Profesa Jay ndo Mwana hiphop bora wa muda wote Afrika Mashariki

Mfalme wa Hip Hop Tanzania si Afande sele au kuna mapinduzi yalifanyika kimyakimya!?..

Tukiongelea EA huko ni kudanganyana, kuna Fid Q, Weusi, Wakazi, Nash Mc, Khaligraph jones, Octopizzo, Nonini, Jua kali etc nao tuwaweke wapi!?..
 
Yes, maUnderground wanafanaya RAP inang'ara...

Lazima muwe VINARA imara kwenye MSAFARA...

RAP na MAZINGAOMBWE abadani haviendani...

Msitegemee TAWILEE iwaokoe katika FANI...

Ni vyema ukafikiri kabla ya kufanya maamuzi...

Tazama mbele usije ukanywa CHAI kwa mruzi...

Naamini Askari kibao, ni lazima upitie DEPO...

Vinginevyo ndugu yangu utakuwa unapaka rangi UPEPO..

Kama unapata moja kwanini usipate na mia...

Hiyo inawezekana kwa wote mlio na NIA...

Sioni sababu za msingi kuomba kwenye MITAA...

Kama una KIPAJI iweje ufe na njaa...
 
Nyimbo za Prof J, mashairi yake yanatumika Katika fasihi advanced level Kwa wanaosoma kiswahili

Prof Shivji ndiye alimpatia jina la Prof J, baada ya kukutana pale mlimani kwenye kongamano flani Prof J enzi hzo anajiita Nigga J, Prof Shivji baada ya kusikiliza mashairi ya Nigga J, akasema *Mimi ni Prof wa sheria lakini wewe ni Prof wa Muziki* kuanzia siku Nigga J, akaanza kuitwa Prof J,

Prof J ndiye mwamba wa Hip Hop Africa Mashariki na Kati
Hahaha.
Prof mkali kwa vigezo vyako pia!
Au proof imefanyika kuhitimisha kuwa prof ni best mc of all time?

Leta majibu hapa.
 
Professor Jay umeamua kuanzisha thread
Hujui fanani na afande sale wapo humu bila kumsahau mchizi MOX na chid Benz wapo
 
Ungeweka na vigezo vilivokupelekea wewe kumuona hvyo, nadhan ndio ingependeza zaidi.

Binafsi namkubali prof jay km msanii mkongwe na mwenye hamasa katika harakti za kuinguza hip hop miaka ya nyuma... Ila sio kwamba ye ni mkali muda woote.


Nyimbo kali ninazozikubali toka kwake.
Bongo dar es salaam
Heka heka za star.
Kubwa kuliko.




Atabakia kuwa miongoni mwa legends ila sio mkali wa wakati wooote.....

Huu utumbo anaoimba imba siku hizi..

Hapana kwa kwwli.
 
Prof noma sana jamani. wasanii wa kitambo walikua wanajua kuandika mistari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…