Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Hivi mpiga kura aliyejiandikisha kata ya segerea jimbo la ukonga, anayo haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Kibakwe, kwa kuwa alipita Mtera akakuta Simbachawene akimkashifu mpinzani wake katika kampeni? Kama ndivyo sheria zinavyotaka, itakuwa vurugu tupu.

yap inawezekana kabisa. nakupa mfano mwingine kama ulivyosema unatoka jimbo la segerea ukafika kibakwe ukashuhudia live mgombea wa huko anatoa rushwa waziwazi, utanyamaza kisa si mgombea wa jimbo lako?. Kwa kifupi wanyonge hatuna haki tena. bora hata SHIVJI na wenzake wameliona hili na wajanja sasa hatupigi kura ng'o kwa sababu hata kama ukidhulumiwa huna pa kulalamika.
 
Shivja anaijadili sheria ilivyo lakini hakuangalia sheria hiyo katika uchaguzi huo wanaopinga matokea waliathiriwaje na madai yao kitu ambacho mahakama imeegemea kutoa hukumu yake. Hao wapiga kura hawakutukanwa na Lema sasa wanasimamaje kudai haki mahakamani wakati aliyetukanwa hakulalamika wala kuwa mmoja wapo wa mashahidi. Pamoja na ugwiji wa sheria katika hali kachemka sana.

:becky: kweli mkuu babu kachemka
 
Hata kama Shivji yuko sahihi kuhusu haki ya mpiga kura, bado kesi husika ilikuwa ya kutunga na hawakuweza kuthibitisha madai yao! Pure CCM political games! Ni kupoteza wakati kujadili case zinazotungwa LUMUMBA!

Hayo sasa ni maneo ya ma-layman kama wewe, huna sababu ya kutuondoa katika msindi wa mada iliyoko hewani. Haijalishi kesi imetungwa LUMuMBA au hukumu imeandaliwa MTAA WA UFIPA KINDONI, hoja ya msingi ni Mpiga kura hana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi? na siyo kutuletea maneno ya vichwa visvyo na shule kama wewe.
 
Shivji kachemka kweli, coz haki ya kufungua kesi ya kupinga ushindi wa mbunge aliechaguliwa na umma na mtu ambaye haki zake si za mojakwa moja ingekuwa ni kuvunja haki za umma wa waliowengi. Ni mwathirika moja kwa moja ndie mwenye haki ya kufungua kesi
 
Hivi hapa tatizo ni gazeti au ni Shivji?

Maamuzi ya kesi ya Lema yalikuwa na sura kuu mbili tu,

1) Waliathirika vipi na kile kilichodaiwa ni matusi? (Na hapa alistahili kusimama mtukanwaji sio vinginevyo)

2) Matusi hayo yaliathiri vipi mwenendo MZIMA wa uchaguzi?

Ninawasiwasi gazeti limepotosha maelezo ya Prof Issa Shivji makusudi.

Yaani hapo wewe hujaelewa nini? ni wazi kuwa hukumu imemnyima haki mpiga kura. Hilo lingezingatiwa kwanza ni wazi matusi yale yalikuwa na effect kubwa tu katika mwenendo mzima wa uchaguzi na ndiyo maana tume ya uchaguzi katika sheria zake jambo mojawapo inalolisisitiza ni kufanya kampeni za kistaarabu kwa sababu wanajua madhara ya kampeni zisizo za kistaarabu.
 
(Kutoka gazeti la mwananchi)
MWANAZUONI aliyebobea katika sheria, Profesa Issa Shivji na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stolla wamekosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, wanasheria hao walisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu wakiongozwa na Nathalia Kimaro, Salum Massati na Bernard Luanda, inapingana na sheria.

Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa Lema, Method Kimomogoro amepinga madai hayo akisema wanaoipinga pengine hawajapata nafasi ya kuliangalia kwa undani suala la haki ya mpiga kura kupinga matokeo mahakamani.

Profesa Shivji kwa upande wake alieleza kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.
Alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi, Katiba ya nchi na Mahakama, vinampa haki mpiga kura kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi.

“Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta haki hiyo ya mpiga kura,” alisema Profesa Shivji.

Katika shauri hilo namba 84 la mwaka 1980 lililofunguliwa na William Bakari na mwenzake dhidi ya Mgonja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mahakama Kuu Tanzania iliamua kuwa, mpiga kura ana haki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Walalamikaji walishinda.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani katika kesi ya Lema, iliamua kwamba hukumu katika kesi ya Mgonja ilikosewa kwani si sahihi kwamba mtu yeyote bila kujali mahali alipojiandikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo katika jimbo lolote nchini hata kama haki zake hazijakiukwa kwa namna yoyote.

