Profesa Ndakidemi Alia na haki za wazee Bungeni

Profesa Ndakidemi Alia na haki za wazee Bungeni

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi, amesema ukatiri dhidi ya wazee yakiwamo mauaji kwa baadhi ya mikoa,ni moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wazee hapa nchini.

Kutokana na Hali hiyo, Profesa Ndakidemi ameishauri serikali kwa kushirikiana na viongozi wa dini pamoja na waandishi wa habari kuhamasisha jamii kuacha kuwafanyia ukatiri wazee.

Profesa Ndakidemi alikuwa akitoa mchango wake Bungeni mjini Dodoma kwenye vikao vya bunge la Bajeti ambako amesema Taifa bado linawahitaji wazee kutokana na mchango wao mkubwa kwa Taifa.

Profesa Ndakidemi alishauri serikali kuongeza vituo vya kulelea wazee wasiojiweza na kushauri kila kanda iwe na vituo vya aina hiyo na kupendekeza wakuu wa wilaya na mikoa kuanzisha majukwaa ya kusikikiza kero za wazee kwa kukaa nao na kuhadilishana mawazo.

Kuhusu sera ya wazee,Profesa Ndakidemi amesema sera ya wazee ya Mwaka 2003 imepitwa na wakati na kushauri serikali kuiboresha kwa kutunga sheria ya wazee ili kuwapatia haki zao kisheria na kisera.

"Mheshimiwa mwenyekiti pamoja na kwamba wazee ni hazina lakini bado wanachangamoto nyingi sana hasa ambao hawakuwa na ajira na hawana pensheni"

"Wazee ambao hawakuwa kwenye ajira na wameshazeeka wako kule Vijijini hawana pesa za kujikimu hata kununua chakula imekuwa ni shida"

Alishauri serikali kuwapatia kadi za matibabu wazee wote ambao hawajiwezi ikiwamo Bima ya afya itakayotibu magonjwa yote okiwamo shinikizo la damu, sukari na magonjwa ya kupoteza kumbukumbu.

Alisema si haki kwa serikali kutoa kadi kwa makundi machache na kuliacha kundi kubwa la wazee wengi likitaabika bila msaada na kwamba kadi laki tano kwenye kundi la wazee Milioni tano haikubaliki.

Aliitaka serikali kuwapatia pensheni wazee wote kama ambavyo serikali ya mapinduzi Zanzibar imefanya ambako wazee wote wanapewa sj, 70,000 kila mwezi n kuhoji Zanzibar wameweza kwa nini bara wsshindwe na kushauri suala Hilo liwe la muungano ili wazee wote wanufaike na pensheni hiyo.
 
Back
Top Bottom