Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Kwa makusudi kabisa sitajadili maudhui ya hukumu ya Lema ingawa nimepitia nakala yake.Niseme wazi kuwa nina wasiwasi na nia ya gazeti la Mwananchi kuendelea kufuatilia uhalali ama ubatili wa hukumu ya Lema kisheria.

Nia yao ya wazi ni kuuza gazeti ili kupata faida kwa stori zinazoonekana zina mvuto kwa wananchi. Mtindo wa wanahabari kutafuta wanataaluma kupata maoni yao kuhalalisha matamanio na mitazamo yao haufurahishi na hauvumiliki. Habari husika ina upungufu kwa kuwa imekiuka moja ya miiko ya taaluma habari kwa kutoweka maoni ya wanasheria wengine wanaoridhishwa na hukumu husika mbali na wakili wetu Kimogoro.

Swali:Baada ya Lema kuvuliwa ubunge wake, April,''Mwananchi'' walitafuta maoni ya Shivji na wengine?Baada ya ile hukumu ya Mnyika, walitaka maoni ya wabobezi wa sheria? Na ile ya Igunga je? Vipi kuhusu ile ya Sumbawanga?

Labda niwaulize ''Mwananchi'':ule mwendelezo wa habari na makala za ''kikombe cha babu wa Loliondo'' umefikia wap?Tusingependa kuletewa tamthilia tena maana kwa hakika yapo masuala mengine ya msingi kujadili.


Nakuongeza na LIKE tena" Nimekasirika sana leo kununua gazeti hili la kipuuzi na kukuta kilichoandikwa humo,lengo la Mwananchi ni mwendelezo wa habari zao za kujipeleka kaburini bila kujua,kwa kuwaza wanaweza kucheza na akili za watanzania kwa habari zinazouza gazeti lakini hazina mashiko yoyote,

Ni kwa nini hawakumhoji Shivji juu ya hukumu ya jaji Rwakibarila? na huyu Mzee kwa sababu amekuwa mnafiki sawa na lengo la aliyemhoji akajiingiza kwenye mkenge,Hivi suala la mtu kuitwa nyumba ndogo kuliathiri vipi haki ya mpiga kura na kumnyima ushindi mgombea wake,hata kama sijui sheria hapa Mzee Shivji amechemka.
 
Aliyejiandikisha Chake Chake ana haki ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Karatu kisheria, kwa sababu kimantiki Mbunge wa Karatu akiwa Bungeni atajadili na kuya-impact maisha ya Chake Chake.

Pia ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha sheria za nchi zinatekelezwa

Msomi Wangu Gaijin,

CA ililiona hilo na ndiyo maana ikatoa ufafanuzi huu:

" So a voter has no right to petition and challenge the election results where his rights were not infringed. Section 111(1) (a) of the Act reads:- 111(1) An election petition may be presented by one or more of the following persons, namely-: (a) a person who lawfully voted or had a right to vote at the election to which the election petition relates.

Currently the rule in Tanzania has been extended to cater for matters of public interest under Article 26(2) of the Constitution then a citizen of this country has locus standi to sue for the benefit of the society. And the test whether a litigation is of public interest depends on the nature of the relief sought and its effect. In Rev. Christopher Mtikila V Attorney General [1995J TLR 31 Lugakingira, J (as he was then) observed what a public interest litigation is.

He said:-
II In matters of public interest litigation this court will not deny standing to a genuine and bona fide litigant even where he has no personal interest in the matter." He went on the say :- II It is not the type of litigation which meant to satisfy the curiosity of the people, but it is a litigation which is instituted with a desire that the court would be able to give effective relief to the whole or a section of the society" In common law in order for one to succeed in an action, he must not only establish that his rights or interests were interfered with but must also show the injury he had suffered above the rest.

In The Attorney General v The Malawi Congress Party and
another, Civil Appeal No. 22 of 1996, the Malawian Supreme Court of Appeal provided the test for locus standi. It said:- II Locus Standi is a jurisdictional issue. It is a rule of equity that a person cannot maintain a suit or action unless he has an interest in the subject of lt; that is to say unless he stands in a sufficient close relation to it so as to give a right which requires prosecution or infringement of which he brings the action"

In our case the issue for consideration and decision is whether or not a registered voter under section 111(1)(a) of the Act has an absolute right to challenge the election result even where his rights were not infringed. We have given a deep thought to the matter. First, we wish to point out that election petitions are not in our view public interest litigation though they are matters of great public importance.

