#COVID19 Profesa Lipumba apata chanjo ya Covid-19, ashauri wananchi wachangamkie fursa

#COVID19 Profesa Lipumba apata chanjo ya Covid-19, ashauri wananchi wachangamkie fursa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Lipumba pc

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepata chanjo ya kwanza ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Profesa Lipumba amepata chanjo hiyo leo Jumatano Julai 22,2021 katika kliniki ya Umoja wa Mataifa zilizopo Masaki.

Akizungumza na waandishi baada ya kutoka kupata chanjo hiyo amesema amejikuta akipata nafasi hiyo kupitia mke wake, Gojina Mtenga, anayefanya kazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto Duniani(Unicef), Cox Bazaar nchini Bangladesh.

"Kama mlivyosikia wenzetu wa mashirika haya ya kimataifa wameruhusiwa kuanza kupata chanjo hizi pamoja na familia zao.

"Hivyo na mimi kupitia mke wangu ndio imeniwezeaha leo kuja kupata chanjo hii hapa na nilipata taarifa usiku wa jana ikinitaka nifike hapa leo saa tano asubuhi nashukuru kwa kulikamisha hili, "amesema Profesa Lipumba.

Hata hivyo amesema baada ya chanjo hiyo ya awali anatakiwa arudi tena baada ya wiki sita mpaka nane kupata chanjo ya pili ili kukamilisha chanjo nzima ya kujikinga ya kujikinga na ugonjwa huo.

Pia mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuchangamkia chanjo hiyo ili kuwa salama.

Wakati kwa upande wa Serikali ameishauri iangalie namna ambayo itawezesha wananchi wanaougua ugonjwa huo kupata matibabu kwa yake kwa gharama nafuu.

MWANANCHI
 
Kakisaliti chama chake cha Cuf sasa anataka kufanya usaliti mwengine kwa wananchi naona.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Huyu msimsikilize haaminiki katu. Si ajabu hiyo ni gheresha. kama aliweza kukisaliti chama chake na umati wa watu nyuma yake, msimuamini nyie kenge, maana watanzania muda mwingine ni makenge (siyo wote) BAK
 
Kama Lipumba ni profesa kweli, basi elimu yetu haina maana kabisa kweny ukanda mzima wa Afrika mashariki.
 
Huyu jamaa ana PhD ya uchumi kutoka chuo kikuu Stanford nchini marekani, wamarekani wenyewe wanapigana vikumbo kupata chance ya kusoma hapo Stanford, lakini mwamba alitoboa huko
View attachment 1863345
Du aisee... Sasa imekuaje profesa mzima awe kilaza hivi. Au wazungu wanamtumia kwa malengo yao fulani kupitia upinzani njaa.
 
Huyu msimsikilize haaminiki katu. Si ajabu hiyo ni gheresha. kama aliweza kukisaliti chama chake na umati wa watu nyuma yake, msimuamini nyie kenge, maana watanzania muda mwingine ni makenge (siyo wote) BAK
Unawaita waTZ makenge the same time unawahitaji wakuunge mkono kwenye madai yako ya katiba mpya!!! Hivi mtu unayemuita kenge then kesho unamuomba akuunge mkono atakubaliana na wewe? Kuna sababu gani ya kuwaita waTZ makenge hata kama unatofautiana nao kwenye mitazamo?
 
Hapo ndipo napochanganyikiwa....
 
Du aisee... Sasa imekuaje profesa mzima awe kilaza hivi. Au wazungu wanamtumia kwa malengo yao fulani kupitia upinzani njaa.
Tatizo la kwanza ni njaa la pili ni fursa, kwa mazingira yetu wanaosoma sana hata vyuo vile vya juu kabisa nje ya nchi wakirudi nyumbani ni ngumu sana kuona fursa za kutumia elimu yao.

Sana sana atafundisha vyuoni ambako na kwenyewe hakuna hela kama alizokuwa anategemea au utamkuta anaenda na upepo wa siasa na huko kwenye siasa ndio huwa wanajitoa ufahamu ilimradi tu apambane na njaa yake.
 
Back
Top Bottom