Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Haki zipi anazo mpiga kura tupe mfano.
1. Haki ya kupiga kura
2. Haki ya kupigiwa kura
3. Haki ya kudai haki kama anaona haki yake inapokonywa
4. Kama Dr Batilda angefungua kesi/angelalamika labda tungekuwa tunakuwa tunajadili kitu kingine lakini (third party)! Hapa labda kama utangeleta sheria inayosema hivyo kwamba akionewa huyu mwenye haki ya kulalamika ani yule mwingine na si aliyeonewa.
 
Mkuu Ritz hebu waache kina EMT watushushie nondo za kisheria hapa bana. Mwenzio nakaribia kukamata LLB kwa nondo nazozisoma hapa.

Ubishani wa kisiasa tuufuate na tuufanyie kwenye mathread ya kina TUNTEMEKE na Masalia yao.

Mkuu Asprin,
Nipo nao hawa toka kule Great Thinkers. Nafyonza elimu tu hapa.
 
Last edited by a moderator:
Mpiga kura atakosaje kuwa na maslahi katika chaguzi za nchini mwake bana?

Nyani!

Nimeisoma mara 2 hukumu ya Mahakama ya rufaa kwenye "concurrence" iliyosainiwa na Jaji Nathalia Kimaro;hukumu hii haijatengua wala kufuta kutumika kwa kesi ya Chadiel Mgonja(1980)kwenye kesi za Uchaguzi hapo baadae!

Lkn Mahakama ya Rufaa imeona kuwa walalamikaji kwenye kesi ya Lema-Arusha WAMESHINDWA KUTHIBITISHA MAHAKAMANI ni vipi haki zao za msingi kama wapiga kura zilikiukwa!!

TUSICHANGANYE MAMBO:ktk Kesi ya LEMA wapiga kura hawa walikuwa wanalalamika kuwa Lema alimtukana Mama Batlida lkn wao wameshindwa kuthibitisha mahakamani matusi ya Lema kwa Mama Batlida ni kivipi yaliaathiri uchaguzi huo na ni vipi yaliwaathiri wao wenyewe kumchagua Mbunge wampendae?

Ni kweli ktk hukmu yao majaji wote 3 hamna aliyaendika "dissent"lkn hii haina maana kuwa kesi ya Mgonjwa haitatumika tena kwenye kesi za wapiga kura wakikimbilia mahakamani!

Kesi hii ya Lema haikuwa ya uchaguzi bali ni ya kashfa na hawa wapiga kura wametupotezea muda tu!Kesi ya Mgonja si iliamriwa kwenye ground ya baadhi ya wapiga kura halali kuzuiliwa kupiga kura?
 
Hawa wapiga kura pamoja na mambo mengine walilalamika kuwa Lema alitumia maneno machafu(matusi) kwa mgombea wao ndo maana akashindwa. Sasa mbona hakuna mahali ambapo Batilda alilalamika kwa tume kutukanwa achilia mbali kujakuthibitish hayo malalamiko mahakamani.

Pili waliofungua kesi ya arusha hakuna uthibitisho mahakamani kuwa ni wapiga kura wa Arusha mjini, ndo maana mahakama imepigilia nyundo kwa kila mpiga kura kufupinga ushindi wa mtu.

Kumbuka mahakama imesema uthibitisho wa kuwa wale walalamikaji wa tatu ni wapiga kura wa arusha mjini, wakili wao alitakiwa alete barua ya uthibitisho kutoa Tume ya Uchaguzi ikitamka hivyo. kwa tafsiri ya harakaharaka kesi ilifunguliwa na watu baki wasio wapiga kura wa arusha mjini
 
Anachosema Prof Shivji ndicho nilichosema mimi awali hapa, ukiondoa mfano wa kesi ya Chediel Mgonja.

Halafu angalia washabiki wa Lema watakavyokuja kijumlajumla bila uelewa wa nini kimepingwa.

Kimomogoro anachekesha. If anything mpiga kura anatakiwa awe na haki kuliko mgombea.

Mkuu ukiangalia kwa undani utaona tatizo lipo kwenye sheria yenyewe kwani sheria haionyeshi ni wapi ambapo mpiga kura haki yake ikikiukwa anahaki iko tu general tena inaonyesha mpiga kura yeyote bila kuzingatia hata kama alipiga kura au la au alijiandikishia wapi0 Maoni yangu hii sheria iangaliwe ili iboreshwe.
 
