Profesa Jay: Afya yake imefikia huku…aliendesha kutoka Bukoba, Aliandaa wimbo afanye na Zuchu, kuna Wahuni…

Profesa Jay: Afya yake imefikia huku…aliendesha kutoka Bukoba, Aliandaa wimbo afanye na Zuchu, kuna Wahuni…

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Black Rhino ambaye ni mdogo wa Profesa Jay amezungumzia kuhusu maendeleo ya kaka yake ambaye amelazwa Muhimbili.

Joseph Haule au Jay ambaye ni mwanasiasa na msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, alikuwa yuko sawa, alienda Bukoba akafanya shoo fresh tu na kudrive kurudi Dar na kuendelea na mishe zake.

“Akiwa yupo Bukoba kwa ajili ya shoo alianza kulalamika kuwa hajisikii vizuri lakini kwa kuwa alikuwa ameshachukua hela ya watu akaamua kufanya shoo na kuondoka kurudi Dar.

“Alipofika hapa (Dar), ikawa kama wiki hivi, analalamika hajisikii vizuri, anaenda hospitali anapewa dawa na kuendelea na maisha, lakini siku kama ya saba hivi tangu atoke safari akasema hajisikii vizuri akaomba tumpelekea hospitali.

“Hivyo, kuhusu anasumbuliwa na nini hilo ni suala la kwake binafsi siwezi kuliingilia au kulizungumzia hadharani.

“Hizo taarifa zinazoendelea mitandaoni siyo za kweli na imetusikitisha sana familia.

“Ukiwa unapitia kitu kama hiki kisha unaona mitandaoni watu wanaongea mambo ambayo siyo ya kweli, imetusikitisha sana kwa kuwa kuna watu hawana ubinaadamu.

“Siyo uungwana kuona mwenzako anaumwa kisha unaanza kusambaza taarifa ambazo siyo za kweli, hao watu ni wahuni au siyo wastaarabu wanaosambaza hizo taarifa, kuna hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa kuhusu uwongo wanaosambaza mitandaoni.

“Watanzania wapunguze hofu, Jay anaendelea vizuri, japo brother alikuwa anaumwa, yaani anaumwa sana lakini kwa sasa kuna nafuu, tuwekeze nguvu kuendelea kumuombea ili anyanyuke na kuweza kutoka hospitali.

“Nilipokuwa kwake mara ya mwisho alinisikilizisha kazi zake na kuna moja alitaka kufanya kazi na Zuchu, akaniambia nimpe ushauri,” anasema Rhino ambaye naye pia ni msanii wa Bongo Fleva.

profesa-jay.jpeg

 
Watangaza Habari / Wasambazaji wa Habari hata kama ni za kweli au Uongo wamekosa Ustaarabu

Na huyu dogo kutumia muda na rasilimali sijui kuanza kufuata sheria sijui ili kuwawajibisha hao wakosa Ustaarabu na yeye anakosa Ustaarabu na Hekima...

Yeye angesema anachosema kwa ufupi na kuwashukuru wote waliofanya mema sio kuwashutumu waliofanya mabaya (huu sio wakati wake) Atasema mwenyewe Prof Siku akirudi Mtaani....

 
Nimesikia zuchu 😁 kwahyo mwana tandale amewahi kete km hawa huyu👇
FB_IMG_16444323388616874.jpg










then J ndoivo tena
 
Stay strong NiggaJ
ALLAH akufanyie wepesi upate kurudia hali yako ya kawaida
 
Kuna watu walidai familia ya Jay inaomba michango ya matibabu kwa watanzania. Nafikiri hilo ndio limewakwaza sana, sijui watu wanapata nini kutunga uongo!
 
Kuna watu walidai familia ya Jay inaomba michango ya matibabu kwa watanzania. Nafikiri hilo ndio limewakwaza sana, sijui watu wanapata nini kutunga uongo!
Wala sio hilo ila kuna wajinga walimpa ugonjwa mbaya
 
Lakini mnakwendaje kuomba msaada kwa jamii halafu mnaogopa kusema mgonjwa anasumbuliwa na nini? Kwanini mnaficha ugonjwa?
 
Back
Top Bottom