Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Florens Martin Turuka, Katibu Mkuu Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Amemteua Bi. Beng’i Mazana Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa. Bi. Beng'i ni Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Amemteua Prof. Tumaini Joseph Nagu kuwa Mganga Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Prof. Nagu alikuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Tiba, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Prof. Nagu anachukua nafasi ya Dkt. Aifello Sichalwe ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Amemteua Bw. Deusdedit Kamalamo Bwoyo kuwa Mkurugenzi wa Idara va Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii. Bw. Bwovo alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki.
Amemteua Bw. James Mahanga Sando kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (Public Procurement Appeals Authority - PPAA). Bw. Sando alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Kampuni ya Crown Accounting and Consulting Firm, Dares Salaam.