This is because the relief sought would not benefit the entire society as a whole. Second the petition was not brought under Article 26(2) of the Constitution which permits any person to bring a public interest litigation. The Article provides:-
26(2) Every person is entitled, subject to the procedure provided for by the law, to institute proceedings for the protection of the constitution and legality. Since an election petition is not a public interest litigation we do not read the section to have done away with the rule of locus standi.

We think in our view, section 111(1)(a) of the Act give rights to registered voter whose rights to vote have been interfered with or violated. In case violation effects the candidate it is for the candidate to challenge the election because his rights were violated. To give the section a broader interpretation that he has an absolute right to petition even where his rights were not interfered with is to defeat the well established principle of law of locus standi and indeed it does not sound well. We are not prepared to do so."
 
Nimesoma maelezo ya Prof. Shivdi kisha nikalinganisha hiyo sheria na hukumu ya Lema, bila kumumunya maneno Prof.Shivdi katika hili AMEPOTOKA KABISA.
Kwa sababu vifuatazo;

(1)Mpiga kura na mgombea hawana haki sawa kisheria katika uchaguzi. Haki za mgombea ni kubwa zaidi ya haki za mpiga kura
(eg.Sio kila mpiga kura ana haki ya kuwa mgombea lakini wagombea wote wana haki zote za mpiga kura)

(2)Haki ya mpiga kura ni kujiandikisha na kupiga kura tu, wakati mgombea ana haki zote za mpiga kura(Kujiandikisha na kupiga kura) Plus haki ya kupiga kampeni, kusimamia zoezi la upigaji kura, kuhesabu kura na kutangazwa matokeo nk.

(3)Hakuna haki yoyote ya mpiga kura(Kujiandikisha na kupiga kura) iliyoelezwa kuvunjwa katika uchaguzi ule katika kesi hii na wafungua kesi.

(4)Wafungua kesi walikosea sana walipoamua kubeba jukumu la mgombea(Kudai kudhalilishwa kwa mgombea wa CCM wakati wa *KAMPENI) wakati wao ni wapiga kura, hivyo wanakosa nguvu ya kisheria kudai na kuhoji haki isiyowahusu.

*KAMPENI ni jukumu na haki ya mgombea na chama chake tu na sio jukumu au haki ya msingi ya mpiga kura kisheria.
 
Mimi siyo Great Thinker kama Gaijin, EMT, au Bu'yaka :becky: lakini hiki anachosema Shivji hata kule kwenye jukwaa la hawa ma Great Thinkers nilikisema.Mpiga kura atakosaje kuwa na maslahi katika chaguzi za nchini mwake bana?
Nyani Ngabu et al. mimi sio mwanasheria, lakini nikiwa kama layman sitopenda mtu aende mahakamani kufungua shauri la kutengua matokeo ya uchaguzi ikiwa haki yake kama mpiga kura haikufinywa.

La sivyo na mpiga kura mwingine anaweza akaenda Mahakamani kupinga mpinga matokeo kutaka kufinya haki yake, na yeye akiwa kama mpiga kura.

Tukiruhusu kitu kama hicho, itakuwa gharama sana kwa serikali yetu, na zaidi; tunaingilia haki za wapiga kura wengine wengi ambao wanaona haki zao kama wapiga kura walizipata ipasavyo, na hivyo kutoamua kufungua kesi mahakamani.
 
