Prof. Tibaijuka: Deni la Taifa sioni kama 'Himilivu', kiwango cha chini cha IMF ni 18% sisi tuko 31%

Prof. Tibaijuka: Deni la Taifa sioni kama 'Himilivu', kiwango cha chini cha IMF ni 18% sisi tuko 31%

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwanasiasa mkongwe Anna Tibaijuka, akizungumza kupitia The Chanzo, amesema deni la taifa linaonyesha dalili za kutokuwa himilivu kulingana na takwimu za bajeti ya hivi karibuni, akisisitiza kuwa maoni yake yanatokana na uchambuzi wa kitaalamu na si msimamo wa kisiasa.

1782046206706.png

Prof. Tibaijuka amesema amekuwa akiandika kuhusu masuala mbalimbali ili kuongeza uelewa wa umma, na hivi karibuni alihoji kupitia akaunti yake ya X kuhusu hali ya deni hilo.

Soma: Professa Tibaijuka ashtushwa na kasi ya ukuaji wa deni la taifa

"Watu wanashangaa, kwa sababu tumeambiwa kwamba deni ni himilivu. Sasa wewe kama sio mchochezi mbona unasema sio himilivu? Elimu yangu ninajua kwamba uhimilivu wa deni kwa nchi kama zetu ni asilimia ya fedha itakayokwenda kulipa madeni.

Sasa hivi tuko kwenye asilimia 40 au wanasema 31, lakini inalala pale. Kiwango cha chini sio cha kwangu, cha IMF—threshold ya IMF ni 18%. Yaani uhimilivu wa nchi hizi za kwetu... Japani, na katika makala zangu nimeandika andika mchezo huo nina nafasi ya kuweza kuzipitia, kwamba Japani deni lake ni asilimia 270 ya pato la taifa, liko kubwa sana, lakini hawasikii. Kwa sababu uwezo wake wa kulipa ni mkubwa."


Soma pia:
 
Wanakopa Fedha kila kona Kwenda.

1. Kununua Magari ya Kifahari, Milioni 500,
Ma Toyota V8 kila wilaya yapo 5.
2. Kununua Furniture za Maofisini Kutoka Nje.
3. Makampuni ya Hewa ya kufufua Umeme.
4. Kujenga Mahekalu Ulaya.
5. Kufungua Account Za Kigeni Ulaya.
6.Ufisadi.
7. Rushwa.
8. Kununua Magari na Upumbavu wa Polisi.
9. Kufanyia ziara za ******* Nje ya nchi.
10.

"Hii nchi ipo siku itapigwa mnada"
JOB NDUGAI.
 
Ufisadi uliowahi kufanyika na baadhi yenu huko nyuma unaweza kupelekea hali hii
 
deni
 

Attachments

  • images - 2026-06-21T191449.770.jpeg
    images - 2026-06-21T191449.770.jpeg
    60.2 KB · Views: 17
  • images - 2026-06-21T180636.503.jpeg
    images - 2026-06-21T180636.503.jpeg
    55 KB · Views: 15
  • images - 2026-06-21T180614.061.jpeg
    images - 2026-06-21T180614.061.jpeg
    43.6 KB · Views: 13
Wakuu Kuna ukweli wowote kwenye hiyo comment ya Athumani Sarafu?
Screenshot_20260621-232221.jpg
 
Ufalme unazidi kufitinika
wamteke na huyo wampoteze kama Polepole, tuone mwisho watabaki wangapi

ndani ya CCM wapo wengi hawapendi maovu yanayofanywa na utawala uliopo
Hiki kisiki huyu unaweza kuta ni zaidi ya deep state huyu mama hata kipindi cha Magufuli ukumfuatilia huyu yuko lank moja Migiro Mumalamula Huyu kafanya kazi UN
 
Ufisadi uliowahi kufanyika na baadhi yenu huko nyuma unaweza kupelekea hali hii
Hiyo haiwezi kumyima haki yake ya kutoa maoni wa afrika huwa tuna pima maoni ya mtu hoja ya mtu bila kujali mabaya yake kila kwenye baya Jitahidi kungamua njema utajifunza mengi
 
1782014622951.png

... 'ako kamama ni kubwa la vigagula! ( ... 'ata kina Warioba ni walewale wanywa uji wa mgonjwa)

NB: 1) Kundi lao ndani ya CCM ni makatili na mafisadi usiombe! (waligawana mpaka nyumba za serikali kwa bei ya mboga na kufanya ubinafsishaji mwingi wa kifisadi huku wakijificha nyuma ya kichaka cha uzalendo, unyonge na ujamaa!
2) Tunachokiona ni vita ndani ya CCM, ... yaani ni kunyang'anyiro cha nani aweke mtu wake bandarini na mauzo mengine ya nchi!

#FAGIA CCM WOTE!
 
Muheshimu Samia yatasha huyo anaipenda nchi sio chama. pampja na makosa yake huko nyuma anasimama ktk ukweli.
ni kweli,
mbibi wa pesa ya mboga anaipenda sana nchi japo kawa mkavu mno baada ya kua nje ya mfumo.

na bado 🐒
 
Back
Top Bottom