Profesa Baregu aonya majungu mjadala wa rasimu ya katiba

Profesa Baregu aonya majungu mjadala wa rasimu ya katiba

Nafikiri wengi wanataka ama Serikali moja au tatu
 
Laana mbaya sana, hata Warioba hatumsikii. Hapa chama hakuna.
 
Awali diwani wa Kata ya Muze, Kalolo Ntilo alisema kuwa suala muungano wa Serikali tatu ambalo rasimu imependekeza hakubaliani nalo ila anataka kuwepo Serikali mbili za Tanzania bara na Zanzibar ambazo zitaunda muungano wa nchi hizo mbili huku wakiwatupia lawama wasomi kwa kudai wanataka kuwepo Serikali tatu ambazo athari zake ni kuvunjika kwa muungano miaka kadhaa ijayo.

Mkazi wa Kaengesa, Lazaro Muntama alisema kuwa ili kunusuru muungano kutovunjika ipo haja ya kuwepo kwa Serikali tatu yaani ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano ambapo alipinga hoja za baadhi ya wajumbe zinazoeleza kuendesha serikali hizo ni gharama kubwa.

"imefika wakati sasa na sisi watu wa bara tunataka Serikali yetu ya Tanganyika ili tuwe na muundo wa Serikali tatu siyo mbili huku ni kujizudhuru haki yetu.
Hivi Muungano haupaswi kuvunjika hata kama pande walizoungana hawautaki tena? Na kama ni hivyo huu ni Muungano wa nani na nani? Kwa nini ni vigumu sana kuacha Tanganyika na Zanzibar ziwe dola huru? Kama itaonekana sote tunauhitaji Muungano kwani si tunakaa pamoja na kuungana tena kwa namna ya mahitaji ya wakati huo?

Is Union a Taboo that should not be broken? Is Union a God ordained Marriage or what?

Hapo kwenye green sawa lakini Muungano uondoke tu!

CC: Ng'wamapalala Mzee Mwanakijiji Nguruvi3 jmushi1 GHIBUU Bin Faza TUMBIRI et al
 
Last edited by a moderator:

Haihitaji kuwa rocket scientist kutambua kuwa kama unataka kujenga nyumba imara lazima msingi wake pia uwe ni imara.

Tatizo la huu muungano siyo yaliyojiri baada ya muungano bali kilichosababisha muungano na kama kipo, ni kweli bado kinahitajika katika mazingira ya sasa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Muungano uliweza kusimama kwa sababu haukuwahi kutikiswa na upepo mkali wa kisiasa unaovuma kutokana na wananchi kufunguliwa macho na midomo ili kuweza kupambana na hoja za kisiasa ndani ya demokrasia ikiwa ndiyo wajibu wao katika mstakabari wa maisha yao kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kwa sasa kipindi cha hoja za nguvu ambazo ndizo zilifanikisha kwa kiasi kikubwa kuwepo na 'kukubalika' kwa muungano hakipo tena. Wananchi wanakuja na nguvu za hoja kutaka kujua chimbuko lake na manufaa kwa wananchi, unfortunately, CCM ambao ndiyo waasisi wa muungano hawajatoa nguvu ya hoja kuweza kujibu maswali haya ya msingi.

Medani za vita zinasema, retreat is not defeat kwa maana kuwa, hata kwenye siasa siyo vibaya kurudi kwenye drawing board tena na kuanza upya kutokana na kushindwa kupata mbadala wa matatizo yanayoongeza kuhusu muungano siku baada ya siku.

CCM wanapenda tuendelee na muungano huu uliopo lakini hawataki kusema sababu zake kwa ufasaha. Tume ya katiba inapenda tuwe na serikali tatu, lakini kiuharisia hii ni lugha ya kisiasa kusema, huu ndiyo mwisho wa muungano.

Yetu macho.
 
I like it. fiew words but yanamaana sana.
 
Mjomba watu hawakupewa midomo wakati huu ndio wakahoji ispokuwa hapo awali muungano huu ulichukuliwa kama ni sheria ambazo ukivunja unahukumiwa, kwa maana ya kwamba ukiongoea kuhusu neno muungano wakati huo wewe unakuwa muhaini, unakwenda jela ukibahatika, au unapotea kimiujiza, hayo ndio akiyafanya nyerere.

Muungano huu, ulikuwa wa lazima toka hapo ulipo asisiwa , baaada ya miezi mitatu tu, ulianza kuwa na kasoro, mpaka hii leo unalalamimikiwa.

Nadhani kama tunataka kuwa na muungano ambao utakuwa na foundation nzuri kwanza turudishiwe mataifa yetu mamlaka kamili, Tanganyika na Zanzibar , halafu baadae tuje tukae juu ya meza kujadili muungano wa aina gani tunao taka na yepi tushirikiane, naona hio ndio foundation nzuri ya muungano.

Ukiangalia sasa huu muungano unayumba kwa sababu hiyo foundation haipo, ,Tanganyika haipo, Zanzibar haina mamlaka yake, vipi mambo haya ?
 
Ng'wamapalala GHIBUU na ndipo najiuliza ni kitu gani kigumu kueleweka na wanasiasa hapo?
Serikali tatu za nini?
 
Last edited by a moderator:
Ng'wamapalala GHIBUU na ndipo najiuliza ni kitu gani kigumu kueleweka na wanasiasa hapo?
Serikali tatu za nini?
Kiufupi wanaogopa aibu, kuvunjika kwa muungano huu hawa viongozi wanaona aibu, eti wanajisifia dunia nzima kuwa muungano mzuri na wapekee, ni kweli wa pekee mkubwa kumnyanyasa mdogo, ila muungano huu haupo kisheria,umevunjika muungano huu pale tanganyika kujita tanzania, ulivunja makubaliano ya muungano.

