja na uchaguzi kwa ujumla. Hapa akiwa na uwezo wa kuthibitsha alivyoathiriwa then he/she should have Locus stand.

N:B
Endapo kufungua kesi katika masuala ya uchaguzi itakuwa haki kamili ya mpiga kura bila kuonesha ni vipi ameathiriwa basi kutakuwa na mrundikano wa kesi ambazo zitakuwa zipo mahakaman muda mrefu maana huyu atakuwa anafungua kwa jambo hili, kesho mwingine ataibuka na jambo lingine na hii inatokana na siasa za Tanzania si za kidemokrasia bali za kukomoana.

Ebwana upo sahihi kabisa, katika uelewa wangu mpiga kura anaweza kufungua kwasababu flani au anapo jiskia siungi hoja ya shivji.
 
Mpiga kura hana Locus stand ya kuchalenge hapo, lakini pia mahakama imetoa sababu za hukumu kua hakuna athari zozote zilizompata mpiga kura katika madai ya msingi ya kesi waliyofungua. mahakama kuu imesimama kwenye haki haijayumba katika kutoa maamuzi katika shauri hili.
 
Unalinganisha udiwani na ubunge?

Nyani Ngabu, ubunge, udiwani na urais vyote vinahusika na upigaji kura. Haki ya mpiga kura inatofautiana kulingana na ama anapiga kura ya urais, ubunge au udiwani. Maana yangu ni kuwa haki ya mpiga kura inategemea na eneo analotoka. Mpigakura aliejiandikisha Chakechake anaweza kupiga kura kumchagua rais mahali popote nchini (Ngara, Kintinku, Ishinabulandi n.k) lakini hawezi kupiga kura kumchagua mbunge nje ya jimbo lake la uchaguzi na hawezi kupiga kura ya kumchagua diwani nje ya kata aliyojiandikisha.

By the same token; there must be a limitation on the right of the registered voter to appeal against the election results.
 
Kwanza inabidi ieleweke unaenda kupinga uchaguzi wa aina gani.

Na pili, kama una compelling evidence kwa nini usiweze?

Nyani Ngabu, hata kama mjuaji ana "compelling evidence" ya election violations Musoma Mjini, yeye akiwa mpigakura wa Kanyenye Tabora haki zake zinazohusiana na uchaguzi (iwe ya ubunge au udiwani) Musoma Mjini zitakuwa zimekiukwaje?
 
Nasikitika kumfananisha shivji na mchungaji(mwl Prof. wa sheria) wa kanisa anayeaminika kwa mafundisho,maombezi na ushauri(elimu ya sheria) kwa waumini(wananchi) wake na sasa amekengeuka(corrupt) na kuwafanya waumini wamkimbie(mimi kuacha kuhudhuria workshop zake popote pale) na kuanzisha harakati za kumpinga kwa kuacha misingi ya sheria na kuanza kufanya siasa.............the deady thought .....kweli kuzeeka kwingine mzigo....nawkilisha.
 
yap inawezekana kabisa. nakupa mfano mwingine kama ulivyosema unatoka jimbo la segerea ukafika kibakwe ukashuhudia live mgombea wa huko anatoa rushwa waziwazi, utanyamaza kisa si mgombea wa jimbo lako?. Kwa kifupi wanyonge hatuna haki tena. bora hata SHIVJI na wenzake wameliona hili na wajanja sasa hatupigi kura ng'o kwa sababu hata kama ukidhulumiwa huna pa kulalamika.
Sawa kabisa mkuu ni haki yako kufungua mashtaka lakini umbumbumbu wa sheria ndio uliowaangusha hao wakata rufaa CA vielelezo je????vithibitisho je????VILIVYOATHIRI mgombea wako asishinde utavionyesha pale mahakamani???????unavyoo????teh,teh,teh SHERIA ISIKIE TU.
 
hii mada mlkua mnajadili lakin toka mlipoanza tumia hii lugha ya kitumwa mmeharibu mambo...

Hata wewe umetumia maandishi ya watu, kama hutaki kujichanganya anzisha maandishi ya kwetu na wala usitumie teknolojia za watu tujue unamaanisha unachoandika.

Mtu unatumia alphabet ya Kirumi, internet ya Kimarekani, computer/simu nina hakika si ya Kitanzania etc etc halafu unabinua pua kuhusu "lugha ya kitumwa"?

Kiswahili chenyewe ni lugha iliyotumika katika biashara ya kitumwa kipande chetu, kuliko kiingereza, na kimejaa maneno ya kiarabu, kwa minajili hii hata wewe nawe hujafanya chochote zaidi ya huyo unayemuamini.

Hizo sheria zenyewe tumerithi za Muingereza, halafu kelele nyyingi lugha ya kitumwa wakati hata ukiandika kiswahili ni lugha iliyotohoa sana kwa watu, hatuna maandishi yetu na sheria zenyewe tumezirithi kwa msingi wa common law za Uingereza na mfumo mzima wa serikali umedesa kwenye Westminster system, kila unapoangalia tumedesa.

Wewe unalalmikia lugha?

Unazunguka harijojo ka guluguja aso uti.
 
Back
Top Bottom