Salaam,
Kwa wenye access na ITV, Watch ITV now, Prof. Issa Shivji, anashusha mhadhara kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya.
Kwa wale ambao mtakikosa kipindi hiki, angalieni TBC-1 saa 1:30 usiku huu.
Please Watch.
Pasco.
NB. Vipindi hivi vitakujia kila siku saa 1:30 TBC-1 na ITV siku za Alhamisi na Ijumaa saa 1: 00 usiku.
UP DATE
Sehemu ya pili ya mada ya Prof. Shiji na Mchakato wa Katiba Mpya kinaendelea ITV saa hizi na kitakuwepo TBC-1 saa 1:30. Leo Prof. Shivji anajibu maswali ya washiriki.
Karibuni tuendelee.
Shivji anasema msingi mkuu wa katiba ni "dira", huwezi kuingia kwenye mchakato wa katiba mpya bila dira. Mchakato wa kukusanya maoni ulitakiwa utanguliwe na "mjadala wa kitaifa kuweke dira", ndipo sasa tutengeneza katiba inayoendana na hiyo dira!.
Amesema, pamoja na mchakato kuanza bila dira rasmi, lakini wajumbe wa kamati hiyo wana mitazamo, hivyo japo hatuna dira, lakini pia tunaweza kupata katiba nzuri!
Ameitaja misingi mikuu minne ya katiba nzuri, ikianzia na uhuru, haki, usawa, udugu na ujamaa.
Uhuru: Huu ni uhuru wa mtu binafsi, lengo zima la uhuru limejengwa kwenye misingi ya haki za binaadamu, maada ya dhana ya uhuru, pia ni uhuru wa nchi, uhuru wa taifa, uhuru wa jamii!. Kama nchi haiko huru, then watu wake hawawezi kuwa huru!. Japo taifa limepata uhuru wa nchi, yaa independence, lakini taifa hilo likawa halijajikomboa "libarated", huwezi kujidai eti una uhuru!. Zaidi ya nchi kupata uhuru, ili mchi iwe na uhuru wa kweli lazima wawe libarated!. Huwezi kudai uko huru huku unanyonywa na mapepari.
Nchi zinataka uhuru
Mataifa yanataka ukombozi
Watu wanataka mapinduzi!.
Amnezungumzia haki, nimemkosa, sasa anazungumzia usawa "equality before law", watu wote ni sawa, tajiri, masikini, mwanamke mwanaume, mkubwa mdogo, walala heri na walala hoi wote wako sawa mbele ya sheria.
Anatoa hadithi ya kesi ya Martha Wejja, uswa huo unategemea, dira ndio ilitakiwa iamue kuhusu hii misingi
Katiba bora ni ile katiba ambayo chimbuko lake litatoka chini kwa wananchi kwenda juu kwa watawala, katiba hii tuyaitengeneza sasa, misingi imetoka juu kwa watawala na kuletwa chini kwa wananchi!.
Amesisitiza dira inatengezwa kwa mjadala wa kitaifa, ili dira hiyo iwe imetokana na wananchi. Kabla ya kuandaa katiba kwanza ni lazima watu waulizwe wanataka kujenga taifa la namna gani, baada ya kujua tunataka nini, ndipo tunaunda tume, kuandaa katiba ya kuitekeza hiyo dira!.
Amesema amemuuliza M/Kiti wa Tume, hayo maoni tunayoyakusanya, ni maoni ya kutengeneza katiba ya kutekeleza nini?, Warioba hana jibu, hivyo tunatengeneza katiba mpya kwa kufuata dira na misingi ya katiba ya zamani kwa sababu Tanzania kama taifa, hatujawahi kukaa chini na kujitafakari, tunataka nini?.
No wonder kuna kiongozi aliulizwa "chanzo cha umasikini wa Tanzania ni nini", akasema "hajui kwa nini Tanzania ni masikini!.
Katiba yetu bado inasema Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi inayofuata misingi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea, huku in reality, Tanzania ya leo sio ya wakulima na wafanyakazi na tunafuata misingi ya upapari na soko huria!.
UP DATE
Sehemu ya pili ya mada ya Prof. Shiji na Mchakato wa Katiba Mpya kinaendelea ITV saa hizi na kitakuwepo TBC-1 saa 1:30. Leo Prof. Shivji anajibu maswali ya washiriki.
Karibuni tuendelee.
Prof. Shivji ameanza na ukosoaji wa Tume ya Katiba, akasema Tume za katiba ziko supposed to be a "professional body" hazikuhitaji uwakilishi, kwenye kukusanya maoni, uwakilishi wa nini?. Amesema, uwakilishi, anahitajika kwenye Bunge la Katiba. Pia ameuliza kwa nchi masikini kama Tanzania, wajumbe 30 wa tume ya kukusanya maoni, "wote hao wa nini?.
Prof. Shivji pia amekosoa bunge la katiba litakaloitishwa, amesema sheria iliyopo inawataja wabunge wote bunge la JMT, na wajumbe wote wa BLW automatically wanakuwa ni wajumbe wa bunge la katiba, akasema "wabunge hawa ni wawakilishi wa wananchi kwa mujibu wa katiba iliyopo, sasa nani kawatuma wajumbe hawa kuwa wawakilishi wa wananchi katika bunge la katiba?. Waunge wote na wawakilishi wote wamechaguliwa kutoka vyama vya siasa. Jee Watanzania wasio wanachama wa chama chochote cha siasa, watawakilishwa na nani?,
Prof. Shivji amesema Bunge la Katiba ni bunge maalum kwa kazi maalum!, Wabunge wa bunge la sasa, hawakupaswa kuwa wajumbe wa bunge la katiba automatically.
Kwa msiojua Katika uundaji wa katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, wabunge wa bunge la Tanzania ndio walijitransform na kujigeuza wajumbe wa Constituent assembly, na bunge likajiuza bunge la katiba, likaipitisha katiba ile within 45 minutes!.
Akatoa angalizo, ukujumlisha wabunge wote na wajumbe wote wa BLW katika ujumla wao, wabunge wa chama kimoja peke yao, wanafikia theluthi mbili za kupitisha katiba mpya!.
Prof. Shivji amesema this is a good chance kwa Watanzania kupata katiba bora, ila tusiharakishe, bora tuchelewe lakini tupate katiba yenye uhalali wa kikatiba na uhalali wa kisheria.
We not only need a good constitution, but a constitution which has the constitutionality of a good constitution!-Prof. Shivji.
Pasco