Mimi nadhani mahakama ya rufani hoja yake ya msingi ingejikita katika uthibitisho je wale wapiga kura waliathiriwa vipi na mtokeo ya uchaguzi. Election has public interests. Nakuhusu haki ya mpiga kura kushtaki mahakama ilitakiwa ieleze kwamba mpiga kura ataruhusiwa kufungua kesi endapo; 1. Haki ya mpiga kura binafsi zimeathiriwa. 2. Kama kuna vitendo vyovyote ambavyo vilifanyika na mpiga kura anaweza KUTHIBITISHA kwamba vitendo vile vilimuathiri yeye pamoja na uchaguzi kwa ujumla. Hapa akiwa na uwezo wa kuthibitsha alivyoathiriwa then he/she should have Locus stand. N:B Endapo kufungua kesi katika masuala ya uchaguzi itakuwa haki kamili ya mpiga kura bila kuonesha ni vipi ameathiriwa basi kutakuwa na mrundikano wa kesi ambazo zitakuwa zipo mahakaman muda mrefu maana huyu atakuwa anafungua kwa jambo hili, kesho mwingine ataibuka na jambo lingine na hii inatokana na siasa za Tanzania si za kidemokrasia bali za kukomoana.
Nadhani hao tunaowajua kuwa ni wanasheria waliobobea ndipo hapa hawapaangalii vizuri. Naomba waangalie maelezo yako kwa sawa sawa. Suala la kutumia maneno ya Kashifa haiwezi kuhathiri haki ya mpiga kura, bali inaweza kumuathiri mgombea na ndiye alitakiwa kulalamikiwa.

Kashifa anaweza kuielewa mkashifiwa maana ndiye anayejua ukweli wake yeye mwenyewe. Kwa mtu mwingine hawezi kujua kuwa mtu kakashifiwa maana huenda yaliyotamkwa ni ukweli na kwa hii naweza kusema kuwa huenda yanayotafsiriwa kuwa kashifa siyo kashifa ndiyo maana mgombea mwenyewe hakulalamika.

Majaji wa mahakama ya Rufaa walitumia hekima ya hali ya juu. Sikatai kuwa wanasheria wetu wanaotoa hoja za kukosoa hukumu siyo wasomi, la niwasomi haswa ila wanakosa component moja katika ubobeaji wao. Wanafalsafa kuna kitu wanaita Pragmatism katika elimu, kwa maana kuwa elimu anayoipata mtu imwezeshe kuendana na hali inayobadirika badirika na siyo kwa kuwa hukumu ilitolewa na itaendelea kuwa hivyo hivyo.

In pragmatic Philosophy they say that there is no absolute truth. Hebu tuwe tayari kubadilika kulingana na mabadiliko. Heri ya Mwaka Mpya
 
"Lakini Profesa Shivji aliitetea hukumu hiyo ya Mgonja akisema imekuwapo kwa zaidi ya miaka 30 sasa na kwamba kwa muda wote huo imekuwa ikifuatwa katika uamuzi wa mashauri mbalimbali, huku akisisitiza kuwa Mahakama haiwezi kuifuta kirahisi tu."

Mimi siyo mwanasheria, lakini kwa tafsiri rahisi tu, sidhani kama hii ni sahihi kama anavyosema Prof. Shivji!
 
Ni jambo zuri kulijadili ili hatimae tuwe na uelewa na kujua vitu ambavyo mwisho wa siku si kwa maslahi ya jamii fulani tuu bali taifa zima.

Hoja ya Shivji na wanasheria wengine ni ya msingi kama mahakama imeondoa au kuzuia haki ya mpiga kula kufungua kesi za uchaguzi.

Hoja nyingine ninavyoiona ni kama mpiga kura ana haki hiyo basi ni kwa wakati au mazingira gani au ni haki hisiyo na mipaka.

Nionavyo tutafika mahali tutakuwa na jibu juu ya suala hili ila Tuwe makini Shivji hapingi Lema kushinda ila ana concern na haki ya mpiga kula.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hivi hapa tatizo ni gazeti au ni Shivji?

Maamuzi ya kesi ya Lema yalikuwa na sura kuu mbili tu,

1) Waliathirika vipi na kile kilichodaiwa ni matusi? (Na hapa alistahili kusimama mtukanwaji sio vinginevyo)

2) Matusi hayo yaliathiri vipi mwenendo MZIMA wa uchaguzi?

Ninawasiwasi gazeti limepotosha maelezo ya Prof Issa Shivji makusudi.
 
Hehehe. Mwalimu wangu aliyenifundisha maana na application ya locus standi nae anapinga?

Ngoja nikakague notes za lectures zake wakati anatufindisha hii kitu kama alisema the doctrine of locus standi does not apply to election litigation, let alone mentioning the case of Mgonja.

Mgonja was a good law until the CA said in Lema it wasn't.

