Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Wanasheria tufahamisheni ni haki zipi ambazo anazo mpiga kura kwenye uchaguzi.
 
Binafsi nnaona mpiga kura haki anayo, ila kwa kesi ya lema, ni hoja gani mpiga kura anakuja nazo?
hapo ndo penye tatizo, mpiga kira anatakiwa aje na hoja zinazomgusa moja kwa moja.
 

Nilitaka kuandika wazo hili, kwa kuwa umeshaandika basi napigia mstari. Hebu tu read btn the lines jamani, tusikurupuke na kipengele kimoja, hasa kwa wanasheria
 
Shivji yuko sahihi kwamba mpiga kura ana haki, lkn haki hiyo ataitumia pale ambapo anaona kuna jinsi flani hajatendewa haki.
Sasa hao wapiga kura ndio waliotukanwa? Locus stand yao ktk kesi hii iko wapi?
Sio kwa sababu ni mpiga kura basi ufungue kesi ktk mambo yasiyokugusa, that is not the law
 
Badala ya kuhangaika na Lema,Prof Shivji angezungumzia hukumu ya Mgombea binafsi iliyoamuliwa na mahakama ya Rufaa.
 
Mkuu msome vizuri Prof Shivji yeye anaelezea tafsiri za sheria wewe umejikita zaidi kwenye ushabiki wa kisiasa.

Ritz inaingia akilini mwako mfano nitukanwe na Honey K halafu wewe Ritz uende kumshtaki mahakamani? Mbaya zaidi hata kunishirikisha mtukanwa kama shahidi isifanyeke, kwanini nirukwe hivyo mtukwanwa mwenye haki na hata kama `sijaonyesha dhamira ya kufungua mashtaka dhidi ya mtusi?

Mambo haya tuweke kwanza ushabiki wa kiitikadi kando tujadili kisheria na hata kama taaluma ya kisheria imetupiga chenga, lakini ile kitu inaitwa common sense tu Shvji ameteleza kidogo.

Hoja ya kujenga utetezi tokana na kesi ya Mgonja ni dhaifu katika maana kwamba upembuzi wa sheria na tafsiri hubadilika tokana nawakati, ndio maana kuna mabadiliko ya sheria mara kwa mara licha ya kuongeza mpya kwani wakati ukuta, vinginevyo tusingekuwa na baraza la kudumu la kutunga sheria, maana serikali haijakamilika bila uwepo wa bunge ambao ni mmoja ya mhimili muhimu wa serikali, mhimili ambayo ndio chimbuko la kutathmini mabadiliko ya miundo ya sheria nchini.

Matumaini yangu makubwa umenielewa ingawa unaweza kuja na jibu ambalo kwa sababu zako unaweza ukalitoa kinyume cha uelewa wako, lol.

Enjoyo Holiday Ritz!
 
Kwa wale wanaofikiri kwamba huenda wale wanaCCM watatu watakata rufaa tena (kutaka jopo kubwa zaidi la Majaji rufaa) kupitia hukumu hiyo wasiwe na hofu kwani rufaa haitafanikiwa.

Hoja hiyo ya 'locus standi' ya warufaa -- yaani iwapo wana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi halikuwa pekee ambalo mawakili wa lema waliliweka katika rufaa yao.

Hoja za kutokuwepo CD za uthibitisho wa matusi ya Lema kwa BB, au jaji wa Mahakama Kuu kukataa ushahidi wa wanachadema kwa sababu ulikuwa wa kishabiki lakini hapo hapo kukubali ule ushahidi wa wanaCCM kwa mfano hayakuguswa kabisa katika ruling ya jaji Kimaro na wenzake na hilo na mengine yanaweza kuibuliwa.

Kumbukeni Rufaa ambayo Azim dewji alimfungulia Dr kabaorou mwaka 1994/95 (yaani baada ya Kaborou kushinda kesi aliyomfungulia Premji katika Mahakama Kuu kupinga ushindi wake katika byelection ya Kigoma Mjini) Jaji Lugakingira (nadhani) aliibua suala la uraia wa Azim Premji kwani aliona suala hilo halikufafanuliwa vizuri (au tuseme lilikuwa wrongly decided upon) katika rufaa ya awali ya Dr Kaborou kupinga matokeo ya ubunge uliompa ubunge Premji.

 
Shivji ni binadamu kama wengine tukubali kuna sehemu anakosea, sawa mpiga kura anahaki ya kufungua kesi coz anamasilahi kwenye uchaguzi lkn suala hapa ni mwenendo wa uchaguzi uliadhiri vp haki ya mpiga kura!
 
Prof. Shivji si avae joho tu,
kwa nini kuongelea pembeni.
 

