Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT?

Baada ya hii aibu, ningekuwa Rais ningefukuza kuanzia Mwanasheria Mkuu na watu wote wanaohusiana na sheria kwenye ofisi yangu.

Haya mambo ya kuongezeana muda inamaana katika Majaji wote wa mahakama ya Rufani hajaona anayefaa kuchukua nafasi? Au kustaafu kwa Jaji mkuu kumekuja kama janga au msiba?
 
Inashangaza sana kuona rais anateua na kuongeza muda wa kiongozi wa Muhimili Mwingine, Tutegemee huo Muhimili utaweza kusimama kweli?
 
Kiongozi, JAJI MKUU anatoka kwenye kundi la MAJAJI. Utumishi wake unatambulika kutokana na ujaji wake, hivyo kama ameongezewa muda kama JAJI, basi anaendelea kuwa JAJI MKUU.
Umekosea
Hapa Mheshimiwa Rais alishauriwa vibaya.

Prof Juma angeozewa muda kuwa Jaji wa Rufani na sio kuendelea kuwa Jaji Mkuu
 
Kiongozi, JAJI MKUU anatoka kwenye kundi la MAJAJI. Utumishi wake unatambulika kutokana na ujaji wake, hivyo kama ameongezewa muda kama JAJI, basi anaendelea kuwa JAJI MKUU.
Unamaanisha JK ameongezewa muda na kuwa JR? Si astafu mtu wa watu apumzike awe mshauri na hii huwa njema sana. Sheria na Katiba inavunjwa na wale tunawategemea sasa wengine watafanyaje
 
Wakati mwingine Hawa Wakuu wa nchi Huwa wanasainishwa tu. Ikulu watu wanaloga jamani!

Jakaya aliwahi kuteua Jaji aliyekuwa undergraduate OUT. Ilizimwa zimwa ile, na nadhani Hadi Sasa anadunda.
Ina maana Undergraduate wa OUT hawezi kuwa Judge kama atatimiza masharti yaliyowekwa na Katiba?
Labda nimekunukuu vibaya, naomba unielezee kidogo ndugu DATAZ.
 
Wakati mwingine Hawa Wakuu wa nchi Huwa wanasainishwa tu. Ikulu watu wanaloga jamani!

Jakaya aliwahi kuteua Jaji aliyekuwa undergraduate OUT. Ilizimwa zimwa ile, na nadhani Hadi Sasa anadunda.
Alikuwa anaitwa nani huyo Jaji?
 
Wamezoea rushwa na kuabudiwa...kufanya kazi kwa mazoea, uzembe, uchawi fitina na choyo mno... naunga mkono hili.
 
Umekosea
Hapa Mheshimiwa Rais alishauriwa vibaya.

Prof Juma angeozewa muda kuwa Jaji wa Rufani na sio kuendelea kuwa Jaji Mkuu
Hii ni aibu kubwa sana kwa Mwanasheria mkuu wa serikali, hapaswi kuwa ofisini hata kwa sekunde moja baada ya waraka huo wa Mugasha J

Nampongeza sana Jaji Mugasha kwa kueleza ukweli huu ambao pengine utafanya achukiwe sana na watanzania wenzetu wajinga ambao ni wengi.
 
kumbe hii Kasumba ya Unatengeneza Tatizo halafu Unalitatua Mwenyewe, Kisha unajiona shujaa kumbe bado ipo 🤓
 
Kiongozi, JAJI MKUU anatoka kwenye kundi la MAJAJI. Utumishi wake unatambulika kutokana na ujaji wake, hivyo kama ameongezewa muda kama JAJI, basi anaendelea kuwa JAJI MKUU.
Sio kweli....kasome tena vizuri katiba ya nchi.
 
Wakati mwingine Hawa Wakuu wa nchi Huwa wanasainishwa tu. Ikulu watu wanaloga jamani!

Jakaya aliwahi kuteua Jaji aliyekuwa undergraduate OUT. Ilizimwa zimwa ile, na nadhani Hadi Sasa anadunda.
Nakumbuka kuna jaji aliteuliwa hana degree ya sheria ila Ana Masters ya sheria ila hii nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…