BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Profesa wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mohamed Bakari amekitahadharisha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuwa makini na kikosi kazi, kwani kinaweza kuwa njia ya kuchelewesha maridhiano.
“CHADEMA wako sahihi kususia kikosi kazi kwa sababu hakina uhalali wa kisheria na kikatiba kama vyombo vingine, lakini kama tunataka tu kufanya mazungumzo basi ni jambo la heri.
“Ni njia fulani ya kufikia maridhiano, kwa hiyo kama kuna jambo zuri tutaliona. Lakini kikosi kazi kisije kikawa ni mkakati wa kuchelewesha hayo maridhiano yenyewe,” alisema.
Kauli ya Profesa Bakari imeungwa mkono na mchambuzi wa siasa, Bubelwa Kaiza aliyesema, “kikosi ni jitihada binafsi ya Rais Samia, kukisubiri kikosi kazi ni sawa na kukubaliana na Rais kuongoza nchi kwa maoni yake binafsi.
“Kwa kuwa CHADEMA hawako kwenye kikosi kazi, waendelee na kazi zao kwa kuwa zinatambuliwa na sheria na Katiba,” alisema.