Prof Tibaijuka alia ujenzi kiholela umegharimu maisha ya watu kariakoo

Prof Tibaijuka alia ujenzi kiholela umegharimu maisha ya watu kariakoo

Ujenzi holela na bado hakuna ukaguzi, ile migunia yote ukiona inaweza support ‘load rate’ ya floor kweli.

Inabidi waanze kukagua magorofa yote kuona watu wanaifadhi stock za namna gani humo ndani na kama jengo linaweza imili.

Kila kitu mzaha Tanzania
 
Nyerere na wenzake akiwa Rais walitunga sheria ya kuthibiti uhujumu wa uchumi, rungu akapewa Waziri mkuu wa wakati ule Sokoine...katika kamata kamata ya wahujumu uchumi akanaswa mwana CCM mwenye heshima kubwa chamani, Sokoine akamn'gangania, akawekwa ndani, Nyerere akapewa taarifa....kufupisha stori ilibidi sheria Ile irudishwe tena bungeni ili iwe na "upenyo" wa kumnusuru Kada wao!

Hii habari aliisimulia Warioba majuzi wakati wanazindua kitabu cha hayati Sokoine.....

Kuna cha kujifunza hapo....hizo sheria za majengo na takataka nyingine ni kwa ajili ya mimi na wewe makapuku...ghorofa zilizojengwa kihorera kama ni za Wana CCM, au wafadhili wao hizo "hazina makosa"
Ujinga huu upo toka zamani labda CCM ife ndipo akili zitakaa Sawa!
 
Back
Top Bottom