Wadau wa muziki maarufu kama Bongo Fleva, mmesikia wimbo mpya wa Prof. J? Unaitwa KamiliGado.
Nahisi Profesa Jay ameanza 'kuzeeka' maana huo wimbo haudhihirishi 'uprofesa' wake. Ameamua kuimba, yeah, autotune and all that but melody ya wimbo ni ya kawaida sana. Mistari pia hain lolote jipya given that anarap kuhusu Mapenzi (atleast angeonesha uniqueness and creativity in rapping about love).
Kwasababu anajua wimbo wake ni mbovu na hivyo unahitaji promo ya ziada, ameamua kuufungulia website (mara ya kwanza kuona wimbo unafunguliwa website) www.kamiligado.com ilhali yeye kama msanii hana website ya kumtambulisha!
The only reason why his song is getting airplay, ni 'kulinda heshima'!
Ushauri wa bure: Nunua mashairi makali ama 'tundika daluga'!