Profesa Janabi apuuzwe!

Sawa.

Lakini, hayo yote hayahalalishi Profesa kusema ukikojoa mkojo wa povu tayari una ugonjwa wa figo.

Tunakojoa mkojo wa povu miaka na miaka baada tu ya kunywa pombe, na ukiacha kunywa pombe mkojo unarudi kuwa hauna povu.

Anatengeneza panic isiyo na lazima.
 
Mkuu, ukiandika tena fanya proof reading kabla ya kuiachia. Kuna sehemu napata shida kung'amua unachokimaanisha.

Turudi kwenye mada;
Kila ugonjwa una dalili. Na maradhi mbalimbali yanaweza kuwa na dalili zenye kufanana. Haimaanishi kuwa dalili fulani LAZIMA iwe ni kwa ajili ya ugonjwa fulani pekee.

Lakini hiyo haimaanishi tuache kutaja dalili za ugonjwa husika kwa kuhofia kuwa zina mfanano na ugonjwa mwingine.

Kabla ya kukupima lazima tukuulize unavyojisikia na hilo litatusaidia kudadisi ugonjwa unaokusibu kutokana na dalili tajwa. Vipimo vitathibitisha.

Prof Janabi alikuwa wazi kuwa dalili za ugonjwa wa figo ni moja, mbili tatu. Na maradhi ya figo yana nyakati tofauti. Ukishaona dalili alizoanisha Janabi basi unakuwa katika nyakati siyo za awali tena bali ugonjwa umeshaanza kukomaa.

Kwa hiyo sijaona kosa lake kutaja dalili hizo. Uthibitisho utakuja baada ya vipimo kufanyika.
 
Natumia simu, nakosoa typos muda wote. Kama kuna niliposahau hujaelewa naomba post number nipitie. Be specific.

Matabibu wana wajibu wa kutofanya mambo yawe mabaya zaidi. First, do no harm.

Na kama ulivyosema, kuna dalili nyingi, kama za uchovu, kukosa hamu ya chakula na kukojoa mkojo wenye povu, zinaweza kuwa za magonjwa mengi tofauti, au si za ugonjwa wowote ni hali fulani tu mtu anapitia kwa sababu kala au kanywa kitu fulani, kapitia mazingira fulani etc.

Sasa, it is irresponsibke kwa Profesa kusema ukikojoa mkojo wa povu tayari una ugonjwa wa figo, hii si dalili ya awali.

It is irresponsible kwa sababu, unaweza kukojoa mkojo wa povu bila kuwa na ugonjwa wa figo. Kuna mtu akila ma supplements fulani tu anakojoa mkojo wa povu.

Unaweza kukojoa mkojo wa povu mara moja kwa sababu umekunywa pombe tu. Ukapata kihoro ukaona una ugonjwa wa figo, Profesa Janabi kasema. Ukafa kwa heart attack. I am overdramatizing for effect, but there is a major point of creating unnecessary panic here. Wakati kumbe hata huo ugonjwa wa figo huna, umekojoa mkojo wa povu kwa sababu umekunywa pombe nyingi kwa nuda mfupi tu, au umekula supplements fulani tu.

This is simple logic that does not need a medical degree.

Profesa anatakiwa kuwa more nuanced kwenye matamko yake, kuna watu wanamsikiliza kama mtaalam na wanafuatisha kila anachosema, akisema mambo bila nuance, anawapotosha watu waone wana ugonjwa wa figo, wakati hawana.

Usichoelewa nini?

Matokeo ya kukosa nuance ndiyo haya sasa watu wanasema "Profesa Janabi apuuzwe", wanakosa msaada mzuri tu ambao Profesa angeweka nuance kidogo tu angeweza kuwasaidia vizuri zaidi.

Yani Profesa kafanya kama anapima joto kwa mkono badala ya kutumia thermometer kuwa specific zaidi.
 
Mkuu vizuri lakini Mwenye kazi hiyo Yupo ambaye ni Dr Ntuli Kapologwe ambaye anahusika na Public Awareness kuhusu Lishe na vingine vinavyohusu ulaji kwanini asiache mamlaka zinazohusika zifanye kazi..

Kama anaona hazifanyi kwanini Asishauri kwa sababu Naamini MNH wana kiti cha Ushari kwa wizara ya Afya atumie hicho..

MKuu nia ya Janabi Tangu akiwa JKCI ilikuwa ni kubring awareness ili wapate watu wengi wanaoenda kufanyiwa uchunguzi pale na kupata wateja wengi..
Hilo linafahamika...

Nia ya mtu unaipimaj?..

