Profesa Ibrahim Lipumba aifunda CHADEMA Dar...

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetakiwa kuweka kando tofauti za kisiasa na kuunganisha nguvu zao, hasa katika kipindi hiki ambacho taifa lipo katika mchakato wa uundaji wa Katiba Mpya.

Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akifungua mkutano wa baraza kuu la chama hicho.

Kauli hiyo ya Lipumba inakuja kutokana na vuguvugu la mgogoro ulioibuka hivi karibuni ndani ya CHADEMA ambao ulisababisha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe kuvuliwa nafasi zake zote za uongozi.

Uamuzi huo pia ulimkumba aliyekuwa mjumbe wa Kamati kuu ya Chama icho Dk Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
 
hakuna upinzani tanzania
 
Hamad Rashid ameruhuaiwa kugombea UKATIBU MKUU?
 
chadema ni chama makini,hawacheki na nyani ili waje kufuna mabua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…