Lakini Profesa Shivji aliitetea hukumu hiyo ya Mgonja akisema imekuwapo kwa zaidi ya miaka 30 sasa na kwamba kwa muda wote huo imekuwa ikifuatwa katika uamuzi wa mashauri mbalimbali, huku akisisitiza kuwa Mahakama haiwezi kuifuta kirahisi tu.

Profesa Shivji alisema mpiga kura ni mwananchi na kwa vyovyote ana masilahi katika uchaguzi husika na hivyo anatarajia kuona uchaguzi ambao ni huru na wa haki.
“Hivyo huwezi kusema hahusiki na nani kashinda au kashindwa kwa kuwa uchaguzi ni muhimu katika kujenga na kukuza demokrasia,” alisema Profesa Shivji.

Chama cha Wanasheria
Kwa upande wake, Stolla alisema: “Nimesikiliza hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutofurahishwa na tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge’ (kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani,” alisema na kuongeza:
“Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, sababu ya kuwa mpiga kura ni ipi nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?”

Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

“Mwaka 2002, sheria zote zilifanyiwa marekebisho na baadaye mwaka 2005, Bunge likatunga sheria mpya inayoitwa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ikafuta ya mwaka 1985. Sheria hiyo na marekebisho yake, ndiyo inayotawala uchaguzi hadi sasa,” alisema.

Alisema hata kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo ya Uchaguzi ya mwaka 1985, tayari kulikuwa na uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja ambayo iliamua kuwa mpiga kura ana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

“Uamuzi wa kesi ya Mgonja ulikuja ‘ku-reflect’ (kuakisi) hata kwenye Sheria ya Bunge ya mwaka 1985. Tangu hukumu hiyo ya Mgonja hakuna uamuzi mwingine wa Mahakama ambao umeshautengua huo, ndiyo maana hata wanasheria wanashangaa uamuzi huu wa Mahakama ya Rufani,” alisema.

Alisema kumekuwa na kesi nyingi mahakamani za wapiga kura kupinga matokeo na kwamba nyingine hata yeye amezisimamia na hakuna wakati ambao Mahakama imewahi kusema kuwa hawana haki hiyo.

Alitoa mfano wa kesi iliyofunguliwa na wapiga kura dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Mbulu, Phillip Marmo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Alisema kesi hiyo ilishindwa kuendelea kutokana na wapiga kura hao kushindwa kuweka mahakamani fedha ya amana kwa ajili ya kuiendesha na si kwa sababu hawakuwa na haki.

Akizungumzia hoja ya Mahakama ya Rufani kuwa hapakuwa na ushahidi kama walalamikaji walikuwa wapiga kura, Stolla alisema hilo halikuwa na ulazima kwa kuwa halikuwa jambo lililokuwa likibishaniwa.

“Hata hivyo, kabla ya kuanza kesi Mahakama Kuu, Jaji Mujulizi (Aloyce) aliitisha vithibitisho ili kujiridhisha kama ni wapiga kura,” alisema Stolla na kuongeza:
“Lakini Mahakama ya Rufani wenyewe walianza kutafuta kama liliibuka Mahakama Kuu na licha ya Mahakama Kuu kuonyesha kuwa ilijiridhisha katika hilo, wao wakakosoa kuwa uthibitisho huo ulipaswa uwe sehemu ya mwenendo.”

Katika uamuzi wake Mahakama ya Rufani ilisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi iwapo vitambulisho vya wapiga kura viliwasilishwa na kupokewa mahakamani na ikaenda mbali zaidi kwa kutilia shaka jinsi rekodi ya kadi hizo zilivyochukuliwa.

Ilisema kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajiburufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao ndiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.

Ilisema Wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughway aliwasilisha kadi za wateja wake kwa Jaji Aloyce Mujulizi kuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali, lakini Mahakama hiyo ikasisitiza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na wamiliki wa nyaraka husika.

Ilisema hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake.

Mugway ashangaa
Wakili Alute Mughway aliyekuwa akiwatetea wajibu rufaa katika rufaa hiyo, alisema Mahakama imeacha jukumu lake la kutafsiri sheria na badala yake ikatunga sheria mpya ambayo inapingana na Sheria ya Bunge na Katiba ya nchi, Ibara ya 26 (2).

