Mkuu unachanganya file. Taarifa maalum za serikali zinakuwa channeled kupitia kwa vyanzo rasmi. Lakini haipo limited kwamba ni LAZIMA ipitie kwa mtu fulani.
Isitoshe Prof Janabi ni Mkurugenzi wa NH. Anaposimama kama alama ya taasisi yake basi hawezi kuacha kuzungumza kwa sababu eti anayepaswa kuzungumza ni fulani. Hiyo haipo.
Kuna podcasts kibao, zinafanywa na Muhimbili National Hospital. Wanaozungumza ni wataalam, akiwemo Prot Janabi. Wala si msemaji wa MNH.
Kama anazungumza lengo lake mama likiwa kuleta awareness basi anapaswa kupongezwa. Watu kwenda kufanyiwa uchunguzi kama matokeo ya awareness waliyoipata basi ni jambo jema.
Na jambo la kheri ni kuwa, hawashauri waende Muhimbili au JKCC tu. Popote pale wanaweza kwenda.
Mkuu hujanielewa, katika uongozi Si kila mtu huwa anaongea tu kwakuwa anajua kitu hatuendi hivyo...
MNH iko chini ya Wizara ya Afya na haiko nuu yako kuna hierarchy mbalimbali na Kuna wasemaji mbalimbali kwenye kila Wizara...
Unafikiri ingeruhusiwa kila mtu aseme kwakuwa anajua Ingekuwaje?..
Ingekuwa chaos kila mahali kwakuwa Daktari huyu kasema hivi yule kasema vile yule kazuia hivi na yule karuhusu hiki..
Na ndo maana tuna Chain of protocol,Mabalaza ya kitaaluma, Mabaraza ya kibingwa na mabaraza mengi tu..
Yeye ni msimamizi ndiyo wa MNH, Je uliwahi kuwasikia wasimamizi wengine wakifanya hivyo??
Je unamsikia Msimamizi wa JKCI wengine wakiongea kama alivyokuwa anaongea yeye baada ya kuondoka..?
Kuna tofaufi kubwa sana kati ya utaalamu na Siasa..
Wapo wanaofanya hizo kazi na wameajiriwa kwa kazi hizo kwanini asiache watu wafanye kazi zao..
Na yeye akabaki mshahuri kwa sababu Ya chief Consultants yake..?
Viongozi wanashindwa kumwambia kwa sababu wanaepusha majibizano Ya kitaaluma ila Niamini kuwa hawapendi kiherehere Chake..
Msemaji wa Magonjwa ya Moyo Taifa yupo,Msemaji wa Lishe yupo, msemaji wa Mgonjwa yasiyo ya kuambukiza yupo..
Ili mpasa yeye kama Proff Janabi astick kwenye JD (Job description) yake kama Mkurugenzi wa MNH..
Hayo mengine awaachie Wizara ya Afya na CMO (Chied Medical officer- Mganga mkuu Taifa)..
wataamua..
Narudia Tena Kama anaona hawafanyi kazi kama inavyostahili... kwenye Baraza la Madaktari Muhimbili wana Kiti pale, wizara ya Afya muhimbili wana kiti chao hakuna Barza ambalo muhimbili hawana kiti kwanni asitumie mabaraza hayo kurekebisha...