1. Haki ya kupiga kuraHaki zipi anazo mpiga kura tupe mfano.
shivji anachemka katika hili
Mpiga kura atakosaje kuwa na maslahi katika chaguzi za nchini mwake bana?
Watu wa Chadema wametoka wapi? Si muijadili hiyo sheria tu bila kuweka siasa kama magwiji ya sheria hapa JF akina EMT walivyofanya?
Wengine kusoma na ku like inatosha!
Anachosema Prof Shivji ndicho nilichosema mimi awali hapa, ukiondoa mfano wa kesi ya Chediel Mgonja.
Halafu angalia washabiki wa Lema watakavyokuja kijumlajumla bila uelewa wa nini kimepingwa.
Kimomogoro anachekesha. If anything mpiga kura anatakiwa awe na haki kuliko mgombea.
Nimeyakuza na kuyapaka rangi maneno yako hapo juu ili kuonyesha msisitizo.. infact hizo ndio sifa zako kwa sababu huoni hata hoja iliyopo nyumba ya wanaopinga hukumu hii.. umeshindwa kuona jinsi mahakama ilivyopinda sheria(bila kujali uzuri au ubaya wa sheria husika) na umeshindwa kuona hata mawakili na wanasheria waliobobea wanapotoa matamshi kwaba"""" HAPA MAHAKAMA IMETUNGA SHERIA MPYA""""Wengine hatukushiriki sana kwenye huo mjadala lakini everytime I come across such blanket statement kama hii yako, I lose interest. Jaribu kuwapa breathing space watu usiokubaliana nao...mara wapenzi wa Chadema, mara wapenzi wa Dr. Slaa na sasa imeongezeka wapenzi wa Lema, duh, eti hawana uelewa wa nini kinachoongelewa. Kiranga nakuheshimu na nisingependa tujiingize kwenye nani zaidi bali tubakie kwenye kupingana kwa hoja...ni hayo tu, sasa tuendeleee. How I wish some of us had more time to participate kwenye mijadala mbalimbali but then...
Binafsi naamini kuna mambo ya kipuuzi tunayoyapa kipaumbele while in actual fact ni non issues from the word go. Sisi tuliobahatika kupata exposure kwa wenzetu ambako demokrasia imekomaa, no voter would dream of going to court to challenge an election result based on mgombea anayemtaka kushindwa uchaguzi kwa sababu alikashifiwa kwenye kampeni huku mhusika hayuko tayari hata kuwa shahidi mahakamani...it is stupid, ridiculous and makes no sense. Nina hakika hata mahakama ililiona hili kwamba ku"entertain" kitu kama hicho ni kuidhalilisha mahakama. Naamini hukumu iliyotolewa ilizingatia hilo.
Ritz inaingia akilini mwako mfano nitukanwe na Honey K halafu wewe Ritz uende kumshtaki mahakamani? Mbaya zaidi hata kunishirikisha mtukanwa kama shahidi isifanyeke, kwanini nirukwe hivyo mtukwanwa mwenye haki na hata kama `sijaonyesha dhamira ya kufungua mashtaka dhidi ya mtusi?
Mambo haya tuweke kwanza ushabiki wa kiitikadi kando tujadili kisheria na hata kama taaluma ya kisheria imetupiga chenga, lakini ile kitu inaitwa common sense tu Shvji ameteleza kidogo.
Hoja ya kujenga utetezi tokana na kesi ya Mgonja ni dhaifu katika maana kwamba upembuzi wa sheria na tafsiri hubadilika tokana nawakati, ndio maana kuna mabadiliko ya sheria mara kwa mara licha ya kuongeza mpya kwani wakati ukuta, vinginevyo tusingekuwa na baraza la kudumu la kutunga sheria, maana serikali haijakamilika bila uwepo wa bunge ambao ni mmoja ya mhimili muhimu wa serikali, mhimili ambayo ndio chimbuko la kutathmini mabadiliko ya miundo ya sheria nchini.
Matumaini yangu makubwa umenielewa ingawa unaweza kuja na jibu ambalo kwa sababu zako unaweza ukalitoa kinyume cha uelewa wako, lol.
Enjoyo Holiday Ritz!
sijasoma sheria hata moja ila hapo ndipo kwenye hoja ya msingi kabisa.Hehehe. Mwalimu wangu aliyenifundisha maana na application ya locus standi nae anapinga?