Na ndo maaana kwa kiapo hicho Kujitangaza kokote huhusishwa na uvunjaji wa Maadilu ya Kidaktari kwa sababu ni vigumu kupima nia Ya mtu...(Kama utakuwa kwenye Kada ya udaktari utanielewa nachosema)
 
Vizuri kabisa..
Alikuwa anapaswa kuwaambia watu wafanye uchunguzi ila sio kucome into conclusion moja kwa moja..
I second you!
 
Safi
 
Binafsi sikuwah mwelewa na simwelewagi kabisa ana mikwara uchwala sana, Ni anatetemekewa sana mpaka aga nashangaa kunani😅
Madaktari kama hawa ndo alexander the great aliusia walibebe jeneza lake siku ya kifo chake , dhumuni lilikuwa ni kuonyeaha linapokuja swala la kifo hata daktari mahiri hawezi zuia .
Janabi kweli ni daktari mzuri , ila anaonekana amelewa sifa hadi anasahau maisha yana ethics zake na hata hao madaktari nguli bado wanaugua hadi kufa magonjwa haya haya tunayokufa nayo sie ngumbaro.
Usile hiki, usifanye kile kumbe ahadi yako ya kifo ipo kwenye ajali ya gari !
 
Tatizo unamlisha Prof Janabi maneno.

Sijaona sehemu popote katika andiko lako na katika mazungumzo ya Prof Janabi alipotanabaisha kwamba ukiwa na dalili ulizoanisha hapo juu (kwa mujibu wa maelezo yake) basi HAKIKA una ugonjwa wa figo.

Dalili pekee haziamui bali vipimo. Lakini kwa kuwa alikuwa kwenye hadhara, ni lazima angeeleza dalili za ugonjwa husika.

Hawezi kuacha kuzitaja dalili kwa kuhofia kuwa jamii itamuelewa vibaya.

Nimepita mtandaoni kujaribu kutafuta video wakati akizungumza kwenye siku ya Prof Jay Foundation, bahati mbaya sijafanikiwa.

Na ni jambo la logic tu. Mtu hawezi kuambiwa anaumwa figo kwa dalili pekee. Hakuna daktari atakuambia kwa sababu una dalili hizi basi tayari unaumwa figo. Bali kuna uwezekano kuwa huenda unaumwa.
 
Mkuu, unajua kusoma kwa ufahamu au hiyo sehemu una tatizo nayo?

Hii direct quote ya Profesa Janabi uliiona au uliiruka?

Amesema.

""Ukiwa na hizi dalili sio za mwanzo tena, tayari wewe umeingia kwenye ugonjwa wa Figo"
 

Angekua makini asingekua anavaa miwani. Haya mambo ni kuwa na kiasi tu , hakuna haja ya kutishana.

Ukitaka kuwa na maisha magumu au wasiwasi msikilize Profesa na ujifanye kumzingatia.
 
Mkuu unachanganya file. Taarifa maalum za serikali zinakuwa channeled kupitia kwa vyanzo rasmi. Lakini haipo limited kwamba ni LAZIMA ipitie kwa mtu fulani.

Isitoshe Prof Janabi ni Mkurugenzi wa NH. Anaposimama kama alama ya taasisi yake basi hawezi kuacha kuzungumza kwa sababu eti anayepaswa kuzungumza ni fulani. Hiyo haipo.

Kuna podcasts kibao, zinafanywa na Muhimbili National Hospital. Wanaozungumza ni wataalam, akiwemo Prot Janabi. Wala si msemaji wa MNH.

Kama anazungumza lengo lake mama likiwa kuleta awareness basi anapaswa kupongezwa. Watu kwenda kufanyiwa uchunguzi kama matokeo ya awareness waliyoipata basi ni jambo jema.

Na jambo la kheri ni kuwa, hawashauri waende Muhimbili au JKCC tu. Popote pale wanaweza kwenda.
 
Mkuu, unajua kusoma kwa ufahamu au hiyo sehemu una tatizo nayo?

Hii direct quote ya Profesa Janabi uliiona au uliiruka?

Amesema.

""Ukiwa na hizi dalili sio za mwanzo tena, tayari wewe umeingia kwenye ugonjwa wa Figo"
Hiyo quote nimeiona. Naomba kupata uthibitisho kwamba ameyazungumza hayo.

Kwenye andiko langu nilikuambia, nimejaribu kutafuta video ili niweze kujihakikishia akizungumza. Lengo lilikuwa kutaka kupata usahihi huo. Sijafanikiwa.

Kwa kuwa wewe umehitimisha, basi tuwasilishie video yake akizungumza hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…