Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini(CCM),Profesa Patrick Ndakidemi ,ameitaka wizara ya Mifugo na uvuvi kuanzisha wakala wa mifugo na uvuvi ili kuweza kusimamia sekta hiyo kwa ufanisi zaidi.
Profesa Ndakidemi alikuwa akichangia makadirio ya mapato na matumizi kwenye bajeti ya wizara ya Mifugo na uvuvi kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 bungeni mjini Dodoma jana.
Akichangia mjadala huo,Profesa Ndakidemi alisema kuwa kuanzishwa kwa wakala hizo zitamsaidia Waziri mwenye dhamana pamoja na wizara kwa ujumla katika kushughulikia changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.
Profesa Ndakidemi pamoja na kuishukuru serikali kwa kuongeza bajeti ya wizara hiyo na kufikia shilingi Bilioni 460,alisema bajeti hiyo haitoshi
Alisema sekta ya Mifugo na uvuvi inahitaji pesa nyingi kwa ajili ya kutekeleza mageuzi Katika kuongeza utafiti,chanjo,huduma za ugqni na vizimba na kushauri serikali kuongeza fedha kama ambavyo kamati yao ilivyopendekeza.
Aliishukuru serikali kwa kusaidia mradi wa shamba Darasa la Kuku Katika kata za Uru kaskazini na Kibosho Magharibi jimboni kwake.
Pia aliishukuru serikali kwa mradi wa Josho na kuomba majosho zaidi Katika kata ya Arusha chini.
Katika hatua nyingine Profesa Ndakidemi ameiomba serikali kusaidia upatikanaji wa mbegu Bora za mitamba zitakazosaidia upatikanaji wa maziwa mengi hasa ukanda wa juu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema mkoa wa Kilimanjaro umebarikiwa kuwa na mazingora mazuri yanayowezesha ufugaji wa Ng'ombe wanaoweza kutoa maziwa kati ya lita 20 hadi 40 kwa siku huku akiomba pia serikali kurahisisha upatikanaji wa mbegu Bora za marisho kwa ajili ya kupeleka maeneo husika.
Kuhusu mradi wa vizimba vya Samaki, Profesa Ndakidemi alishauri serikali kuwakopesha vizimbq miongoni mwa vizimba 497 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana ya namna ya kufuga Samaki kwa kutumia Teknolojia ya vizimba.
Akaishauri serikali kuajili maofisa ugani wengi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wananchi wa ukanda wa chini jimboni kwake juu ya ufugaji wa Samaki Hawa kwa wakulima wa mpunga Katika kata Kahe na Mabogini.