Alisema Kifungu cha 111 (1) cha Sheria ya Uchaguzi, Hukumu ya kesi ya Mgonja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinampa haki mpiga kura kufungua shauri mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi.

Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, miongoni mwa watu wanaoweza kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi ni aliyepiga kura au aliyekuwa na haki ya kupiga kura na kwamba tangu wakati huo kifungu hicho hakijawahi kufanyiwa marekebisho.

Wakili wa kujitegemea, Vedasto Audax alikaririwa na gazeti dada la The Citizen akisema: “Swali langu ni kwamba ni lini uamuzi wa kesi ya Mgonja ulionekana kuwa na makosa kisheria? Ni kuanzia leo baada ya Mahakama ya Rufani kutamka kuwa una makosa?”

Wakili wa Lema
Kimomogoro alisema hukumu ya kesi ya Mgonja haijitoleshelezi kwa sababu haikusema ni katika mambo gani mpiga kura ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo mahakamani huku akisema kwa maoni yake, anakuwa na haki pale tu haki zake kama mpiga kura zinapokiukwa.

“Mpiga kura hawezi kuwa na haki sawa na mgombea. Mgombea haki zake ni kubwa kuliko mpiga kura kwa sababu kwanza yeye ni mpiga kura na pili ni mgombea,” alisema na kuongeza:

“Ndiyo maana mpiga kura anaruhusiwa kupiga kura katika kituo kile alichojiandikisha tu lakini mgombea huweza kupiga kura katika kituo chochote.”

Alisema mwananchi wa kawaida tu ambaye hajajiandikisha hata kama akimwona mgombea akitoa rushwa hadharani, hana haki ya kufungua kesi mahakamani, lakini alipoulizwa kwa upande wa mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura alisema hakuwa na rejea za sheria kwa kuwa alikuwa Karagwe kwa mapumziko.

Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Buriani.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.

Lema alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kuikubali.

Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.
“Hivyo mpiga kura hana haki ya kisheria kufungua kesi kuhoji matokeo ya uchaguzi pale ambapo haki zake hazikukiukwa,” ilisema Mahakama ya Rufani.

Ilisema kwa mujibu wa Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya Tanzania, raia anakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi kwa masilahi ya jamii, kama ilivyotokea katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa SerikaIi ya mwaka 1995.

Ilisema kesi dhidi ya Lema haikufunguliwa chini ya Ibara ya 26 (2) ambayo inampa fursa na haki raia yeyote kufungua shauri mahakamani lenye masilahi ya umma, huku ikisisitiza kuwa madai ya wajibu rufani katika kesi hiyo hayagusi masilahi ya jamii yote.


"Maamuzi ya COURT of Apeal ndiyo ya mwisho , to that point it can not be apealed from.
the only remedy that i will advise pro. shivji to extend legal advise to those three petitioners to mr. lema is
apply 4 review"
Hukumu ya Lema imefungua ukurasa mpya katika kesi za uchaguzi Tanzania. kwamba sio kila mpiga kura au mtu
yeyote aweza kushtaki kama ilivyokuwa maamuzi katika kesi ya Mgonja, ila sasa kesi ya Lema imeweka limitation
kwamba Mpiga kura [yeyote] aweza kushtaki ila ili ashtaki [as kuanzia hukumu hiyo ilipotolewa?] lazima aonyeshe
yeye kaathirika vipi katika hayo anayoshtaki yaani aonyeshe LOCUS STANDI kwanza, so as from now wanasheria
lazima utakapopeleka shauri la uchaguzi mahakamani lazima (you must establish locus standi ya client wako)
Tatizo ni tafsiri, iacheni mahakama itafsiri sheria, wengi wenu pamoja na Prof Shivji ni mbumbumbu wa suala hilo,
Prof Shivji na huyo mwenzake wa TLS ndio wale wale utawasikia wakitamba mjini kuwa " i studied at the Hill" wakijitapa kuwa wamesoma UDSM. while
they should have sayed ' I studied at the Mountain'. If we really take the meaning of Mountain to mean 'Mlimani' there is quite a big difference between a Hill and A Mountain.A Hill in swahili is mwinuko while Moutain ni Mlima This is to conclude that the issue of interpretation is a big problem.
Tujiulize maswali yafuatayo.
1. Issue ya LOCUS STANDI was it not raised in the High Court at Arusha?
The answer is YES
2. Is Justice Rwakibarilwa so naive not to notice the effect of lack of LOCUS STANDI
NO, he is so learned in law only that he had intended to satisfy those who appointed him.
3. Was his decision embrace the so called "independence of the Judiciery"?
Absolutely, NOT!
4. What about the Decision of the Court of Appeal, does it embrace the same?
The anwers is in affirmative, yES
namalizia kwa kuacha nukuu hii:-
" it is not of merely some importance, but it is of fundamental importance that justice should not only be done
but should manifestly and undoubtedly be seen to have been done" Justice Hewart in R.v Sussex Justices exparte Mc Carthy
 
Hehehe. Mwalimu wangu aliyenifundisha maana na application ya locus standi nae anapinga?

