Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 6,106,516,794.00 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Kata ya Old Moshi Mashariki katika Jimbo la Moshi vijijini.
Hayo aliyasema Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za Kata ya Old moshi Mashariki uliohudhuriwa na Diwani wa Kata hiyo Jane Mandara, Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhan Mahanyu, viongozi wa CCM na Serikali kutoka Kata ya Old moshi Mashariki .
Mkutano huo pia uliwashirikisha Maofisa kutoka Mamlaka ya Majisafi na uondoshaji majitaka(MUWSA)ambako Ofisa uhusiano wa mamlaka hiyo, Flora Nguma alihudhulia.
Profesa Ndakidemi alisema kuwa maendeleo makubwa ya miradi ya afya, elimu, barabara, pamoja na maji yaliyofanyika kwenye kata ya Old Moshi Mashariki kwa miaka minne kwa kupitia fedha walizopewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mkubwa kutoka Mbunge na Diwani wa Kata hiyo, Jane Mandara na viongozi wa Chama na Serikali Wilayani na Mkoani Kilimanjaro pamoja na watendaji wote wa Serikali.
Profesa Ndakidemi amesema kuwa kwa kipindi cha miaka minne serikali imetoa Shilingi bilioni 6,106,516,794.00 kwa miradi ya maendeleo katika kata ya Oldmoshi Mashariki.
Mbunge aliishukuru sana serikali kwa kuwajengea wananchi wa Old moshi Mashariki shule ya Sekondari ya wasichana ya Kidato cha 5 na 6 iliyoigharimu Shilingi Bilioni moja ambapo katika ukaguzi wa mradi huo, Mbunge aliridhishwa na ujenzi wa kiwango cha juu uliofanywa na mafundi wenyeji.
Prof Ndakidemi amewataka wananchi wa Oldmoshi Mashariki waendelee kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwenye kata yao na kuwaomba kuepukane na propaganda za aina yeyote ile zinazolenga kuchelewesha maendeleo katika jamii yao. Katika mkutano huo, Mbunge Ndakidemi aligawa miche bora ya migomba kwa wananchi.
Wananchi wengi waliopata fursa ya kuongea katika mkutano huo, walieleza kukerwa na tatizo la upatikanaji wa maji katika Kata hiyo.
Akijibu kero hiyo, mwakilishi wa MUWSA, Flora Nguma alisema kwamba taasisi yao itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya Maji katika Kata ya Old Moshi Mashariki.
Aliwaomba wananchi na viongozi wa Vijiji na Kata kutoa ushirikiano ili kufanikisha azma yao badala ya kupinga mipango kabambe ya Serikali ya kuwapatia wananchi huduma ya maji.
Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhan Mahanyu amewataka wananchi wa Kata ya Old Moshi Mashariki kushirikiana na Mbunge na Diwani ili waendelee kunufaika na neema ya miradi kutoka katika serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.