It does not matter that Mgonja had been binding for 30 years. Tunazo sheria za muda mrefu mbovu nyingi tuu.

May be before Lema, the CA did not have an opportunity to consider whether Mgonja was a good law.

Bado haijaniingia akilini eti mtu aliyejiandikisha na kupigia kura Chake Chake anakuja kumshtaki diwani aliyeshinda uchaguzi Ngara eti kwa sababu anayo haki ya kufanya hivyo hata kama haki zake hazijawa affected.

Kesi ya Lema itazuia wanasiasa wenye uchu wa madaraka kujificha nyuma ya wapiga kura wa kawaida kufungua kesi halafu wakishindwa wanawakana inapofikia muda ya kulipia gharama za kesi.
Safi kamanda wanaopinga hukumu hii inawezekana hawajaisoma kwa makini, CA ilichokifuta ni kwa mpiga kura kuwa absolute rights of litigation in election matters. Lakini wanavyochangia ni as if CA imefuta kabisa haki ya mpiga kura kufungua kesi ya uchaguzi hata pale ambapo haki zake kama mpiga kura zimevunjwa
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hivi hapa tatizo ni gazeti au ni Shivji?

Maamuzi ya kesi ya Lema yalikuwa na sura kuu mbili tu,

1) Waliathirika vipi na kile kilichodaiwa ni matusi? (Na hapa alistahili kusimama mtukanwaji sio vinginevyo)

2) Matusi hayo yaliathiri vipi mwenendo MZIMA wa uchaguzi?

Ninawasiwasi gazeti limepotosha maelezo ya Prof Issa Shivji makusudi.
Nakuunga mkono asilimia 100 kamanda.
 
Ndiyo hawahawa watatuabia tukubaliane na ushoga na kuutetea kisheria sababu tu UK wanafanya hivyo kutokkaka na sheria zao tunazozifuata pia katika maamuzi yetu.
 
Mkuu EMT unaweza kusoma hapa na hii ndio basis ya uamuzi wa majaji hao kwenye kesi hii.

Katika uamuzi wake Mahakama ya Rufani ilisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi iwapo vitambulisho vya wapiga kura viliwasilishwa na kupokewa mahakamani na ikaenda mbali zaidi kwa kutilia shaka jinsi rekodi ya kadi hizo zilivyochukuliwa.
Ilisema kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajiburufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao nOwdiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.


Ilisema Wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughway aliwasilisha kadi za wateja wake kwa Jaji Aloyce Mujulizi kuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali, lakini Mahakama hiyo ikasisitiza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na wamiliki wa nyaraka husika.

Ilisema hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake."





Thanks GT, kwa maoni yangu msingi hasa wa uamuzi wa majaji wa mahakama ya rufaa kwa maoni yangu ulijikita kwenye hoja kuwa wajibu rufani hawakuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali kwa kujumuisha vielelezo.
 
EMT,

..lakini malalamiko dhidi ya Mgonja yalihusisha masuala ya rushwa.

..wakati hii ya Lema inahusisha matamshi aliyoyatoa wakati wa kampeni ambayo wapiga kura watatu wanaamini ni kashfa na wameathirika.

Wameathirika vipi mkuu????
Kumbuka hata anayedaiwa kutukanuwa hakuathirika na hakutaka hata kuwa shahidi kwenye hiyo kesi.


 
(Kutoka gazeti la mwananchi)
MWANAZUONI aliyebobea katika sheria, Profesa Issa Shivji na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stolla wamekosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, wanasheria hao walisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu wakiongozwa na Nathalia Kimaro, Salum Massati na Bernard Luanda, inapingana na sheria.

Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa Lema, Method Kimomogoro amepinga madai hayo akisema wanaoipinga pengine hawajapata nafasi ya kuliangalia kwa undani suala la haki ya mpiga kura kupinga matokeo mahakamani.

Profesa Shivji kwa upande wake alieleza kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.
Alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi, Katiba ya nchi na Mahakama, vinampa haki mpiga kura kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi.

“Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta haki hiyo ya mpiga kura,” alisema Profesa Shivji.

