Wachangiaji wengi kwenye mada hii ni utopolo! Kwa nini tunalazimisha kutomwelewa mleta mada? Anacholalamikia ni mazoea ya Watanzania kuwazodoa wanaoshindwa kutamka maneno ya Kiingereza huku tukiwaacha wanaoshindwa Kiswahili! Mliona Mh. Jiwe aiposhindwa kusema "Front Page " na kusema "Font Fed" na pia aliposhindwa kutamka "Entrepreneurship". Mapeji na Mapeji yalijaa hapa JF na kule twittani! Hapo ndipo hoja ya mleta mada ilipojificha "kwa nini tuwabeze wa Kiingereza na kuwapotezea wa Kiswahili?"