Profesa Mukandala kushindwa kutamka neno Wahafidhina nini tatizo?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Wanangu hamjamboni?

Sijui niuite usomi, ujinga, ukoloni wala sijui. Wakati akisoma utangulizi wa Kitabu cha Mzee Ali Hassan Mwinyi, Profesa Rwekaza Mukandala alishindwa mara mbili kutamka neno wahafidhina. Ingekuwa kashindwa kutamka neno la kimombo ungesikia stori kibao.

Je, hii inamaanisha nini wanangu?
 
La yaani ndio umeona kitu muhimu kutuletea hapa?
 
La yaani ndio umeona kitu muhimu kutuletea hapa?
Hata mie nashangaa yaani hii nayo ameona aanzishe uzi. Watu kuna maneno kibao huwa yanatushinda kutamka tena ni ya kiswahili. Sioni kama ni issue sana.
 
Neno hilo lina mzizi wa kiarabu ni aghalabu jamii nyingi za waafrika walioanza kujifunza lugha zao za asili kabla ya kiswahili kupata shida kutamka maneno ya kiswahili yenye asili ya kiarabu, Prof Mukandala ni Muhaya.--- Hakuna cha ajabu hapo.
 
Wala hakuna tatizo watu wengi tu hawawezi kulitamka hilo neno labda kwa kulisoma, neno lenyewe limekaa Kiarabu mno (wahafidhina).
 
Sasa na wewe hilo neno uliloanza nalo tuite ni ufala au tukuite kilaza? Unajiona unajua kumbe hujui!
 
Wachangiaji wengi kwenye mada hii ni utopolo! Kwa nini tunalazimisha kutomwelewa mleta mada? Anacholalamikia ni mazoea ya Watanzania kuwazodoa wanaoshindwa kutamka maneno ya Kiingereza huku tukiwaacha wanaoshindwa Kiswahili! Mliona Mh. Jiwe aiposhindwa kusema "Front Page " na kusema "Font Fed" na pia aliposhindwa kutamka "Entrepreneurship". Mapeji na Mapeji yalijaa hapa JF na kule twittani! Hapo ndipo hoja ya mleta mada ilipojificha "kwa nini tuwabeze wa Kiingereza na kuwapotezea wa Kiswahili?"
 
Kwani yeye ni malaika ajue kila kitu kwamba asikosee.

Rubbish
 
Wahaya wengi hawajui kiswahili kabisa, ng'ombe wanaita gombe na vituko vingine
 
huo ndio unyumbu sasa katika uhalisia wake.
 
Sure mkuu
 
Nafikiri watz labda tujaribu zaidi, kuelekeza nguvu zetu nyingi kwenye issues ambazo ni 'objective' 'kwa maendeleo, na jinsi ya kutatua changamoto than kuwa 'too subjective' .... tumechelewa sana.
yalitokea kwa marehem,mpaka wasomi watu wazima wakajikita kwenye jambo lile.

inawezekana hata katika maisha binafsi tunafeli kwa sababu hizi hizi.
 
Neno hilo lina mzizi wa kiarabu ni aghalabu jamii nyingi za waafrika walioanza kujifunza lugha zao za asili kabla ya kiswahili kupata shida kutamka maneno ya kiswahili yenye asili ya kiarabu, Prof Mukandala ni Muhaya.--- Hakuna cha ajabu hapo.
Hata KP leo neno hilo hilo limempa chenga kidogo kwenye PB.

Anyway ulimi hauna mfupa.
 
Hilo nalo ni la kujadili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…