Ngoja nikakague notes za lectures zake wakati anatufindisha hii kitu kama alisema the doctrine of locus standi does not apply to election litigation, let alone mentioning the case of Mgonja.

Mgonja was a good law until the CA said in Lema it wasn't.

It does not matter that Mgonja had been binding for 30 years. Tunazo sheria za muda mrefu mbovu nyingi tuu.

May be before Lema, the CA did not have an opportunity to consider whether Mgonja was a good law.

Bado haijaniingia akilini eti mtu aliyejiandikisha na kupigia kura Chake Chake anakuja kumshtaki diwani aliyeshinda uchaguzi Ngara eti kwa sababu anayo haki ya kufanya hivyo hata kama haki zake hazijawa affected.

Kesi ya Lema itazuia wanasiasa wenye uchu wa madaraka kujificha nyuma ya wapiga kura wa kawaida kufungua kesi halafu wakishindwa wanawakana inapofikia muda ya kulipia gharama za kesi.

EMT.
Mimi sio mtaalamu wa sheria lakini kwa jinsi nilivyofuatilia wataalamu wengi wa sheria wanachopinga ile statement ya "mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi"

Hata mimi naona ulakini katika hapo, mahakama ilipotumia statement kuamua rufanu ile imekuwa kama wametunga sheria mpya.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Uliianza vizuri
Wengine hatukushiriki sana kwenye huo mjadala lakini everytime I come across such blanket statement kama hii yako, I lose interest. Jaribu kuwapa breathing space watu usiokubaliana nao...mara wapenzi wa Chadema, mara wapenzi wa Dr. Slaa na sasa imeongezeka wapenzi wa Lema, duh, eti hawana uelewa wa nini kinachoongelewa. Kiranga nakuheshimu na nisingependa tujiingize kwenye nani zaidi bali tubakie kwenye kupingana kwa hoja...ni hayo tu, sasa tuendeleee. How I wish some of us had more time to participate kwenye mijadala mbalimbali but then...
nikasema leo Kiranga kapewa za mbavu

Sisi tuliobahatika kupata exposure kwa wenzetu ambako demokrasia imekomaa,
Hee kumbe upo exposed...

no voter would dream of going to court to challenge an election result based on mgombea anayemtaka kushindwa uchaguzi kwa sababu alikashifiwa kwenye kampeni huku mhusika hayuko tayari hata kuwa shahidi mahakamani...it is stupid, ridiculous and makes no sense. Nina hakika hata mahakama ililiona hili kwamba ku"entertain" kitu kama hicho ni kuidhalilisha mahakama. Naamini hukumu iliyotolewa ilizingatia hilo.
Mbona unawaibisha wenzako wakomavu wakisiasa na uchambuzi kama huu...
 
(Kutoka gazeti la mwananchi)


Katika shauri hilo namba 84 la mwaka 1980 lililofunguliwa na William Bakari na mwenzake dhidi ya Mgonja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mahakama Kuu Tanzania iliamua kuwa, mpiga kura ana haki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Walalamikaji walishinda.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani katika kesi ya Lema, iliamua kwamba hukumu katika kesi ya Mgonja ilikosewa kwani si sahihi kwamba mtu yeyote bila kujali mahali alipojiandikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo katika jimbo lolote nchini hata kama haki zake hazijakiukwa kwa namna yoyote.

Lakini
Profesa Shivji aliitetea hukumu hiyo ya Mgonja akisema imekuwapo kwa zaidi ya miaka 30 sasa na kwamba kwa muda wote huo imekuwa ikifuatwa katika uamuzi wa mashauri mbalimbali, huku akisisitiza kuwa Mahakama haiwezi kuifuta kirahisi tu.

.

Hukumu ya Mgonja inaonekana kuwa ndio basis ya argument ya Prof Shivji. Je, hukumu hiyo ilikuwa sahihi? Na kama hakikuwa sahihi (kama walivyosema majaji kwenye kesi ya Lema) iendelee kutumika kwa sababu tu imekuwepo kwa miaka mingi sasa?

