Prof. Shivji aukosoa Mchakato wa Katiba Mpya, aliponda Bunge la Katiba

Mie naona katika hili Shivji hayuko objective,kwanza anaonyesha kuwa ana hofu ya serikali 3, lakini pia anajikanganya anaposema muungano usiangaliwe kwa kigezo cha idadi ya serikali papo hapo anasema alipoombwa kutoa ushauri kwenye Baraza la Wawakilishi alipendekeza muundo wa serikali 2.

Hoja yangu hapo ni kwamba kama muungano hautakiwi kujadiliwa kwa idadi ya serikali mbona na yeye aliuingia mtego huo huo ?
 
Ndio sababu hawakumuweka kwenye tume ya katiba maana angemkosoa live hata Warioba na ToR alizopewa azishikilie!!kile kichwa ni balaa!!!
Mkuu Lambardi, nilitumai, jina la Prof. Shivji baada ya kukosekana kwenye tume, lingeibukia kwenye bunge la katiba!.
Pasco
 
hivi inawezekana baada ya kuuponda mchakato ndio maana amekosekana?
 
nakubaliana na "Shivji"tulikosea tangu mwanzo,kuna mambo makuu mawili tulitakiwa kuanza nayo, na kupata muafaka wa kitaifa kabla ya kuipa kazi tume ya kukusanya maoni,

1. tulitakiwa kwanza tuwe na referendum juu ya muundo wa muungano.

wananchi wangeulizwa wanataka muundo upi wachague watakaoshinda ndo katiba iandikwe kufuata matakwa ya wananchi

2.tuwe tukubaliane kwenye dira, itakayo tuongoza kutafsri siasa, uchumi

hapa tulitakiwa tuwe makini, kwa sababu nyakati tulizomo zimebadilka sana, na si rahisi kupata majibu ya moja kwa moja kutoka kwa wananchi juu ya mfumo gani unafaa kuendesha uchumi na siasa zetu, hivyo basi baada ya tume ya warioba kukusanya maoni ya wananchi nchi nzima walitakiwa waje na mapendekezo ya "dira"

kwa kifupi, ni hivi kwanza tungepiga kura ya maoni, kuchagua muundo wa muungano, na dira ya taifa
baadaye ndo tungelianza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ni kipi kiingizwe kwenye katiba ya Muundo "A" na dira "B"

au tungelianza na muundo wa muungano, tukafuatiwa na maoni ya wannchi baadaye tukakubaliana juu dira kazi ya kuandika katba mpya ingekuwa rahisi mno.
 
Too Late Prof. Shivji you can not change anything now. Watu wako busy na safari ya Dodoma. huyu hakuwa na kigezo cha kushirikishwa kwenye bunge hili? naona angeweza kuleta tofauti.
 
Too Late Prof. Shivji you can not change anything now. Watu wako busy na safari ya Dodoma. huyu hakuwa na kigezo cha kushirikishwa kwenye bunge hili? naona angeweza kuleta tofauti.
Tunaweza kumwingiza kupitia kundi lenye malengo yanayofanana : Wachawi, Wanga, Waganga wa Kienyeji labda.
 
Tunaomba afungue website na awe na youtube channel yake

huyu mtu ni hazina sana nchi hii
 
Kwa level ya huyu profesa hakustahili kabisa kuujadili muungano bila ya kupata walau kopi ya hati ya mkataba wa muungano.

Kwangu mimi profesa Shivji alitakiwa kuiheshimu taaluma yake.
 
Kufuatia Prof. Shivji kuzungumza tena leo akibonda, kuponda na kuisagasaga tume ya Warioba, nimeona afadhali niwakumbushe tuu kuwa Shivji kubonda na kuponda hakuanza leo!,

Hebu msomeni humu na kumlinganisha na alichosema leo!.

Pasco
 

daa huyu professor shivji ni kiboko
 
Wanabodi, msikilize Askofu Gwajima Bungeni Jana
Hicho alichokisema kuhusu Dira, ndicho alichokisema Prof. Shivji hapa,

Hivyo japo kwenye baadhi ya issues Askofu Gwajima anaonekana kama kiazi fulani, Lakini kwenye hoja hii,he is very right.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…