Wengine hatukushiriki sana kwenye huo mjadala lakini everytime I come across such blanket statement kama hii yako, I lose interest. Jaribu kuwapa breathing space watu usiokubaliana nao...mara wapenzi wa Chadema, mara wapenzi wa Dr. Slaa na sasa imeongezeka wapenzi wa Lema, duh, eti hawana uelewa wa nini kinachoongelewa. Kiranga nakuheshimu na nisingependa tujiingize kwenye nani zaidi bali tubakie kwenye kupingana kwa hoja...ni hayo tu, sasa tuendeleee. How I wish some of us had more time to participate kwenye mijadala mbalimbali but then...

Binafsi naamini kuna mambo ya kipuuzi tunayoyapa kipaumbele while in actual fact ni non issues from the word go. Sisi tuliobahatika kupata exposure kwa wenzetu ambako demokrasia imekomaa, no voter would dream of going to court to challenge an election result based on mgombea anayemtaka kushindwa uchaguzi kwa sababu alikashifiwa kwenye kampeni huku mhusika hayuko tayari hata kuwa shahidi mahakamani...it is stupid, ridiculous and makes no sense. Nina hakika hata mahakama ililiona hili kwamba ku"entertain" kitu kama hicho ni kuidhalilisha mahakama. Naamini hukumu iliyotolewa ilizingatia hilo.
Nimeyakuza na kuyapaka rangi maneno yako hapo juu ili kuonyesha msisitizo.. infact hizo ndio sifa zako kwa sababu huoni hata hoja iliyopo nyumba ya wanaopinga hukumu hii.. umeshindwa kuona jinsi mahakama ilivyopinda sheria(bila kujali uzuri au ubaya wa sheria husika) na umeshindwa kuona hata mawakili na wanasheria waliobobea wanapotoa matamshi kwaba"""" HAPA MAHAKAMA IMETUNGA SHERIA MPYA""""

Huoni kwamba kazi ya kutunga sheria sio ya mahakama bali kazi yake ni kutafsiri sheria iliyotungwa na bunge....... unaendekeza mapenzi/chuki kuliko mantiki na umepofushwa na ushabiki kiasi cha kutoona ukweli ulio wazi... pambana kwa hoja neno kwa neno na sio kukimbilia kuzikashifu sheria zilizopo bila kutoa ushauri wa jinsi tutakavyoziondoa katika maoni ya katiba ijayo..
 
Ritz inaingia akilini mwako mfano nitukanwe na Honey K halafu wewe Ritz uende kumshtaki mahakamani? Mbaya zaidi hata kunishirikisha mtukanwa kama shahidi isifanyeke, kwanini nirukwe hivyo mtukwanwa mwenye haki na hata kama `sijaonyesha dhamira ya kufungua mashtaka dhidi ya mtusi?

Mambo haya tuweke kwanza ushabiki wa kiitikadi kando tujadili kisheria na hata kama taaluma ya kisheria imetupiga chenga, lakini ile kitu inaitwa common sense tu Shvji ameteleza kidogo.

Hoja ya kujenga utetezi tokana na kesi ya Mgonja ni dhaifu katika maana kwamba upembuzi wa sheria na tafsiri hubadilika tokana nawakati, ndio maana kuna mabadiliko ya sheria mara kwa mara licha ya kuongeza mpya kwani wakati ukuta, vinginevyo tusingekuwa na baraza la kudumu la kutunga sheria, maana serikali haijakamilika bila uwepo wa bunge ambao ni mmoja ya mhimili muhimu wa serikali, mhimili ambayo ndio chimbuko la kutathmini mabadiliko ya miundo ya sheria nchini.

Matumaini yangu makubwa umenielewa ingawa unaweza kuja na jibu ambalo kwa sababu zako unaweza ukalitoa kinyume cha uelewa wako, lol.

Enjoyo Holiday Ritz!

Mkuu vipi kesi ya Mgoja mwaka 1980?
 
Prof.Shivji na Stolla yawezekana hawajaisoma hukumu vyema. Kabla ya yote,Mahakama ilijiridhisha kama Warufaniwa walikuwa wapiga kura waliandikishwa kisheria.Hapakuwa na ushahidi kulingana na Sheria ya Ushahidi. Kadi za wapiga kura hazikuwasilishwa kama ushahidi.Hivyo,hawakuwa wapiga kura waliosajiliwa(registered voters).Hapo ndipo Lema alipoibukia kidedea.
 
