Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Aliyekuwa CAG wakati wa Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli Profesa Mussa Assad Amesema ya kuwa Mshahara wake kabla ya Makato ulikuwa ni Milioni 7 . Ambapo Baada ya Makato alibakiwa na Million 5.
Amesifia Nafasi hiyo kwa kusema ni nafasi yenye marupurupu manono,Gari zuri na Tamu aina ya V8 lenye kila aina ya Raha na starehe .
Ambapo Masrahi ya kwenye U CAG yalikuwa ni Manono na matamu ukilinganisha na alipokuwa akifundisha chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo alikuwa akilipwa Million 4 kama Profesa Wakati Huo.
Bila shaka nazani sasa kila mmoja anaweza kuelewa kwanini wengine Ma Profesa haamua kupumzika kufundisha vyuoni na kuingia katika Siasa ili walau wapate kupumzika na kupumzisha Mishipa ya shingo ya kuongea na kuzungumza kwa muda mrefu madarasani wakati mwingine kwa kurudia rudia mpaka wanafunzi waelewe.
Kikubwa ni kuwa kama unaona sehemu haikulipi basi wewe hamia unapoona moyo wako utakuwa na Amani na siyo kulialia tu kama kengele. Na lazma tufahamu kuwa Duniani kote mishahara haiwezi kufanana kwa watumishi wote.
Hivyo kila mmoja aridhike na alipo au aende na kutafuta nafasi ya kwenda anapoona panamfaa . Lakini kwa nyongeza ni kuwa Hakuna Mshahara unaomtosha mtu na ndio maana ni vyema sana ukaridhika na unachokipata na kadri unavyopata ndivyo hamu yakupanda juu na kupata sana inavyoongezeka.
Na ndio Maana hadi leo Elon Musk licha ya utajiri wake bado anaendelea kutafuta Zaidi na zaidi. Ndio maana pia Reginald Mengi alikufa huku akiendelea kutafuta hela . Ndio Maana pia akina Aliko Dangote pamoja na utajiri wao bado wanataka kupata pesa nyingine zaidi na zaidi.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.