Katika shauri hilo namba 84 la mwaka 1980 lililofunguliwa na William Bakari na mwenzake dhidi ya Mgonja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mahakama Kuu Tanzania iliamua kuwa, mpiga kura ana haki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Walalamikaji walishinda.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani katika kesi ya Lema, iliamua kwamba hukumu katika kesi ya Mgonja ilikosewa kwani si sahihi kwamba mtu yeyote bila kujali mahali alipojiandikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo katika jimbo lolote nchini hata kama haki zake hazijakiukwa kwa namna yoyote.

Lakini Profesa Shivji aliitetea hukumu hiyo ya Mgonja akisema imekuwapo kwa zaidi ya miaka 30 sasa na kwamba kwa muda wote huo imekuwa ikifuatwa katika uamuzi wa mashauri mbalimbali, huku akisisitiza kuwa Mahakama haiwezi kuifuta kirahisi tu.

Profesa Shivji alisema mpiga kura ni mwananchi na kwa vyovyote ana masilahi katika uchaguzi husika na hivyo anatarajia kuona uchaguzi ambao ni huru na wa haki.
“Hivyo huwezi kusema hahusiki na nani kashinda au kashindwa kwa kuwa uchaguzi ni muhimu katika kujenga na kukuza demokrasia,” alisema Profesa Shivji.

Chama cha Wanasheria
Kwa upande wake, Stolla alisema: “Nimesikiliza hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutofurahishwa na tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge’ (kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani,” alisema na kuongeza:
“Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, sababu ya kuwa mpiga kura ni ipi nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?”

Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

“Mwaka 2002, sheria zote zilifanyiwa marekebisho na baadaye mwaka 2005, Bunge likatunga sheria mpya inayoitwa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ikafuta ya mwaka 1985. Sheria hiyo na marekebisho yake, ndiyo inayotawala uchaguzi hadi sasa,” alisema.

Alisema hata kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo ya Uchaguzi ya mwaka 1985, tayari kulikuwa na uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja ambayo iliamua kuwa mpiga kura ana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

“Uamuzi wa kesi ya Mgonja ulikuja ‘ku-reflect’ (kuakisi) hata kwenye Sheria ya Bunge ya mwaka 1985. Tangu hukumu hiyo ya Mgonja hakuna uamuzi mwingine wa Mahakama ambao umeshautengua huo, ndiyo maana hata wanasheria wanashangaa uamuzi huu wa Mahakama ya Rufani,” alisema.

Alisema kumekuwa na kesi nyingi mahakamani za wapiga kura kupinga matokeo na kwamba nyingine hata yeye amezisimamia na hakuna wakati ambao Mahakama imewahi kusema kuwa hawana haki hiyo.

Alitoa mfano wa kesi iliyofunguliwa na wapiga kura dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Mbulu, Phillip Marmo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Alisema kesi hiyo ilishindwa kuendelea kutokana na wapiga kura hao kushindwa kuweka mahakamani fedha ya amana kwa ajili ya kuiendesha na si kwa sababu hawakuwa na haki.

Akizungumzia hoja ya Mahakama ya Rufani kuwa hapakuwa na ushahidi kama walalamikaji walikuwa wapiga kura, Stolla alisema hilo halikuwa na ulazima kwa kuwa halikuwa jambo lililokuwa likibishaniwa.

“Hata hivyo, kabla ya kuanza kesi Mahakama Kuu, Jaji Mujulizi (Aloyce) aliitisha vithibitisho ili kujiridhisha kama ni wapiga kura,” alisema Stolla na kuongeza:
“Lakini Mahakama ya Rufani wenyewe walianza kutafuta kama liliibuka Mahakama Kuu na licha ya Mahakama Kuu kuonyesha kuwa ilijiridhisha katika hilo, wao wakakosoa kuwa uthibitisho huo ulipaswa uwe sehemu ya mwenendo.”

Katika uamuzi wake Mahakama ya Rufani ilisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi iwapo vitambulisho vya wapiga kura viliwasilishwa na kupokewa mahakamani na ikaenda mbali zaidi kwa kutilia shaka jinsi rekodi ya kadi hizo zilivyochukuliwa.

Ilisema kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajiburufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao ndiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.

Ilisema Wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughway aliwasilisha kadi za wateja wake kwa Jaji Aloyce Mujulizi kuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali, lakini Mahakama hiyo ikasisitiza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na wamiliki wa nyaraka husika.