Kwa makusudi kabisa sitajadili maudhui ya hukumu ya Lema ingawa nimepitia nakala yake.Niseme wazi kuwa nina wasiwasi na nia ya gazeti la Mwananchi kuendelea kufuatilia uhalali ama ubatili wa hukumu ya Lema kisheria.

Nia yao ya wazi ni kuuza gazeti ili kupata faida kwa stori zinazoonekana zina mvuto kwa wananchi. Mtindo wa wanahabari kutafuta wanataaluma kupata maoni yao kuhalalisha matamanio na mitazamo yao haufurahishi na hauvumiliki. Habari husika ina upungufu kwa kuwa imekiuka moja ya miiko ya taaluma habari kwa kutoweka maoni ya wanasheria wengine wanaoridhishwa na hukumu husika mbali na wakili wetu Kimogoro.

Swali:Baada ya Lema kuvuliwa ubunge wake, April,''Mwananchi'' walitafuta maoni ya Shivji na wengine?Baada ya ile hukumu ya Mnyika, walitaka maoni ya wabobezi wa sheria? Na ile ya Igunga je? Vipi kuhusu ile ya Sumbawanga?

Labda niwaulize ''Mwananchi'':ule mwendelezo wa habari na makala za ''kikombe cha babu wa Loliondo'' umefikia wap?Tusingependa kuletewa tamthilia tena maana kwa hakika yapo masuala mengine ya msingi kujadili.

 
Hehehe. Mwalimu wangu aliyenifundisha maana na application ya locus standi nae anapinga?

Ngoja nikakague notes za lectures zake wakati anatufindisha hii kitu kama alisema the doctrine of locus standi does not apply to election litigation, let alone mentioning the case of Mgonja.

Mgonja was a good law until the CA said in Lema it wasn't.

It does not matter that Mgonja had been binding for 30 years. Tunazo sheria za muda mrefu mbovu nyingi tuu.

May be before Lema, the CA did not have an opportunity to consider whether Mgonja was a good law.

Bado haijaniingia akilini eti mtu aliyejiandikisha na kupigia kura Chake Chake anakuja kumshtaki diwani aliyeshinda uchaguzi Ngara eti kwa sababu anayo haki ya kufanya hivyo hata kama haki zake hazijawa affected.

Kesi ya Lema itazuia wanasiasa wenye uchu wa madaraka kujificha nyuma ya wapiga kura wa kawaida kufungua kesi halafu wakishindwa wanawakana inapofikia muda ya kulipia gharama za kesi.
sijasoma sheria hata moja ila hapo ndipo kwenye hoja ya msingi kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mpiga kura ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi, lakini katika mazingira yapi????

Malalamiko yaliyowasilishwa mahakamani na wapinga matokeo binafsi niliyaona yana walakini.

Wapiga kura wanalalamika kwamba mgombea wao alishindwa kwa vile alitukanwa kwamba ni side dish ya waziri mkuu wa zamani!!!!
Sasa sijui tamko hilo linamnyima kura vipi mgombea na linampa kura vipi aliyetamka na zaidi linawanyima haki wapiga kura vipi.

Kuna watu tunawaheshimu kwa mvi zao, lakini nadhani wakti umefika naamini wanatakiwa wakakojoe walale.

Well said Mkuu, lazima tujiuliza maswali hayo kama mgombea mwenyewe angefungua hii kesi hapo ingekuwa applied kuwa haki zake zimeadhiriwa kwani alidhalilishwa lakini akaja mjomba wake akadai kuwa haki zangu zimeadhiriwa kwakuwa ni tegemeo lake hapana hapo pana ukakasi wanasheria watu wanapaswa kusugua vichwa tena.
 
Mimi siyo Great Thinker kama Gaijin, EMT, au Bu'yaka :becky: lakini hiki anachosema Shivji hata kule kwenye jukwaa la hawa ma Great Thinkers nilikisema.

Mpiga kura atakosaje kuwa na maslahi katika chaguzi za nchini mwake bana?


naoma kujuzwa kilichosemwa kwenye kesi ni kuwa mpiga kura hana maslai katika uchaguzi wa nchi yake au yale matusi ndio hayakuwaathiri wapiga kura na hivyo kukosa haki kisheria ya kufungua kesi. na haswa ikizingatiwa kuwa walishinda kupeleka ushahidi wa matusi hayo kama yalkikuwepo au la?
 
