Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. SOSPTER MUHONGO AGAWA CHAKULA CHA DHARURA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO
Leo, Jumanne, 4.4.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo ametembelea Kijiji cha Kusenyi, Kata ya Suguti kwa malengo yafuatayo:
1. Kutoa pole kwa waathirika wa mafuriko ya juzi na jana
2. Kushuhudia uharibifu uliotokana na mafuriko hayo
3. Kugawa chakula cha dharura
Chakula alichogawa Mbunge huyo:
1. Magunia 25 ya Mahindi, kila gunia lenye Kilo 108
2. Maharage Kilo 100
Vitongoji vilivyoathirika sana
1. Kitongoji cha Nyabweke, Kaya 26 zimeathirika sana
2. Kitongoji cha Kwikuyu, Kaya 24 zimeathirika sana
Tathmini inaendelea kufanywa:
Wakati taathimini ya uharibifu uliotokana na mafuriko hayo ikiendelea kufanywa, Mbunge huyo amebaini yafuatayo:
1. Baadhi ya nyumba zimebomoka na kuanguka
2. Baadhi ya nyumba zimepasuka hazifai kutumika
3. Baadhi ya Kaya, Chakula chao kilichotunzwa majumbani kimeharibika na kingine kimesombwa na maji
4. Kuku na Bata wamesombwa na Maji
5. Tope ni nyingi sehemu za makazi ya watu
Tunategemewa kupata tathmini kamili ndani ya wiki hii.
Kilichosababisha maafa haya:
Wananchi, kwa uzoefu wao, wamebaini sababu kuu mbili:
1. Ujenzi wa barabara ya lami ya km 5, haukuzingatia uwekaji wa njia za kutosha kupitisha maji kwenda ziwani (Ziwa Victoria)
2. Wakulima wa Mpunga, n.k. walioko sehemu ya juu ya Kijiji cha Kusenyi wameweka miundombinu yao ya kilimo inayozuia maji kutitirika kwenye mikondo inayoelekea ziwani.
OMBI KUTOKA KIJIJINI KUSENYI
Waathirika wa mafuriko ya Kijijini Kusenyi wanaomba tuwasaidie:
1. Chakula
2. Vifaa vya ujenzi (tathmini itaainisha idadi)
3. Ujenzi wa miundombinu mikubwa ya kutiririsha maji ziwani.
Michango ipelekewe kwa: DC Wilaya ya Musoma; +255 756 088 624
Picha za hapa zinaonesha matukio mbalimbali ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mhe. Prof Sospeter Muhongo akiwa na:
1. Waathirika wa mafuriko Kijijini Kusenyi, Kata ya Suguti
2. Viongozi 3 kutoka Kijijini Kusenyi wakipokea magunia 25 ya mahindi (Kilo 108), na gunia 1 la maharage la kilo 100.
TAFADHALI SANA TUJITOKEZE KUWASAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO YA KIJIJINI KUSENYI
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumanne, 4.4.2023