Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,303
- 12,679
View: https://youtu.be/gm6k0gc9PW4?si=StdiqWV7Dj1gTll5
===================
Naomba uongozi wa Jamiiforums Active mmfanyie mahojiano ya kina Prof Tibaijuka
Pia mngemfanyia Mahojioano Mhandisi mzoefu wa Ujenzi wa Maghorofa marefu.
Pia mngemfanyia Mahojioano Mtaalam wa Mipango miji
===================
Kwa muda mrefu watu tumelalamika kwamba Maghorofa ya Kariakoo sio salama. Pia kariakoo imejaa inabidi pawe na kariakoo ndogondogo kama 7 nje ya jiji la Dar es salaaam. Au Mkoa mwingine, ili kupunguza msongamano na majanga. Muda mrefu sana mrangi Salary Slip amekuwa akizungumzia hilo suala la maghorofa kuota kama uyoga Kariakoo, kuwa ni hatari mno.
NB: Kariakoo sio salama. Majengo sio salama. Maghorofa yamekaribiana mno, maghorofa mengi sana yamejengwa kinyume na sheria za mipango miji. Pia yapo kinyume na utaalam wa kihandisi, ma engineer wanaita "structural analysis".
Kwa mujibu wa sheria za mipango miji.
Urban Planning (Planning Space Standards) Government notice No.93 published on 9/3/2018, Ukurasa wa 4 kwenye
(b) Specific Standards for mixed use- Low Rise, High Rise and Skyscrapers
Kiwanja cha ghorofa(kisheria) kitaalam kinapaswa kiwe na ukubwa ufuatao
1. Kuanzia angalau kwa jengo la ghorofa 1-5 ukubwa ni 2000sqm-4000sqm. Nafasi kati ya ghorofa moja hadi jingine inapaswa iwe 10m-25m+
Vipimo vya urefu na upana wa kiwanja
2000sqm= 50mx40m
4000sqm= 50mx80m/63mx63m
2. Ukubwa wa kiwanja cha ghorofa 6-10 ukubwa wa kiwanja ni 4001sqm-8000sqm. Nafasi kati ya ghorofa moja hadi jingine inapaswa iwe 15m-25m+
Vipimo vya urefu na upana wa kiwanja
8000sqm= 160mx50m/89mx90m
3. Ukubwa wa kiwanja cha ghorofa 11-20 ukubwa wa kiwanja ni 8001sqm-20,000sqm. Nafasi kati ya ghorofa moja hadi jingine inapaswa iwe 15m-25m+
Vipimo vya urefu na upana wa kiwanja
20000sqm= 100mx200m/141mx141m
Pia hayo maghorofa yanatakiwa yawe na nafasi ya parking ya magari. Pawe na barabara za njia nne kila upande wa mtaa. Kwa ajili ya usafiri na kwa ajili ya dharura.
Kariakoo sio salama, maghorofa yamebanana kama maharage kwenye gunia.
Serikali ipange kariakoo nyingine kama 7. Viwanja wapime vya ukubwa kulingana na sheria na utaalam
1. Ghorofa 1-5, ukubwa wa kiwanja kuanzia 2000sqm-4000sqm
2. Ghorofa 6-10, ukubwa wa kiwanja kuanzia 4001sqm-8000sqm
3. Ghorofa 11-20, ukubwa wa kiwanja kuanzia 8001sqm-20,000sqm
4. Upana wa barabara uwe barabara za njia nne (30m-60m+)hadi barabara za njia nane hadi kumi na mbili.
Kwa dharura yafuatayo yangefanyika
1. Ukaguzi wa majengo yote
2. Zoezi ya ujenzi wa maghorofa mapya ungesimama. Mpaka ukaguzi wa kina ufanyike
3. Mazoezi ya kuboresha maghorofa ya zamani yangesitishwa. Mpaka ukaguzi wa kitaalam ufanyike
4. Mazoezi ya kuweka godown kwenye maghorofa yasitishwe.
5. Mazoezi ya kuweka underground/basement kwe maghorofa ya zamani yasitishwe
Poleni sana kwa wahanga wote. Kalaga Baho Nongwa
Yoda reyzzap mdukuzi Bams Stuxnet Erythrocyte Mshana Jr
Akilindogosana