Wakuu EMT na Jokakuu,

Mimi nawaheshimu sana na sisi wote ni brothers na makomredi ambao watu wanatusoma hapa, na ninyi ni wanasheria.

Sasa ni lazima tulenge kwenye principles kwamba mzee Shivji amekurupuka na hoja yake.

Kama alivyotanabaisha JokaKuu kwamba kesi ya Mgonja ilihusu madai kwamba kulikuwepo rushwa na hii kesi ya Mheshimiwa Lema ilikuwa na madai tofauti.

Kimogoro amesema sheria hampi haki mwanchi kumshitaki mtoa rushwa kwenye uchaguzi akaulizwa na mwananchi vipi mpiga kura anaweza kumshitaki akasema ngoja ariew sheria ha ha pana tatizo kwenyesheria yenyewe.
 
Hapana! Pamoja na kwamba sikubaliani na argument ya Prof. Shivji sidhani kama amewatusi majaji waliotoa hukumu.

It is normal in the legal field to criticise court judgements. Ndiyo maana kwenye nchi za watu controversial decision kama hii inazalisha articles hata 500 within the first few months, some applauding, others, criticising, the decision.

It is normal kabisa na kufanya hivyo haina maana kuwa mtu ana-question intergrity ya jaji aliyetoa hukumu.

Tumefundishwa kukubaliana kutokubaliana. Kwa vile sijakubaliana na wewe haina maana kuwa nimekudharau au nimekutusi.

You will still be my learned brother/sister. lol.

Shivji amechemka sana kwenye hili hukumu ya CAT hainyimi wapiga kura haki ya kushtaki au kupinga matokeo ila imeweka vigezo lazima mpiga kura awe ameadhirika na athibitishe ameadhirika vipi kabla hajafungua kesi,kwa hiyo haki ya kupinga ipo ila sio kil mtu bila sababu THERE IS NO ROOM FOR BUSY BODIES IN COURT OF LAW
 
Walichokifanya mahakama ya rufaa ni kuidhibitisha kauli ya kisheria "NO ROOM FOR BUSY BODIES" mpiga kura hajanyimwa haki ya kupinga matokeo ila awe ameadhirika moja kwa moja na aweze kuthibitisha hilo
 
Ningemuona Shivji wa maana kama angeanzisha mjadala kwanza kwa hukumu ya jaji Rwakibarila,
ya kutoa hukumu wrong ya kumzuia Lema kushiriki siasa,je ilikuwa sahihi?kwa nini hakuanza na
hili kwanza,Jibu ni:MNAFIKI"
 
1. Mahakama inaweza kutunga sheria kutokana na hukumu zake. Wakina shivji wakasome hukumu za judge Demining wa uingereza jinsi hukumu zake zilivhotengeneza sheria nyingi za jumuia ya madola. Kama kulikuwapo na hukumu ya 1980 inamaana haiwezi kutenguliwa tena?
2. Mahakama haikusema wapiga kura hawana haki ila hicho walichofungulia kesi ndio kina ulakini. Kumbuka wale wanaharakati waliofungua kesi ya kugomea malipo ya dowans mahakama ilisema wazi kuwa hawana haki kwa vile sio party to the contract. Lakini hao wanaharakati na watanzania wote ni walipa kodi na tuna haki wao hawakuliona hilo? Mahakama zimeweka utaratibu kuwa lazima uwe muadhirika au ufungue kesi kwa niaba ya mwadhirika kwa ridhaa yake. Au mtu ukiona jirani amewekewa X unaweza kwenda mahakamani kupinga kwa vile utapoteza jirani? Mwadhirika wa kesi hakwenda mahakamani na kesi ya kutukana kama ni kweli wangepaswa wapeleke polisi ili jamhuri imfungulie shitaka la jinai. Kama mwanachi anaweza kufungua mashitaka ya jinai basi hata wanachi wafungue kesi za watuhumiwa wa epa si wote ni waadhirika na tuna haki na kodi zetu?

UMEMALIZA KILA KITU.SHIVJI Anazeeka vibaya baada ya kutoswa na JK ujumbe wa katiba mpya.
 
tunawasubiri wanasheria mliobobea sheria niliyosoma ni kidogo sana nika ilikuwa yakunilinda kwenye mikataba tu na ufanyaji wa kazi sehemu mbalimbali
 
Back
Top Bottom