ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
VERSE..1
Nashukuru Macho yangu mawili hayana upofu/ na mdomo upo wazi kukemea mambo maovu/ siku inapofika naona Heri ya jana/ maisha ya wabongo yanakuwa kama ya wanyama/ hiki ninachosema kila jicho linaona/ nina futa chozi la mnyonge kilio cha kila kona/ damu ya mtanzania naona sasa inavuja/ na hali ya hatari kwa kasi nayo inakuja/ ni macho mangapi yanatazama hospital Kina mama wanajifungua kwenye mazingira ya hatari/ utu unatutoka inapotokea Ajali/ majeruhi wana uwawa watu waibe mali/ nafuta jasho la mlala hoi chozi la mnyonge/ na ililia damu ya zanzibar wote tuombe/ jasho linashamili kwenye Uso wa mlala hoi/ na sauti inakauka kwenye koo la Turn boy..
CHORUS..
Tunaishi kama hakuna kesho/
Amani kwa yatima,kina mama, watoto wenye mateso
Machozi ,jasho na damu kwa watanzania /
Ya wote tuwe pamoja tu sali kwa nia/
Tunauwana kama hakuna kesho/
Amani kwa machinga ,wana Apolo,masela wenye mateso/
Machozi,jasho na Damu kwa watanzania /
Na mungu atasikia tusali kwa nia...
VERSE..2..
Msalamba wa dhiki bado una muelemea / mtanzania halisi hana pa kuengemea/ najaribu kuishika vizuri fimbo ya mnyonge/ nwendo wa miguu mitatu na anapiga moyo konde/ mkutano wa Beijing ungefanyika kijijini/ labda na bibi yangu nae angekuwepo ku ndini/ misaada haipati inaishia mijini/ tajiri anaongezewa ni vipi kwa masikini/ ninasema kwa Uchungu wengine wananicheka/kwenye kambi ya lahana ujue wewe mateka/ siasa ya kiBongo imeanza kunuka Damu/ndugu watanzania wana uwana kwa zamu/ nani ataizoa damu inayo mwangika / nyerere alitabiri ya kwamba tuta adhirika/ siasa sio mchezo kama karata tatu/ jazba inapo panda ina ng'oa nyoyo za watu/ mishale na mikuki imetawala kilosa/ nachali na wachaka wauwa bila makosa/wote walikufa mungu walaze pema/ rehemu marehemu wapate safari njema/ futa machozi yangu msanii ya hati miliki/ kila nikijivuta naona si thaminiki / upendo unatoweka ngiza ndio linatanda/ unyama ufedhuli mututu juu ya Anga/ msio penda Amani toeni na roho yangu/ mnao nyonya watu sikia kilio changu/ mnaotaka haki guseni na hoja zangu/ wote wenye mateso shikeni mkono wangu...
CHORUS..
Tunaishi kama hakuna kesho/
Amani kwa yatima,kina mama, watoto wenye mateso
Machozi ,jasho na damu kwa watanzania /
Ya wote tuwe pamoja tu sali kwa nia/
Tunauwana kama hakuna kesho/
Amani kwa machinga ,wana Apolo,masela wenye mateso/
Machozi,jasho na Damu kwa watanzania /
Na mungu atasikia tusali kwa nia...
VERSE..3.
Kila nikinyamaza naji sikia kusema / kuishikiana mitutu wa Bongo bado mapema/ sijawahi kuona mimi masikio yakizindi kichwa/ ila sasa kwa mbali naanza kuifuta picha/ naota nusu nusu masuala mengi ya vita/ nafikiri kwa kina ni nani ata athirika/ mtoto wa kigongo masomoni London/ au bibi na Babu wanao lima shambani / hatua kwa hatua nadhani huo ndio mwendo/
Mambo yanavyo kwenda hakuna cha uzalendo/ naona hata vibaka Msheli wanajishuku/ ni bora kuiba mabilioni kuliko kuku/ kibaka na mla rushwa nani angeuke mfano/ jasho la mahabusu halimo kwenye mikingamo/ watu wanapofanya maovu bila vificho / ndipo napo gundua Dunia yafika mwisho/ jasho la mlala hoi lazindi kuchuluzuka/ na upande wa pili vigongo wananuka Rushwa/ nakuta kundi la watoto wengi kwenye mitaa/ nauliza wanachofanya wanadai wana ngaga njaa/ tufumbe macho tusadiki tumuombe Allah / serikali imelala na haya si masihara/ wengi wana acha shule wengi wana kuwa malaya/ wengi wanakuwa wezi na wengi wanapata miwaya/ ni nani atairisha yatima kwenye mitaa/ nani atakae zuia Ukimwi unao zagaa/ nani atazuia vita na baa la njaa / eeh Mwenyezi mungu epusha hili balaa..
CHORUS..
Tunaishi kama hakuna kesho/
Amani kwa yatima,kina mama, watoto wenye mateso
Machozi ,jasho na damu kwa watanzania /
Ya wote tuwe pamoja tu sali kwa nia/
Tunauwana kama hakuna kesho/
Amani kwa machinga ,wana Apolo,masela wenye mateso/
Machozi,jasho na Damu kwa watanzania /
Na mungu atasikia tusali kwa nia...
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202