Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Matumaini na imani ya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), yamebaki vile vile kama ilivyokuwa miaka 25 iliyopita, baada ya kumchagua tena Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti wao taifa.
Profesa Lipumba anaukwaa wadhifa huo, baada ya kupata kura 216 katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho, akiwashinda wenzake saba waliokuwa wakichuana katika nafasi hiyo.
Soma, Pia: Profesa Lipumba ajitosa kwenye kinyang’anyiro cha Uenyekiti CUF
Hii inampa nafasi mwanasiasa huyo aliyebobea katika masuala ya uchumi ya kukiongoza chama hicho kwa miaka mitano ijayo na hivyo kuweka historia ya kuwa Mwenyekiti wa chama cha siasa kwa miaka 30 nchini.
Katika uchaguzi huo, uliofanyika jana Jumatano, Desemba 18, 2024, Profesa Lipumba ameshinda kwa kura 216 kati ya kura 592 halali zilizopigwa.
Kura zote zilizopigwa zilikuwa ni 596, kati ya hizo kura halali 592 na kura nne (4) ziliharibika
Katika uchaguzi huo uliokuwa na wagombea tisa (9) wagombea wengine walikuwa ni Ali Juma Khamis ambaye alijitoa 'dakika za mwisho', mgombea wa pili alikuwa ni Athman Kanali aliyepata kura tano (5), Hamadi Hamadi alipata kura 181, Juma Shaban alipata kura sita (6), Maftaha Abdallah Nachuma alipata kura 102, Wilfred Lwakatare amepata kura 78, Ngaitile Siwale amepata kura mbili (2) na Chifu Lutalosa Yemba amepata kura mbili (2)