Profesa Mkumbo: Serikali yatengeneza ajira milioni 8 ndani ya miaka 5

Profesa Mkumbo: Serikali yatengeneza ajira milioni 8 ndani ya miaka 5

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Serikali imesema katika kipindi cha kuanzia Novemba 2020 hadi Februari 2025, jumla ya ajira 8,084,204 zimezalishwa nchini. Kati ya hizo zipo zitokanazo na sekta rasmi na isiyo rasmi.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025/2026 iliyowasilishwa leo, Juni 12, 2025 Bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo.

Kati ya ajira zilizozalishwa, wanaume walikuwa 4,125,987 (asilimia 51.0) na wanawake walikuwa 3,958,218 (asilimia 49.0) ya ajira zote zilizozalishwa kwa kipindi husika. Aidha, kiasi cha ajira 1,047,179 (asilimia 13.0) zilizalishwa katika sekta rasmi, na ajira 7,037,024 (asilimia 87.0) zilizalishwa katika sekta isiyo rasmi.

1749730636325.png

Source:mwananchi
 
Mama si kasema serikali haina wajibu wa kuajiri vijana sasa hizo kazi wewe Mkumbo umezitoa wapi lakini eenh?
 
Kwa mwendo huu mpaka 2030 tutakuwa na ajira nyingi kuliko idadi ya wananchi wanaoweza kuajiriwa 🙌
 
Back
Top Bottom