Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT?

Waraka hauna mashiko, UJAJI MKUU UNAKOMA PALE ANAPOSTAAFU. Sasa kama ameongezewa muda kuwa JAJI unasemaje hana sifa za Kuwa JAJI MKUU?
 
Hata hujasoma andiko lote la huyo mama. Ungesoma usingeandika hicho ulichoandika.

Shida ya Watanzania ku comment bila kusoma.
Nimelisoma na halina maana yoyote, yaani uongezewe muda wa UJAJI wako then ukose sifa za kuwa JAJI MKUU KISA UMRI?
 
Sheria inaruhusu sayansi kuamuwa umri wa mtu siyo makaratasi. Hususan kwa nchi zetu ambazo hazina "proper" records mpaka leo.

Hili wala siyo suala la kuumiza watu vichwa wala kuzozomoka. Wengi sana serikalini waliofikia umri na muda rasmi wa kustaafu wanapewa mikataba na wanaendelea na kazi.

Kuna wengine wasiotakiwa kuendelea na kazi wanastaafishwa kibabe bila kujali katiba wala ratiba. Rejea visa vya Profesa Assad na Ndugai. Sasa mmoja anafanya kazi zake chuo kikuu, mmoja yuko benchi.
 
Kwani shida ni nini?? Mradi si mtanzania,kwani hawana haki ua kushika madaraka?? Mbona hizi hisia hazikuwepo wanapotawala wa upande wa kikristo??magufuli ameteua baraza zima waislamu wawili tu mbona hakuna mtu aliyejitokeza kuhoji udini??

Mijinga mijinga
 
Jaji Stella Mugasha Apewe Maua Yake! kama nilivyo shauri hapa Jaji Mugasha Apewe Maua Yake Kupinga Uvunjifu wa Katiba Ukomo wa CJ, ila Mbona Hili ni Dogo Tuu, Kubwa ni Katiba Yetu Imenajisiwa! Why Wako Kimya?!.
P
 
Ningekuwa ndio mimi ningestaafu tu maana miaka 65 ni mingi. Hakuna cha kupoteza, mafao makubwa bado kuna pensheni ya kila mwezi
 
Watz tutafika mbinguni tumechoka sana, yani kila siku inaibuka mijadala mipya kabla ya zamani haijaisha. Tumekuwa kama bendera yani.
 
Waraka hauna mashiko, UJAJI MKUU UNAKOMA PALE ANAPOSTAAFU. Sasa kama ameongezewa muda kuwa JAJI unasemaje hana sifa za Kuwa JAJI MKUU?
kwahiyo alipostaafu june 15, ndio ujaji mkuu wake ulikoma kikatiba. na hakuna ibara inayoextend ujaji mkuu. ila kuna ibara inayoextend u JA. watu mnashindwa kutofautisha kati ya vyeo hivi viwili vinavyoundwa na ibara mbili tofauti.mnaviweka vyote pamoja na mnafeli sana.
 
Mwaka 2005 ilitumika ibara gani kumuongezea muda Jaji Mkuu B. Samatta?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…