Namsikiliza Prof. Shivji kupitia ITV. Shortly anasema Wamasai walihamishiwa Ngorongoro kutokea Serengeti Mwaka 1958 na kuahidiwa kutohamishwa. Anasema tusiwe na haraka ya kuwatoa Wamasai. Muhimu kuangalia haya.
1. Je Kuna wasio Wamasai wangapi waliojaa ndani ya Ngorongoro.
2. Tujadili nao mustakabali wao.
Kwa ufupi amepinga jambo hili la kuwahamisha wamasai
Watanzania wengi hawajui wachokiongea na sishangai waongeaji wengi ni wenyeji wa pwani ambao hawajui hali halisi ya ngorongoro sisi tuliokaa Arusha ndiyo tunajua
1. Tatizo sio watu bali ni mifugo hivyo huyu Professor anaongelea watu kama vile ndiyo tatizo la hasha tatizo kubwa ndugu zangu ni hao ng'ombe ambao ni karibu 1M kutangatanga mbungani
2. Wamassai ni waharibifu wa mazingira. Watanzania tujiulize imekuwaje Wamassai wanasomba ng'ombe kutokea Mondoli mpaka Lindi! wamejaa bagamoyo, morogoro na Tanga na migogoro mingi ni ya kwao. Monduli nendeni mkaone jangwa lililo letwa na wafugaji hawa!.
3. Wamassai wamekuwa kama wafanyakazi wa watu wamassai wenye pesa na wafanyabiashara wanawapa ng'ombe wao wawafugie na wengine wanatoka mpaka Kenya na wengine ni viongozi serikalini
4. Mabadiliko ya mazingira yanayoendelea Dunia tatizo la malisho ya mifugo litaendelea hivyo ni bora watolewe sasa na sio baadae
5. Umefika muda wa kuwa na mifugo ya kisasa hivyo sio tu wanatolewa lakini wanaenda kuelekezwa ufugaji wa kibiashara na sio kufuga ili kuongeza wake pekee. Utamaduni huu wa sasa hauna tija kwa nchi. Watoto ni lazima wasome sio kushinda kucha kuchunga ng'ombe ambao nusu wanakaa mpaka wanakufa bila faida yoyote. Ngombe wa kimassai ni bei rahisi kuliko mbuzi wa South Afrika kwasababu wamekondo balaa.
Mimi binafsi na rafiki zangu tuna heka 62 kidomole pale Bagamoyo kila siku ni kugombana na hawa wamassai. Hawana faida yeyote wanaoleta kwa jamii zaidi ya ugomvi, uharibifu wa mazingira na kuendeleza ulimbukeni. Hatuwezi kutunza kabila kama vile nao ni utalii kama wanyama hii sio sawa. Hawa wana haki kama watanzania wengine na tuache tabia ya kuwadekeza badala yake tuwaulize. Kwanini watoto hawaendi shule, tutawapaje hospitali za kisasa katikati ya mbuga? je wakianza kuliwa na wanyama pori tuanze kuuwa wanyama mbugani? au tutume polisi akazuie tembo mbugani!. Wamassai watolewe na kama Professor yupo serious akakae nao kule mwezi mmoja tuone kama atapona
Hata USA kuna mbuga ambazo watu hawaruhusiwi kujenga.