Ngoja nikakague notes za lectures zake wakati anatufindisha hii kitu kama alisema the doctrine of locus standi does not apply to election litigation, let alone mentioning the case of Mgonja.
Mgonja was a good law until the CA said in Lema it wasn't.
It does not matter that Mgonja had been binding for 30 years. Tunazo sheria za muda mrefu mbovu nyingi tuu.
May be before Lema, the CA did not have an opportunity to consider whether Mgonja was a good law.
Bado haijaniingia akilini eti mtu aliyejiandikisha na kupigia kura Chake Chake anakuja kumshtaki diwani aliyeshinda uchaguzi Ngara eti kwa sababu anayo haki ya kufanya hivyo hata kama haki zake hazijawa affected.
Kesi ya Lema itazuia wanasiasa wenye uchu wa madaraka kujificha nyuma ya wapiga kura wa kawaida kufungua kesi halafu wakishindwa wanawakana inapofikia muda ya kulipia gharama za kesi.
Mpiga kura ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi, lakini katika mazingira yapi????
Malalamiko yaliyowasilishwa mahakamani na wapinga matokeo binafsi niliyaona yana walakini.
Wapiga kura wanalalamika kwamba mgombea wao alishindwa kwa vile alitukanwa kwamba ni side dish ya waziri mkuu wa zamani!!!!
Sasa sijui tamko hilo linamnyima kura vipi mgombea na linampa kura vipi aliyetamka na zaidi linawanyima haki wapiga kura vipi.
Kuna watu tunawaheshimu kwa mvi zao, lakini nadhani wakti umefika naamini wanatakiwa wakakojoe walale.
Wakuu EMT na Jokakuu,
Mimi nawaheshimu sana na sisi wote ni brothers na makomredi ambao watu wanatusoma hapa, na ninyi ni wanasheria.
Sasa ni lazima tulenge kwenye principles kwamba mzee Shivji amekurupuka na hoja yake.
Kama alivyotanabaisha JokaKuu kwamba kesi ya Mgonja ilihusu madai kwamba kulikuwepo rushwa na hii kesi ya Mheshimiwa Lema ilikuwa na madai tofauti.
Hapana! Pamoja na kwamba sikubaliani na argument ya Prof. Shivji sidhani kama amewatusi majaji waliotoa hukumu.
It is normal in the legal field to criticise court judgements. Ndiyo maana kwenye nchi za watu controversial decision kama hii inazalisha articles hata 500 within the first few months, some applauding, others, criticising, the decision.
It is normal kabisa na kufanya hivyo haina maana kuwa mtu ana-question intergrity ya jaji aliyetoa hukumu.
Tumefundishwa kukubaliana kutokubaliana. Kwa vile sijakubaliana na wewe haina maana kuwa nimekudharau au nimekutusi.
You will still be my learned brother/sister. lol.
1. Mahakama inaweza kutunga sheria kutokana na hukumu zake. Wakina shivji wakasome hukumu za judge Demining wa uingereza jinsi hukumu zake zilivhotengeneza sheria nyingi za jumuia ya madola. Kama kulikuwapo na hukumu ya 1980 inamaana haiwezi kutenguliwa tena?
2. Mahakama haikusema wapiga kura hawana haki ila hicho walichofungulia kesi ndio kina ulakini. Kumbuka wale wanaharakati waliofungua kesi ya kugomea malipo ya dowans mahakama ilisema wazi kuwa hawana haki kwa vile sio party to the contract. Lakini hao wanaharakati na watanzania wote ni walipa kodi na tuna haki wao hawakuliona hilo? Mahakama zimeweka utaratibu kuwa lazima uwe muadhirika au ufungue kesi kwa niaba ya mwadhirika kwa ridhaa yake. Au mtu ukiona jirani amewekewa X unaweza kwenda mahakamani kupinga kwa vile utapoteza jirani? Mwadhirika wa kesi hakwenda mahakamani na kesi ya kutukana kama ni kweli wangepaswa wapeleke polisi ili jamhuri imfungulie shitaka la jinai. Kama mwanachi anaweza kufungua mashitaka ya jinai basi hata wanachi wafungue kesi za watuhumiwa wa epa si wote ni waadhirika na tuna haki na kodi zetu?