Nilimsikiliza jana Prof.Kabudi,huyu ni mwalimu wangu ninamuheshimu sana.
Jana ametoa somo kubwa sana...akawajibu wale wanaotaka kueneza propaganda kuwa Tundu Lissu kamtukana Mwalimu Nyerere....lakin Kabudi katuonyesha kuwa,bado Lissu alitumia Lugha laini sana,kumbe huko nyuma kuna watu walioifananisha Tanganyika ya Nyerere na Wakoloni,na wakasema hatutaki kuwa koloni la Tanganyika
Na kwamba ujinga wa kizazi cha Mwalimu Nyerere na Karume hauwezi kuwa wa kwetu...ukiwa na akili timamu atamuelewa Tundu Lissu,lkn kwa kumsikiliza Hamphley Polepole na Prof.Kabuti nimapata picha kwanini CCM walikataa wajumbe wa Tume ya Katiba wasiwe sehemu ya Bunge la Katiba.
Aibu ni pale TBC walipozima matangazo wakati Prof.Kabuti akichanachana hoja ya S2 ya Ma-CCM,
Mayalla, nakuheshimu na tena naheshimu mawazo yako!... Nakumbuka saana ulipoendesha kipindi cha kiti moto kwa mafanikio makubwa.Ningekuwa na uwezo wa kumshauri mwalimu wangu, dean wangu, na super visor wangu wa LL.B dissertation yangu, Prof. Palamagamba Kabudi, ningemshauri, aizamishe hii sense ya Tanganyika ndani ya vichwa vya CCM!. Hili ni suala tuu la kuwapatia elimu CCM, waelimike, waachane na ujinga wao wanaotaka kuulazimisha kwenye bunge maalum!.
Asante Prof. Kabudi, kulizungumzia hili.
Thanks.
Pascal.
Mayalla, nakuheshimu na tena naheshimu mawazo yako!... Nakumbuka saana ulipoendesha kipindi cha kiti moto kwa mafanikio makubwa.
Kwani ni huyu Pascal Mayalla au Pasco?
Jambo hili hata wanaopinga wengi wao wanafahamu ukweli huu, (isipokuwa wachache waliozoea kutumika kwa maslahi binafsi kama hawa waliopo huku jf) Cha kusikitisha mkuu wa nchi akaamua kujidhalilisha kutoa alichokiita maoni yake kwa mgongo wa chama. Mh JK angekaa kimya na kutafakari asingeropoka kwa kuelemewa na kelele za chama angejenga heshima, na angefuatilia na kutafakari kwa undani kabla ya kutumika kama chambo kwa kudhani pengine watz wataguswa na maneno ya mkuu wa nchi. Ukweli wanaufahamu ila ndg zangu hawa wamejaa hofu iletwayo na ubinafsi
Wale wanaonufaika na aina ya muundo wa sasa ,hawataki kusikia Serikali 3 Maana masilahi Yao yatapotea,Nchi hii inacopy mengi toka Ng'ambo kwenye Tekinolojia zote inajitahidi kwenda nao kwa kiasi fulani , lakini suala la Muungano hawataki kubadilika wakihofia kupoteza Ulaji wao,Haya masilahi ya Wachache ndio kikwazo kikubwa kwa Serikali 3 ni Wakati wa kuamka tuidai Tanganyika kwa nguvu zote.Wanahitaji ushauli juu ya tanganyika,maana hapo kuna zanzibar + tanganyika =TANZANIA hapo hapo eti wanahitaj serkar 2,zip ss
Ningekuwa na uwezo wa kumshauri mwalimu wangu, dean wangu, na super visor wangu wa LL.B dissertation yangu, Prof. Palamagamba Kabudi, ningemshauri, aizamishe hii sense ya Tanganyika ndani ya vichwa vya CCM!. Hili ni suala tuu la kuwapatia elimu CCM, waelimike, waachane na ujinga wao wanaotaka kuulazimisha kwenye bunge maalum!.
Asante Prof. Kabudi, kulizungumzia hili.
Thanks.
Pascal.
Ulee muungano wa Nyerere na karume japo haukuwa na Hati ulikuwa muungano mzuri hakukua na Ujanja ujanja mwingi Kama Muungano huu wa sasa ambao umepenyeza mambo mengi Kienyeji kienyeji pasipo lidhaa ya Watanganyika matokeo yake Zanzibar wameibuka na Kuwa Nchi Kinyemela, tena kibaya zaidi Pesa ya kujijenga mpaka Kuwa Nchi inatoka Tanganyika,sasa Zanzibar wanawaona Tanganyika ni Mazoba na wapo million 44 lakini Wanapelekeshwa na Wazanzibar million 1.5 tu Kama Kondoo ! zimetumika pesa nyingi sana kwa ajili ya kuubembeleza Muungano ambao hauna faida kwa Watanganyika ,huku ZNZ akifaidika kwa mengi kwani Wamelundika Lundo la Watumishi wa Umma na Utitiri wa Wabunge kisha Wanategemea Mishahara itoke Tanganyika,kwa kweli ZNZ anainyonya Tanganyika hadi wamepitiliza sasa,cha ajabu Wazenji wanakula wakishashiba wanavulumusha Vuvuzela ili kuwapumbaza Watanganyika ambao walikuwa wamelala sasa wameanza kuamka ndio Maana wanaitaka Tanganyika irejeshwe haraka.Dah! Kweli msumari umewaingia. Maana B7 leo siwaoni. Ila kidogo naona chris kwenye mada zingine akili imeanza kurudi.
Anyway ni ukweli uliodhahiri kuwa watanzania wengi uongo kwao ndiyo kweli na iwapo ule uongo walioaminisha watu ukiwekwa hadharani hutengeza chuki za maneno,vitendo,hila na hata mauaji. Huwezi kusema unataka serikali mbili kwa nchi mbili zilizoungana. Leo unakataa Tanganyika je tarehe 9/12 ni kwa ajili ya nchi gani? Mfano katika biashara Mnapoungana inamaana mnakuwa na leseni moja,akaunti moja na inapofikia wakati wa kugawana faida kila mtu anakuwa na akaunti private. Huu ni ujinga wa shule za kata kuunganisha nchi mbili na kuweka serikali mbili. Wakubali kuwa na serikali moja wa tatu.
Shida nyingine ni kujaza wanasiasa kuliko wanasheria
Out of Topic: "nikitaka kui-delete TBCcm kwenye king'amuzi changu cha Azam nafuata taratibu zipi??
Out of Topic: "nikitaka kui-delete TBCcm kwenye king'amuzi changu cha Azam nafuata taratibu zipi??