Ilisema hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake.

Mugway ashangaa
Wakili Alute Mughway aliyekuwa akiwatetea wajibu rufaa katika rufaa hiyo, alisema Mahakama imeacha jukumu lake la kutafsiri sheria na badala yake ikatunga sheria mpya ambayo inapingana na Sheria ya Bunge na Katiba ya nchi, Ibara ya 26 (2).

Alisema Kifungu cha 111 (1) cha Sheria ya Uchaguzi, Hukumu ya kesi ya Mgonja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinampa haki mpiga kura kufungua shauri mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi.

Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, miongoni mwa watu wanaoweza kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi ni aliyepiga kura au aliyekuwa na haki ya kupiga kura na kwamba tangu wakati huo kifungu hicho hakijawahi kufanyiwa marekebisho.

Wakili wa kujitegemea, Vedasto Audax alikaririwa na gazeti dada la The Citizen akisema: “Swali langu ni kwamba ni lini uamuzi wa kesi ya Mgonja ulionekana kuwa na makosa kisheria? Ni kuanzia leo baada ya Mahakama ya Rufani kutamka kuwa una makosa?”

Wakili wa Lema
Kimomogoro alisema hukumu ya kesi ya Mgonja haijitoleshelezi kwa sababu haikusema ni katika mambo gani mpiga kura ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo mahakamani huku akisema kwa maoni yake, anakuwa na haki pale tu haki zake kama mpiga kura zinapokiukwa.

“Mpiga kura hawezi kuwa na haki sawa na mgombea. Mgombea haki zake ni kubwa kuliko mpiga kura kwa sababu kwanza yeye ni mpiga kura na pili ni mgombea,” alisema na kuongeza:

“Ndiyo maana mpiga kura anaruhusiwa kupiga kura katika kituo kile alichojiandikisha tu lakini mgombea huweza kupiga kura katika kituo chochote.”

Alisema mwananchi wa kawaida tu ambaye hajajiandikisha hata kama akimwona mgombea akitoa rushwa hadharani, hana haki ya kufungua kesi mahakamani, lakini alipoulizwa kwa upande wa mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura alisema hakuwa na rejea za sheria kwa kuwa alikuwa Karagwe kwa mapumziko.

Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Buriani.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.

Lema alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kuikubali.

Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.
“Hivyo mpiga kura hana haki ya kisheria kufungua kesi kuhoji matokeo ya uchaguzi pale ambapo haki zake hazikukiukwa,” ilisema Mahakama ya Rufani.

Ilisema kwa mujibu wa Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya Tanzania, raia anakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi kwa masilahi ya jamii, kama ilivyotokea katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa SerikaIi ya mwaka 1995.

Ilisema kesi dhidi ya Lema haikufunguliwa chini ya Ibara ya 26 (2) ambayo inampa fursa na haki raia yeyote kufungua shauri mahakamani lenye masilahi ya umma, huku ikisisitiza kuwa madai ya wajibu rufani katika kesi hiyo hayagusi masilahi ya jamii yote.

Hoja zilizorudisha Ubunge wa Lema ni hizi hapa
Hizi ndio hoja za Kisheria zilizorudisha Ubunge wa Lema - YouTube
 
Anachosema Prof Shivji ndicho nilichosema mimi awali hapa, ukiondoa mfano wa kesi ya Chediel Mgonja.

Halafu angalia washabiki wa Lema watakavyokuja kijumlajumla bila uelewa wa nini kimepingwa.

Kimomogoro anachekesha. If anything mpiga kura anatakiwa awe na haki kuliko mgombea.

Hata kama Shivji yuko sahihi kuhusu haki ya mpiga kura, bado kesi husika ilikuwa ya kutunga na hawakuweza kuthibitisha madai yao! Pure CCM political games! Ni kupoteza wakati kujadili case zinazotungwa LUMUMBA!
 
Hivi mpiga kura aliyejiandikisha kata ya segerea jimbo la ukonga, anayo haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Kibakwe, kwa kuwa alipita Mtera akakuta Simbachawene akimkashifu mpinzani wake katika kampeni? Kama ndivyo sheria zinavyotaka, itakuwa vurugu tupu.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom