Prof. Shivji: Wamasai wasiondolewe Ngorongoro


1. Wamaasai walihamishwa na WAKOLONI toka Serengeti wakapelekwa Ngorongoro ili kutoa nafasi ya kuanzisha mbuga ya Serengeti.

2. Sasa hivi kuna migogoro miwili inayoendelea.

..Mgogoro wa kwanza upo Ngorongoro. Wananchi wake wanahamishwa kwenda Handeni.

..Mgogoro wa pili upo Loliondo. Wananchi wanakuwa squeezed out of Loliondo area bila fidia yoyote.

3. Matatizo hayo yasingekuwepo kama SERIKALI ingekuwa na program ya muda mrefu ya kupunguza idadi ya watu na mifugo Ngorongoro.

4. Program ya kupunguza mifugo Ngorongoro inatakiwa ihusishe mafunzo, na incentives, kuwezesha Wamaasai kufuga wanyama wachache wenye tija, na kuachana na uchungaji wa makundi makubwa ya mifugo.

5. SERIKALI inastahili lawama zaidi kuliko Wamaasai. Serikali ilikuwa wapi miaka yote huku idadi ya watu na mifugo ikiendelea huko Ngorongoro?

6. Je, kuna umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa KAMPUNI YA UWINDAJI maeneo ya Loliondo? Je, uwepo wa kampuni hiyo unachochea migogoro Loliondo?

7. Je, mazingira ya Ngorongoro yanaharibiwa na kutishiwa na Wamaasai peke yao? Je, MAHOTELI na miundo mbinu ya kudumu huko Ngorongoro hayaharibu mazingira?

8. Je, tumejiridhisha kwamba mahoteli yote huko Ngorongoro na ktk mbuga zetu za wanyama yako nje ya maeneo ya mapito na mazalia ya wanyama?

9. Je, idadi ya Watalii na misafara ya magari inayoingia Ngorongoro ni salama kwa uhai wa Ngorongoro 5 or 10 yrs down the road?

Cc Phillipo Bukililo, Ngongo
 
Mkuu Joka kuu nadhani cha muhimu ni somo kuwaingia wamasai mpaka ugomvi wao wa kuua mtu kwa mkuki linabakia historia.

Ni kweli serikali inastahili lawama kwa kulipiga danadana hili tatizo na miaka ikawa inakwenda pasipo kupatiwa suluhisho.

Hao hao wenye kustahili lawama kwa kutowapa mafunzo wakazi wa eneo husika ndio wamewajengea nyumba kule Handeni na masuala yote muhimu ya kibinadamu yameweza kujengwa, pamoja na kuwapa fidia.

SSH anajitahidi sana kutofanya maamuzi yanayoweza kuwakera raia anaowaongoza, hatumii nguvu wala kujionyesha kwamba anayo mamlaka ya urais, anatumia zaidi a human face.
 


Ni kweli lakini Raisi huyu ni mtekelezaji hawazi kulaumu kwamba program za muda mrefu zingekuwepo yeye kama Raisi anatakiwa kutatua tatizo lililopo sasa huo ndiyo uongozi. Hivyo ninkweli program ingekuwepo lakini sasa tuko hapa tulipo na hatuwezi kuna cha kwasababu hiyo maamuzi magumu ndiyo uongozi.

Pili hata loliondo wamassai watolewe kwenye vyanzo vya maji. Nenda Monduli ukaangalie ilivyobaki janjwa
 

..Vipi kuhusu ujenzi wa mahoteli kwenye maeneo ambayo ni njia na mazalia ya wanyawa, je uendelee?

..Je, idadi ya watalii wanaoingia Ngorongoro na misafara yao ya magari ni sustainable kwa uhifadhi wa Ngorongoro?

..Je, kampuni ya uwindaji ya Loliondo iendelee kupewa eneo kubwa kuliko jamii yenye asili na eneo hilo? Je, kampuni hiyo iendelee kuwepo Loliondo?

Cc Phillipo Bukililo , Ngongo
 
Misafara ya Ngorongoro ni seasonal. Miezi yenye wageni wengi haizidi minne kati ya kumi na mbili ya mwaka mmoja.

Hapo kuna miezi nane ya ku-recover.
 
Mtu utaachaje kukerwa hata kama unazawaidiwa kama unavyosema wewe vitu vizuri kama hukupewa taarifa (elimu) ya kutosha juu yanayokutokea.
Hayo mazuri unayoona unapewa, nyuma yake unaambiwa ukighairi utakiona cha mtema kuni, vitisho chungu nzima vikiambatana na "kupewa zawadi"!

People can quite easily see through that deception of a "human face" charade.

It all boils down to leadership with a deficit in being trustworthy.
 
Hasira za kukosa uteuzi. Kule Zanzibar kuna waliokosa ulaji nao wanampinga Mwinyi asilete wawekezaji.

Yajayo YANAHUZUNISHA!.
Huyu prof njaa mm nilimdharau tangu kipindi cha bunge la katiba. Alipo amua kuyakanyaga machapisho yake yote yanayohusu kupinga muundo wa muungano wa serikali 2.
 
Kati ya ekari 4,000 za Loliondo Game Controlled Area iliyopo kisheria tokea 1968 na mwarabu akakodishiwa mwaka 1992 ekari 2500 sasa zitakuwa mkononi mwa wananchi sio wamasai maana kuna makabila mengine pia na sasa eneo la Loliondo GCA limebaki ekari 1500. Sasa hapa kaongezewa nani na nani kapunguziwa eneo?. Na nani analo eneo kubwa?.

Tukumbuke kuwa wamasai sio wenye asili ya eneo hilo. Wao walitokea up north na kuhamia hilo eneo upande wa Tanzania na Kenya. Walikuta makabila mengine ambayo yalihamia maeneo ya Lake Eyasi kukwepa ubabe na ubinafsi wao. Ni makabila ya Wahadzabe, Datoga na jamii kama hizo.
 
Mkuu amesema sababu za kiikolojia?kwamba uwepo wao unatishia mbuga yetu?
Na pia,kulko kukataa kuwatoa hao wamasai kisa wengine wapo hawatolewi,kwanini asitoe rai kwamba wote watolewe kwa pamoja na si kugoma tuu?
Anauhuru wakutoa maoni ila kwa hili nampinga.
 
Kwani wanatolewa wamasai au watu wote wanaoishi kwenye hifadhi?

Mambo ya mwaka 1958 ndo yatuzuie kufanya kitu positive leo. Hata huko Handeni wanapopelekwa mwaka 2070 pakaonekana pana madini watatolewa tu.
Kumbe lengo sio uhifadhi ?,nimeelewa kupitia reply yako ya kwamba wapishe mzungu achimbe madini,sasa wanazunguka mbuyu wanini hii serikali yako?
 
Swali lake la mtego, "Je kuna wangapi wasii wamasai kuke ngorongoro" .

Wapo wengi tu profesa na wakiondolewa wamasai watajaa wengine na wengine wasio wamasai
Tuko pamoja sana
 
Viongozi hawana maono, hakuna sera elekezi ya matumizi ya ardhi, na kama ipo imefungiwa makabatini. Majengo madogo ya serikali hayajengwi tu kwenye miradi mipya, hata ya zamani. Nilitembelea nhif Tabora, ofisi zao zipo haspitali ya mkoa. Upanuzi unaendelea hospitali hiyo, lakini yote ni majengo madogo, si ghorofa, japo hospitali haina eneo kubwa.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…