Prof. Wajackoyah aomba Rais Samia amruhusu awekeze kwenye bangi

Prof. Wajackoyah aomba Rais Samia amruhusu awekeze kwenye bangi

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Mwenyekiti wa chama cha roots na mgombea urais katika uchaguzi uliopita nchini Kenya Profesa George Wajackoyah yupo hapa Tanzania muda mfupi amemaliza kuongea na EATV na kuomba kuonana na Rais Samia ili awekeze katika kilimo cha bangi, profesa Wajackoyah aligombea uchaguzi nchi Kenya kwa sera ya kulifanya zao la bangi kuwanufaisha wakenya na kukili kubwa yeye pia amekuwa mtumiaji mzuri wa madawa hayo ya kulevya tangu akiwa mdogo.

''Niko na jambo ningependa kuanza mazungumzo na Rais Samia na CHADEMA tuangalie kama tunaweza kujenga uchumi wetu maana tuko na bangi nyingi sana na eneo la Kilimanjaro linaweza kuzalisha bangi bora sana duniani'' - Prof. George Wajackoyah, Kiongozi wa Roots.

''Nikipata nafasi ya kumuona Rais Samia nitamshukuru mama yeye ndio mama yetu hapa Afrika Mashariki na ni mtu ambaye tunataka tumkarimu na tumpende. Kenya tutakuja kuwa na mama lakini yeye ndio mama wa kwanza'' -

Prof. George Wajackoyah, Kiongozi wa Roots.

#EastAfricaRadio #SupaBreakfast

USSR
 
Nchi yetu hii bado iko usingizini Sana. Bangi ilipaswa kuchangamkiwa ili tuweze kuingiza fedha za kigeni kwa wingi.

Nchi kibao washaanza kuifanya bangi kuwa zao la biashara lkn sisi tunaendelea kukamatana tu.

Tutakuja kistuka wakati halina thamani kabisa
 
Wakiruhusu kilimo cha bangi hakuna kijana ataendesha Bodaboda mtaani
 
Hii nchi hata mirungi wanazuia tumekalia uchumi huku umasikini umetawala.
 
Hii nchi hata mirungi wanazuia tumekalia uchumi huku umasikini umetawala.

Somalia na kenya inaingiza mabilioni ya pesa kwenye mirungi kuliko kawaida sijui alieleta ujamaa alikua na maana gani yaani hatupo kiushindani hapa duniani
 
Mwenyekiti wa chama cha roots na mgombea urais katika uchaguzi uliopita nchini Kenya Profesa George Wajackoyah yupo hapa Tanzania muda mfupi amemaliza kuongea na EATV na kuomba kuonana na Rais Samia ili awekeze katika kilimo cha bangi, profesa Wajackoyah aligombea uchaguzi nchi Kenya kwa sera ya kulifanya zao la bangi kuwanufaisha wakenya na kukili kubwa yeye pia amekuwa mtumiaji mzuri wa madawa hayo ya kulevya tangu akiwa mdogo
  1. Picha yake tafadhali
  2. Kabla ya yote aongee na Ruto hukuhuko kwanza ndipo aje huku
  3. Rais aongee na mtumiaji wa mmea!!
 
Hebu amuache mama kwanza maana kama anataka kwenda na mjani pale mahala patakatifu akauwashe pale itakua patashika

Laprofeseri tulia muache mama
 
Nchi yetu hii bado iko usingizini Sana. Bangi ilipaswa kuchangamkiwa ili tuweze kuingiza fedha za kigeni kwa wingi.

Nchi kibao washaanza kuifanya bangi kuwa zao la biashara lkn sisi tunaendelea kukamatana tu.

Tutakuja kistuka wakati halina thamani kabisa
Vp umevuta mala ngapi leo?
 
Chama hiki sio cha kukiamini kabisa
20230222_094053.jpg
 
Bangi sio Tatizo

Tatizo sio Bangi

Watu ndio Tatizo

Vita ya bangi ililetwa na kutumiwa kama Silaha ya kukandamiza Jamii. Mizizi yake karne lukuki zilizopita, pale watu wa Ulaya walipohenyeshwa nyakati za Mongolian Empire. Kama kawaida yao mabeberu haya yana visa....vizazi vingine vikachukua haya na kuleta visasi vyao katika karne za hivi karibuni, na kupitisha sheria kali dhidi ya 'Wachina' kwenye bara waliloteka.....suala la bangi kuhusishwa na Makabila tofauti na ya Ulaya ni suala la Chuki, ni saula la Visasi.

Leo hii hawa mabeberu, kana kwamba wamejitoa ufahamu na kwa ulafi wa hali ya juu wanabadilisha gia angani.....'Sayansi haijaonyesha athari za bangi' na ndio tunaona na kuelewa nadharia iliyojengwa kwa uhasama hasi ikipurutika na kujengewa hoja na nadharia za kibepari bepari.

Sheria na mitazamo ya Bangi ibadilishwe tuende na Wakati.
Hatuwezi kuendelea kupigana vita zisizotuhusu. Kuna ulazima wa kuchukua 'Advantage' kwa sasa.

Kitaeleweka
 
Back
Top Bottom