Profesa Kabudi awasha moto Katiba Mpya

Tiba ya yote ni kubinafusisha TBC kisha mwekezaji aje na watu wake .

Zanzibar ndio wenye shida hawataki tatu hawataki moja wanataka mbili lakini wasiguswe. Yaani seti yao iwe kubwa kuliko ya Tanganyika ikiwa doted ndani ya duara zima la Zanzibar.
 

- Kabudi ni professor wa nini hasa maana sijawahi kumsikia? au mbunge naye kama kuna anayejua anifahamishe maana anaongea kama mbunge wa ukawa au?

Le Mutuz System
 
Mimi nawashangaa sana hawa Wazanzibari CCM wakiwa kwenye BLW wakali kweli kama PILIPILI KICHAA kwamba wanataka serikali 3. Wakija Dodoma wapole sana kama PILIPILI HOHO wanataka serikali 2. Swali la kujiuliza Je, hawa Wazanzibari CCM wataendele kucheze hili shere hadi lini?
 
Wengi mmelisoma hili andiko la THE SO CALLED PROFESSOR kwa mihemko.
Binafsi sioni kama hotuba yenyewe INA hadhi ya kutolewa na professor.
Kama wewe ni professor unashindwa kuiona tofauti ya " TANZANIA BARA NA TANGANYIKA" lazima tuwe na wasiwasi na taaluma yako.
NO WONDER TUNAKUWA NA PRODUCT YA WASOMI WASIO NA ELIMU KAMA AKINA BEN SAANANE. kumbe walimu wenyewe ndio akina PALAMAGAMBA!!!!!!!!!!!!!!
 

Pascal huu ndo muda muafaka wa kuibua kipindi chako cha Kiti Moto.. wahoji wanaS3 na S3...ila usije na misimamo ya mpwa wako Pasco maana yule bana kuna siku uwa anachafua hali ya hewa na kukimbiaa...Ahasanta
 

Pokea BONGE la like!!!
 
Pascal huu ndo muda muafaka wa kuibua kipindi chako cha Kiti Moto.. wahoji wanaS3 na S3...ila usije na misimamo ya mpwa wako Pasco maana yule bana kuna siku uwa anachafua hali ya hewa na kukimbiaa...Ahasanta
Asante Ben, kipindi ilikuwa kirudi siku nyingi, logistics zikikamilika, soon mtakiona hewani, ila ni kwa jina jingine!. Pasco achana nae kabisa, hana maana kabisa!, yeye kila siku anang'ang'ana na ukweli tuu, as if hajui siasa zetu ni za uongo uongo!. Afadhali yangu, kwenye ukweli nitasema, ila kwenye uongo nitajinyamazia!.

Paskali
 

Funza
Nashukuru wewe umeulewa aina ya muungano tulio nao... muungano wa Changu Changu, Chako Chetu. CCM wameshindwa kuzuia hali hiyo Zanzibar na kuiruhusu kuwa nchi, sasa wanataka sisi tubebe upuuzi wao. Hatutaki - Tanganyika Daima.

Tunataka Muungano wenye usawa wa nchi mbili, na serikali ya muungano. Mapato na mchango kwa serikali ya muungano uwe kwa uwioano. Sio kuinyonya Tanganyika, halafu wanajidai eti wao ni koloni letu. Ni either waue ZNZ tuwe na serikali moja ya Tanzania au tuwe na serikali tatu.
 

Kama umewaangalia wengi mi wajinga wajinga tu wachumia tumbo, hakuna cha maana wanachoongea pale zaidi ya kufikiria watajaza vipi choo.
 
Mkuu nimekuona leo TBC kwenye marudio ya kipindi fulani, nafikiri mlikuwa Mnazi mmoja. Unaelezwa na yule mama Umi kwamba hati za kuridhia muungano zipo za pande zote za muungano. Ulishindwa kumuuliza hata swali moja kwa hiki ambacho kimelalamikiwa hata na mzee Jumbe aliyekuwa mjumbe wa BMZ kwa miaka 20? Matter of fact, Pasco wa JF is doing better than you.
 
This time sujui ccm na usalama
wao wa taifa watamng'oa meno na kucha nani kwa maana kila kona ya nchi
mambo yamebana ba watu wanataka Tanganyika na Zanzibar yao...

Mm nipo tayari kung'olewa kucha na meno bila ganzi lakini Tanganyika yangu itarejea
 
Mkuu Gagi, nakubaliana na wewe kabisa, mimi na Pasco wa jf ni watu wawili tofauti, mimi nafanya kitu kinaitwa "responsible journalism", nikipeleka kipindi TBC, nitauliza aina ya maswali yale tuu yakuvumilika TBC!. Responsible Journalism, ni uandishi/utangazaji wa uwajibikaji, hivyo nikipeleka kipindi TBC nakuwa responsible na TBCIISIM!. Pasco wa jf, hatumwi na yoyote, hamtumikii yoyote na hawajibiki kwa yoyote, yaani hayuko responsible kwa yoyote na yuko answerable to no one, hivyo anawezsa kusema lolote, chochote, popote, hajali kitu!, mimi najali!.
Paskali.
 
Utaniwia radhi mkuu wangu. Kama hii ndiyo responsible journalism, unafikiri kutakuwa na uhalali wowote wa kuendelea kuwa na nyie kama watumishi wa umma siku ccm ikiondolewa? Tunawafuatilia kwa uamkini msioweza kufikiria.
 
tunataka Tanganyika !!!!!!!!!!!!!!??
 
Pascally na wengine.....Kama uwasilishwaji wa Rasimu ungefanywa na Prof. Kabudi.....naamini pale Dodoma pasingelitosha, na ndio maana Deputy Speaker wa Bunge la JMT yuko very focused ktk hii issue, ujio wa mchakato, gharama na target all were wrong. Waamuzi hawakuwa ktk right track.....Professor Kabudi amenijibu kitu muhimu kilichoniumiza sana juu ya Waingereza na Tanganyika? Amethubutu kuifunua history ya nchi kwa umakini na dhati.....anachokosea Lissu ni maumbile yake kubeba sura ya jazba ktk uwasilishwaji wa hoja zake....ni maumbile, anahitaji Mshauri wa kumjenga udhibiti wa jazba na kuuvaa uhusika tuli, wenye lishe ya kweli ichagizwayo na minofu ya utajiri alojaaliwa wa hoja makini.

Prof. Kabudi aliwamiliki hadhira ile kwa hoja, upole, utafiti, vielelezo, kweli na udhati wake ulioikana papara na jazba.

Kabudi is someone needed by Samuel J. Sitta kuwaweka sawa wabunge juu ya rasimu.
 
Kuitambua Tanganyika kunazua hofu nyingi.
Lakin hofu zote zinatokana na watu kupenda utawala wa kudumu.
Mfano ni huu: Serikali tatu zitafufua upya wafu wawili ( TANU & ASP) hii maanayake nini? Hii iyasababisha kufa kwa kiumbe hai (CCM). Ikiwa hivo kitakachofata nini? Kitakachofata ni kutengeneza upya Katiba ya TANU yenye kuridhiwa na wengi. Baada ya hili kufanyika nadhani wote tunajua kitakachotokea!!? (Miungu watu katika Chama na Serikali watakua wamekatwa makali). So chakufanyika, ni kuipinga ibara hii ya muundo wa muungano kwa Nguvu zao zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…