TANZIA Profesa George Shumbusho afariki dunia

TANZIA Profesa George Shumbusho afariki dunia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho amefariki dunia leo Jumatano Februari 24, 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Profesa Ganka Nyamsogoro ambaye ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema Profesa Shumbusho aliyekuwa Rais wa Ndaki ya Mbeya, amefariki saa 6:30 mchana.

Profesa Honest Ngowi, Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam (MUDCC) amesema Taifa limepoteza msomi katika lugha ya mawasiliano aliyebobea kwa miaka mingi.

“Alinifundisha shahada yangu ya kwanza Mzumbe miaka ya 1990, baadaye tumeendelea kuwa pamoja Mzumbe na yeye akapelekwa kuwa Rasi wa Mzumbe Mbeya na mimi nikaletwa Dar es Salaam, lakini kwa ujumla alikuwa makini, mtafiti mzuri sana, ni majonzi na Taifa limepoteza mtu muhimu,” amesema.

Shumbusho.JPG

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom