GE2025 Profesa Mkumbo azisaka kura hadi kwenye mabanda ya kubeti, Je ataendelea kuwatembelea akiupata ubunge?

GE2025 Profesa Mkumbo azisaka kura hadi kwenye mabanda ya kubeti, Je ataendelea kuwatembelea akiupata ubunge?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Nimemuona Mgombea ubunge jimbo la Ubungo Profesa Kitila Mkumbo akifanya shughuli za ujenzi, lakini pia amefika hadi ofisi za kubeti ili kuomba kura kutoka kwa wananchi hao

Sasa swali je ataendelea kuwatumikia zaidi wananchi hata pale atakapoupata huo ubunge au ndio danganya toto?
================

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Mapinduzi Professa Kitila Mkumbo ameendelea na kampeni zake kwa kufanya ziara ya mtaa kwa mtaa katika Kata ya Mburahati. Ziara hiyo ilihusisha mikutano na makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo Bodaboda, Mama ntilie, wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali katika mitaa ya NHC, Barafu na Kisiwani.

Akiwa katika ziara hiyo, Prof. Mkumbo aliomba wananchi kumpa kura ifikapo Oktoba 29, 2025, ili aweze kuendelea kulitumikia Jimbo la Ubungo sambamba na kumpigia kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.

 
Back
Top Bottom