Leo wakati akiongea katika mdahalo uliofanyika UDSM, mhadhiri mwandamizi wa sheria profesa Issa Shivji ameeleza kuwa mkataba wa uendeshaji bandari kati ya Tanzania na Dubai una dosari kutokana na vifungu vilivyotajwa hapo juu kukinzana na matakwa ya kikatiba ya Tanzania. Na akaeleza kesi inaweza kufunguliwa mahakamani kuwa Bunge limepitisha azimio ambalo ni batili kwa sababu linaashiria uvunjwaji wa katiba.
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Rais wa Tanzania ana mamlaka ya kusitisha (revoke) hati yoyote ya ardhi wakati wowote kwa mujibu wa sheria. Vifungu vya mkataba wa uendeshaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai hapo juu (inawezekana) vinaenda kinyume na mamlaka hayo ya Rais, yaliyowekwa kilkatiba kwa kuingilia/kuzuia mamlaka yake halali. Je, kama ni kweli, jambo hilo sio uhaini wa kwa mujibu wa katiba hiyo hiyo? Na kama ni kosa, adhabu yake ni nini?
Kwa mnaojua sheria naomba mnisaidie kuelewa.