Asante kwa kumbukumbu yako. Akina Mkanga hawatathubutu kukata rufaa tena kuna masuala mengine hayakuguswa na yanaweza kuibuliwa kama unavyosema.
 
Mkuu Ritz hebu waache kina EMT watushushie nondo za kisheria hapa bana. Mwenzio nakaribia kukamata LLB kwa nondo nazozisoma hapa.

Ubishani wa kisiasa tuufuate na tuufanyie kwenye mathread ya kina TUNTEMEKE na Masalia yao.
 
Last edited by a moderator:

Aren't some black people unsuitable to serve on juries?
 

Umenena vema kiongozi. Ni jambo ambalo haliwezekani kila mtu afungue kesi kisa ni mpiga kura. Ingekua kwamba Lema amechukua kadi yake ikasababisha asipige kura, au angetishwa kwa namna yoyote, hapo ana haki ya kufungua kesi na angeshinda. Lakini matusi ni personal attack, hayo hayo tunayoyaona matusi kwa wenzetu wa tamaduni zingine ni majina ya heshima sana-nenda Japan utakubaliana na mimi.
 
Shivji kaamua kuchafua hewa kwa makusudi kabisa na hii ni dhambi ambayo itamrudia tu.
Hii ni 2012 awareness ya binadamu inazidi kuongezeka kila sekunde inayopita.
Tutarajie kuna madudu mengi kutoka kwa watu wenye majina kama Shivji.

Shivji got point (social reason),but ni complete mbulula wa legal reason..na sio logic kusema eti hukumu ina makosa, sheria ni loop holes na logic ziko wazi kutumika to win..

Labda tukumbuke kesi ya lema haikufunguliwa chini ya ibara ya 26(2) ambayo inampa fursa raia yoyote kufungua shauri mahakaman yenye maslahi ya umma..na ipo wazi iyo kesi hata haina maslahi kwa umma wa watanzania.. Shivji naona angeingilia ile kesi ya dowans ambayo ilikua na maslahi 100% kwa umma..

Ila pia sijaona kwenye gazeti hawakuonesha what shivji think and why hiyo hukumu imetolewa hivyo anahisi kua jopo la majaji halikufikiria hicho anachosema but sio kweli they got iyo idea tht why walisema ile kesi ya mgonja was wrongly judged!
 
Kuna jimbo moja lilipingwa hapo dar es salaam kisa ni masanduku yalipotea.Pingamizi likatupiliwa mbali.Je ni hukumu gani ambayo haikuwa halali kati ya hii Lema na hiyo?
 
Mkuu Ritz hebu waache kina EMT watushushie nondo za kisheria hapa bana. Mwenzio nakaribia kukamata LLB kwa nondo nazozisoma hapa.

Ubishani wa kisiasa tuufuate na tuufanyie kwenye mathread ya kina TUNTEMEKE na Masalia yao.

Umenena mkuu.!
 
Last edited by a moderator:
#jaman WATANZANIA tuache kuishi kwa mazoéa,shvji ni shvji tu lakn ni BINADAMU kama walivo majjaji wale RUFANI!!!sio akisema fulan basi na ww hapo hapo NO!!
kumbuken JAJI anauwezo wa kufanya nn akiwa mahakaman,kwa namna gani na kwa maslahi gan!!!
kwa mtazamo wangu,HUKUMU haina kasoro maana ushaidi hautoshelezi toka mwanzo kule ARUSHA!!!
 

1. Wanasheria kutofautiana ni kitu cha kawaida sana katika sheria (ni kama wanavyotofautiana wanafalsa na wanateolojia).

2. Ndio maana mtu anaweza kushinda kesi mahakama ya mwanzo mrufani akaja kushinda kwenye mahakama ya hakimu mkazi au ya wilaya na pengine kushindwa tena akienda mahakama kuu na kuendelea kushindwa akienda mahakama ya rufaa au kushinda.

3. Sheria zinatafsiriwa na ndio maana wanaotafsiri wanatofautiana pia. Ukisoma hukumu ya Jaji Mwalusanya kupinga hukumu ya kifo (Mahakama Kuu) na kuibadilisha kuwa kifungo cha maisha (sababu alizozitoa ni za msingi) na ukisoma pia jinsi Mahakama ya Rufaa ilivyopitia hukumu yake na kuichambua na kukubaliana naye kuwa hukumu ya kifo inapingana na haki za binadamu, ni ya kikatiri na haki ya kuishi lakini mahakama hiyohiyo iliyotambua hivyo ilisema kuendelea kuwa na hukumu hii si kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na bado ndivyo ilivyo hadi leo mpaka hapo tutakapoibadili kwenye Katiba Mpya (kama tutafanya hivyo).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…