Profesa Baregu afunguka sakata la Membe na 2020

Profesa Baregu afunguka sakata la Membe na 2020

Joined
Apr 18, 2012
Posts
95
Reaction score
213
B-Membe.jpg

Sakata la tuhuma dhidi ya Bernard Membe kuanza mapema mchakato wa kuwania nafasi ya kugombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi ujao, lililowekwa wazi na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Bashiru Ally limemuibua Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu.

Profesa Baregu ameeleza kuwa sakata hilo linatoa fursa chanya kwa kambi ya upinzani endapo halitatafutiwa ufumbuzi mapema, kwani inaonesha dhahiri kuwa ndani ya CCM bado kuna makundi.

“Membe [wa Twitter] amejibu vizuri kidiplomasia. Ila naona huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM ni kama kuna makundi sasa. Mambo yanaweza kuwa magumu kwa CCM kwa sababu wanaweza kupata mgombea ila asiungwe mkono na wanachama wake wakachukua hatua,” amesema Profesa Baregu.

Dkt. Bashiru amemuita Membe ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Awamu ya Nne na pia alikuwa miongoni mwa waliowania nafasi ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015.

Katibu Mkuu huyo wa CCM alimtaka Membe kufika ofisini kwake ili azungumze naye kuhusu tuhuma hizo, akiweka msimamo kuwa njia aliyotumia kumuita kupitia mkutano wake ni njia sahihi kwani hakuna mwanachama mwenye nguvu kuliko chama.

Mwanasiasa huyo amekuwa kimya tangu kumalizika kwa mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hivi karibuni, alikuwa miongoni mwa makada wakongwe na viongozi wa CCM waliotuhumiwa na Syprian Musiba kuwa wanahujumu chama hicho, akitajwa kuwa anafanya vikao vya chinichini kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Source: Dar24 Profesa Baregu afunguka sakata la Membe na 2020
 
Hakuna kitu, Membe ataenda na ataonywa ata nyamaza ni mtu ambaye kwa nyazifa zake hawezi kufanya chochote maana anaweza kujitia matatani fasta.
Tena kwa huyu jamaa atakutana na mateso ya Pilato
 
Kete za upinzani zimekwisha ndiyo maana wanambembeleza nape, mwigulu na Zitto
Una ushahidi wa haya? Fala kama mwigulu jimbo lake ambalo halina maendeleo yoyote wanini? Zitto ni mavi alishawekwa maliwato hawezi rudishwa tumboni napegwa nnauye ana nini zaidi ya kubwata ushafika mtama jimbo baya na lakimaskini kuliko yote?
 
Kuna kitu nahisi hu ni mtego wa maneno amewekewa Membe ili amalizwe kisiasa
 
Akili za nyuma hizi, endelea kupambana na utoto wako mpaka ubwabwa wa shingo utakapokutoka.
Ndo lugha zenu mkikutana na hoja, hata wanaharakati wenu washawajua sasa mlivyo vizuri kwenye lugha za kuudhi na matusi
 
Ndo lugha zenu mkikutana na hoja, hata wanaharakati wenu washawajua sasa mlivyo vizuri kwenye lugha za kuudhi na matusi
Pensheni za wazee wote wenye miaka 60+ na million 50 kila kijiji mmeshatoa?
 
Hakuna kitu, Membe ataenda na ataonywa ata nyamaza ni mtu ambaye kwa nyazifa zake hawezi kufanya chochote maana anaweza kujitia matatani fasta.
Hata kabla ya hapo alikuwa amenyamaza, au unamaanisha kunyamaza jumla mkuu?
 
Hakuna kitu, Membe ataenda na ataonywa ata nyamaza ni mtu ambaye kwa nyazifa zake hawezi kufanya chochote maana anaweza kujitia matatani fasta.
Umeona ehh
 
Una ushahidi wa haya? Fala kama mwigulu jimbo lake ambalo halina maendeleo yoyote wanini? Zitto ni mavi alishawekwa maliwato hawezi rudishwa tumboni napegwa nnauye ana nini zaidi ya kubwata ushafika mtama jimbo baya na lakimaskini kuliko yote?
tulia We Kada Wa Chama Mpevu, Jenga Hoja Acha Matusi Siasa Huzijui
 
Hata kabla ya hapo alikuwa amenyamaza, au unamaanisha kunyamaza jumla mkuu?
Tunza maneno yangu ata atakachoulizwa na atakacho waambia ni tofauti, hakika hamtakaa mjue nini kinaendelea.
 
Back
Top Bottom