Inakuwaje tujadili katiba ya muungano wakati tanganyika haipo ? Ni sawa watu kujadili harusi wakati biharusi hayupo ila mume yupo tunapanga ndoa vipi ndoa hio hio ? Kwanza tumtafute biharusi na bwana harusi, ikisha tufanya ndoa. Inamaana ya kwamba kwanza Tanganyika irudi, then tukae juu ya meza tuunde shirikisho na hivyo kwa sasa haina haja tena kwa sababu EAC ipo .

Cha msingi ni kutiliana mikataba ya kushirikiana tu, kama vile china na Tanzania au America na Tanzania .
 
Kiufupi wanaogopa aibu, kuvunjika kwa muungano huu hawa viongozi wanaona aibu, eti wanajisifia dunia nzima kuwa muungano mzuri na wapekee,
Aibu ya nini? Azimio la Arusha limekufa hakuna anayeona aibu. Ujamaa umekufa hakuna anayeona aibu. Kwa nini kwa hili tuone aibu? Tufanye lililo na manufaa kwa nchi, aibu haina nafasi katika maamuzi!

ni kweli wa pekee mkubwa kumnyanyasa mdogo, ila muungano huu haupo kisheria,umevunjika muungano huu pale tanganyika kujita tanzania, ulivunja makubaliano ya muungano.
Nakubaliana na wewe kuwa kisheria hakuna Muungano hasa ila nikukumbushe mambo machache. Sijajua una maana gani kusema mdogo anamnyanyasa mkubwa kwa kuwa Mzanzibari anamiliki ardhi bara ila si kinyume chake ingawa ni nchi moja. Na sio hilo tu angalia hata idadi ya Wabunge ulinganishe na "umbo la mdogo". Issue ya umeme nadhani unaifahamu na mengine kadha wa kadha. Ninyi wenzetu mna baraza la wawakilishi kuwatetea katika mambo ya Zanzibar, sisi hatuna. Mna rais wenu sisi hatuna. Mna mahakama, wimbo wa Taifa na mengineyo ambayo sisi hatukuyakuta na hatuna!

Hivyo kusema kwamba Watanganyika tunawaonea sio sawa. Sijawahi kuona Mtanganyika yeyote akimuonea mzanzibari kwa sababu ya Uzanzibari wake, bado! Ila kwa kuwa Wazanzibari wanajisikia wanaonewa na kwa kuwa muungano huu sio ndoa kutoka mbinguni na kwa kuwa Watanganyika tunaona Zanzibar ni kama inapendelewa ni vema tukatengana kwa amani. Hii italeta kuheshimiana zaidi kwa kuwa manung'uniko kama haya hayatakuwapo tena.

Inakuwaje tujadili katiba ya muungano wakati tanganyika haipo ? Ni sawa watu kujadili harusi wakati biharusi hayupo ila mume yupo tunapanga ndoa vipi ndoa hio hio ? Kwanza tumtafute biharusi na bwana harusi, ikisha tufanya ndoa. Inamaana ya kwamba kwanza Tanganyika irudi
Hakuna logic hapo. Ili Ujadili Muungano lazima wadau wa Muungano wawepo. Hii ya Wanasiasa na hasa CCM kutuambia mambo ya Watanganyika yasimamiwe na serikali ya Muungano, mimi binafsi yamenikinai! Warudishe Tanganyika yetu na si kama Chadema wanavyosema serikali tatu au CCM serikali mbili bali iwe Dola huru! Wazanzibari nao wajiundie dola yao. Undugu wetu ulikuwepo kabla ya mwaka 1964 na utaendelea hata baada ya Muungano.

Hatukuwa ndugu kwa sababu ya Muungano, tuliungana kwa sababu tulishakuwa ndugu. Na hivyo kufa kwa Muungano sio kufa kwa udugu huo!

then tukae juu ya meza tuunde shirikisho na hivyo kwa sasa haina haja tena kwa sababu EAC ipo .
Tuachane kwanza ili tuone kama kuna mahali tunahitaji kuungan na kisha tuungane kulingana na mahitaji hayo!

Cha msingi ni kutiliana mikataba ya kushirikiana tu, kama vile china na Tanzania au America na Tanzania .
Ujirani mwema kama Kenya, Malawi na Mozambique! That is it!
 
Stefano Mtangoo

Hivi Muungano haupaswi kuvunjika hata kama pande walizoungana hawautaki tena? Na kama ni hivyo huu ni Muungano wa nani na nani? Kwa nini ni vigumu sana kuacha Tanganyika na Zanzibar ziwe dola huru? Kama itaonekana sote tunauhitaji Muungano kwani si tunakaa pamoja na kuungana tena kwa namna ya mahitaji ya wakati huo?

Is Union a Taboo that should not be broken? Is Union a God ordained Marriage or what?

Hapo kwenye green sawa lakini Muungano uondoke tu!

CC: Ng'wamapalala Mzee Mwanakijiji Nguruvi3 jmushi1 GHIBUU TUMBIRI et al

hawa ndugu zetu wana CCM, wanaufanya muungano ni dini yao

sisi tuna uona muungano si zaidi ya bughuza tu, hakuna mtu anafaidika na chochote

Sifahamu mtu wa Muze anafaidika na nini na hu muungano?
 
Huyo diwani inaonyesha wazi hajui hata anacho jadili kwamba ni kitu cha kudumu ambacho kikijadiliwa kwa umakini katiba hiyo itadumu vizazi kadhaa! Yeye anadhani jambo dogo,kwa hiyo zibaki serikali 2 na matatizo yake na baada ya miaka michache tuanze kujadili jambo lile lile!!! Haya mabaraza ya kata yaliojaa wana ccm ni janga!
 
Back
Top Bottom