Pili, bado sijaelewa ni kwa vipi 'matusi' ya Lema yamewathiri wapiga kura/waleta mashitaka? Na maadam kesi hii inahusu uchaguzi wa mbunge wa Arusha Mjini, je, matokeo ya uchaguzi yangekuwa tofauti kama Lema hakusema hayo matusi?
 
yap inawezekana kabisa. nakupa mfano mwingine kama ulivyosema unatoka jimbo la segerea ukafika kibakwe ukashuhudia live mgombea wa huko anatoa rushwa waziwazi, utanyamaza kisa si mgombea wa jimbo lako?. Kwa kifupi wanyonge hatuna haki tena. bora hata SHIVJI na wenzake wameliona hili na wajanja sasa hatupigi kura ng'o kwa sababu hata kama ukidhulumiwa huna pa kulalamika.
Kama ni hivyo kwanini sheria itamke mpiga kura na si mwananchi yeyote? Je, mpiga kura ni yule tu aliyejindikisha kupiga kura? Kama raia amejiandikisha kupiga kura halafu hakupiga kura, kwa sababu nyingine zaidi ya safari za kikazi, ugonjwa au kuzuiliwa na taratibu za upigaji kura anakuwa na sifa za mpiga kura (mfano sikutaka tu kupiga kura)? Kwanini sheria ininyime haki ya kupiga kura popote na wakati huohuo inipe haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi popote?
 
Yaani hapo wewe hujaelewa nini? ni wazi kuwa hukumu imemnyima haki mpiga kura. Hilo lingezingatiwa kwanza ni wazi matusi yale yalikuwa na effect kubwa tu katika mwenendo mzima wa uchaguzi na ndiyo maana tume ya uchaguzi katika sheria zake jambo mojawapo inalolisisitiza ni kufanya kampeni za kistaarabu kwa sababu wanajua madhara ya kampeni zisizo za kistaarabu.

Wafungua kesi walishindwa kuthibitisha waliathirika vipi na madai ya matusi, pia mtukanwa hakuthibitisha kama alitukanwa kweli na hayo matusi yalimuathiri vipi katika uchaguzi! Hizi argument ndo zilipelekea mahakama ya rufaa kutoa uamuzi iliyotoa!
 
Mambo yameanza!!! but hata wakate tena rufaa but Lema is a winner!!! Kweli anaogopwa sana huyu mheshimiwa!! Hamtaki wanaarusha wawe na mwakilishi?
 
Kama ni hivyo kwanini sheria itamke mpiga kura na si mwananchi yeyote? Je, mpiga kura ni yule tu aliyejindikisha kupiga kura? Kama raia amejiandikisha kupiga kura halafu hakupiga kura, kwa sababu nyingine zaidi ya safari za kikazi, ugonjwa au kuzuiliwa na taratibu za upigaji kura anakuwa na sifa za mpiga kura (mfano sikutaka tu kupiga kura)? Kwanini sheria ininyime haki ya kupiga kura popote na wakati huohuo inipe haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi popote?

...kweli mkuu,maswali yako ni yamsingi sana...
 
hii inaonyesha ni jinsi gani hili linchi lina hali ngumu....semen msemavyo...cha msingi mweshimiwa lema yupo jimboni!!!
 
Japo mimi sio gwiji katika sheria kama Prof Shifji nadhani hayuko sahihi. Sheria inayoweza kutumiwa vibaya imepata tafsiri nzuri ili kukomesha matumizi yake vibaya. Sikubaliani kama mahakama ya rufani imetunga sheria mpya, ila imetafsiri sheria iliopo kwa namna chanya kuelekea kupata haki.
 
Hii thread ni muhimu sana kwa kujifunza.

Sisi ambao hatujui sheria nashauri tukae pembeni na kuwaacha wenye ujuzi watuelemishe.

Hili suala halina siasa ndani yake wala halina uhusiano na Lema kurudishiwa ubunge au kutokurudishiwa. Hii ni tafsiri kubwa zaidi ya siasa za CCM na CHADEMA.

Tusiivuruge kwa mapenzi ya vyama vya siasa na badala yake tuwaachie wanaojua kuliko sisi watuelemishe.
 
hii nchi hii inashangaza hii nani alisema hii nchi ina sheria,toka mwanzo kesi ilianza kinafiki na bahati nzuri imeisha kinafiki shame tanzania unaangamia kwa upumbavu wako.
 
Back
Top Bottom